Wanafunzi wa kubadilishana kutoka SISU
Chen Jingqi(kushoto) na Ling Jiayi(kulia)
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China
12 February 2025 | By 凌佳艺 Njoki ,陈静祺 Zuhura | SISU
Sherehe hiyo iliyofanyika Januari 24 mwaka wa 2025 ilianza majira ya saa 11:30 jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo balozi wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Chen Mingjian, Waziri wa mambo ya Nje, Mheshimiwa Kombo, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Dkt. Mahakala, pamoja na wanadiplomasia wa nchi mbalimbali, wawakilishi wa mashirika ya Kichina nchini Tanzania, na zaidi ya wageni 200 wa jamii ya Wachina wanaoishi nchini Tanzania.
Hafla hii ililenga kuimarisha uhusiano wa kirafiki kati ya China na nchi nyinginezo (hususan Tanzania), kukuza biashara na ubadilishanaji wa tamaduni, na kutoa jukwaa la mshikamano kwa jamii ya Wachina wanaoishi Tanzania kusherehekea sikukuu kwa pamoja.
Katika hafla hiyo, Balozi Chen Mingjian aliwatakia wageni waheshimiwa heri ya Mwaka Mpya wa China. Alikumbuka mafanikio kuhusu maendeleo ya China katika mwaka uliopita na uboreshaji wa uhusiano kati ya China, Tanzania na Afrika, na kutakia matarajio mazuri kuhusu Kushikamana Kuhimiza Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa Kichina na Kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja. Aliwatia moyo Wachina wanaoishi hapa Tanzania kufanya kazi kwa bidii na kutoa michango katika urafiki baina ya China na Tanzania.
Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, alisoma salamu za Mwaka Mpya kutoka Rais Hassan na alisema kwamba Tanzania iko tayari kushikamana na China kuhimiza matokeo ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), na kuimarisha uhusiano wa kimkakati kati ya nchi hizi mbili.
Pia Ubalozi uliandaa sherehe ya sanamu ya Mwaka Mpya wa Kichina, mashindano ya kushani vitendawili vya taa, na tamasha la vyakula vya Kichina, ili kuwaleta wageni wapate uzoefu wa utamaduni wa Kichina kwa ukaribu.
Wanafunzi na walimu kutoka Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walitoa burudani mbalimbali, palikuwa na dansi ya "Xiao", muziki wa guqin wa "Jiukuang", na wimbo wa kwaya "Kesho Itakuwa Bora". Hali ya sherehe ilikuwa ya furaha tele na nderemo kubwa.
Baada ya hiyo, wageni walifurahia chakula cha jioni pamoja, wakibariki ustawi wa China na maendeleo ya uhusiano kati ya China na Tanzania.
Mjumuiko huu uliongeza hisia za wanafunzi hao wa kigeni kujisikia nyumbani katika nchi hii ya kigeni.
Chen Jingqi, Mwanafunzi wa Lugha ya Kiswahili, aliyeanza masomo katika chuo hicho cha Shanghai mwaka 2022, alikuwa na haya ya kusema:
"Kushiriki katika hafla ya mwaka mpya ya ubalozi wa China nchini Tanzania ni tukio kubwa katika maisha yangu ya kusoma nje ya nchi. Kama mwanafunzi wa kimataifa, kushiriki katika tukio lenye sifa halisi za Kichina kunanifanya nijisikie fahari kubwa. Mazingira ya hafla yalikuwa yamejaa vipengele vya Kichina, na eneo la makazi ya ubalozi kando ya Bahari ya Hindi lilifanya mandhari kuwa maridadi. Tulisherehekea Mwaka Mpya kwa pamoja, huku tukijadili kuhusu tamaduni na uzoefu wa maisha. Kupitia tukio hili, niliweza kuelewa urafiki kati ya China na Tanzania kwa undani zaidi na nikapata msukumo mkubwa wa kusambaza utamaduni wa Kichina nje ya nchi."
Ling Jiayi, Mwanafunzi wa Kiwango cha mwaka 2022, Lugha ya Kiswahili, SISU:
"Mwaka Mpya wa Kichina ni sikukuu muhimu kabisa kwa watu wa China, na hafla ya mwaka huu katika ubalozi ilinifanya nihisi tofauti sana. Kama mwanafunzi wa kupelekeana nchini Tanzania, kusherehekea pamoja na marafiki kutoka mataifa mbalimbali kulinifanya nijisikie furaha sana katika sikukuu hii. Palikuwa na maonyesho ya “Wushi” ya Kichina, na wanafunzi wa Tanzania walicheza dansi pamoja na nyimbo za Kichina, jambo hili lilinivutia sana. Pia, nilipata nafasi ya kukutana na Balozi Chen Mingjian na Mheshimiwa Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambao nimewaheshimu sana kwa muda mrefu. Kwa kupitia sherehe hii ninajihisi kuwa nina uhusiano wa karibu zaidi na nchi yangu, na kujivunia zaidi haiba ya utamaduni wa Kichina."
Katika mazingira ya uhusiano imara na unaoendelea kati ya China na Tanzania, hafla ya mwaka mpya iliyoandaliwa na ubalozi ni hatua ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili, inasaidia kuzidi mawasiliano miongoni mwa China na sehemu mbalimbali za Tanzania. Hafla hii siyo tu ni sherehe ya mwaka mpya wa Kichina, bali pia ni ishara ya urafiki kati ya China na Tanzania, ikichangia mawasiliano ya utamaduni, kuongeza maelewano na heshima baina ya pande zote. Iliwapa Watanzania na watu wanaotoka nchi nyingine nafasi ya kufahamu zaidi utamaduni wa kujadi wa kichina. Pia, ni fursa kwa wanafunzi wa kupelekeana kuhisi hali ya sherehe ya Kichina wakiwa mbali na nyumbani.
Zaidi ya hayo, kabla ya Mwaka Mpya, ubalozi uliandaa mkutano kuhusu wanafunzi wa China wanaokaa nchini Tanzania. Balozi Chen Mingjian, Mshauri Che Zhaoguang, na Mwalimu Xu Yongliang anayetoka Idara ya Utamaduni walikutana na wanafunzi, walielewa hali yao na kuwahimiza kutumia Kiswahili vizuri ili wawe daraja la urafiki kati ya China na Tanzania.
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China