Ramani na Maelekezo

Ramani ya Chuo

Tafadhali tumia ramani yetu ya mtandao (http://map.shisu.edu.cn ) ili uweze kutazama mandhari na majengo makuu ya SISU na majirani zake. SISU ina matawi mawili mjini Shanghai; yaani, Hongkou Campus na Songjiang Campus.

Kusafiri Shanghai kwa Ndege

Shanghai ina nyanja mbili kuu za ndege, ambazo ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pudong na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hongqiao, ukipenda kujua zaidi, tafadhali piga +86 (21) 96990.

Baada ya kufika uwanja wa ndege, unaweza kutumia basi, metro, treni ili kusafiri hadi mjini. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hongqiao uko karibu zaidi na SISU. Ukisafiri kwa teksi kutoka Pudong hadi SISU, itakuchukua mwendo wa kama saa 1 hivi (umbali ni kilomita 44, na gharama ni yuan 150 hivi), ukitumia basi au metro, itakuchukua mwendo wa kama saa 2 kufika SISU (Hongkou Campus).

Maelekezo ya Gari

Ukitaka kufika SISU (Songjiang Campus) kutoka mjini, uwanja wa ndege au mahali pengine, unaweza kufuata maelekezo ya ramani ya mtandao ya Gaode au Baidu. Zote unaweza kupata kwa urahisi katika duka lako la Google Play Store au Apple App Store.

Usafiri kwa Mfumo wa Umma

Shanghai ina mfumo madhubuti wa usafirishaji abiria wa umma, yakiwemo mabasi, teksi na metro zilizopangika vizuri. Kadi ya ya abiria ya mfumo wa umma inatumika katika kila moja ya vyombo hivi hapa juu ila teksi.

Treni ya Metro

Unaweza kwenda Hongkou Campus kwa metro nambari 3, na kushuka katika Kituo cha Barabara ya Chifeng (Chingfeng Road) au Kituo cha Uwanja wa Soka wa Hongkou (Hongkou Soccer Stadium) na kubadilisha hadi u metro namba 8 katika kituo hicho.

Unaweza kwenda Songjiang Campus kwa kupanda metro namba 9 na kushuka katika Kituo cha Mji wa Vyuo Vikuu wa Songjiang (Songjiang University Town).

Tafadhali uwe na makini kuhusu wakati wa kuanza kazi na kufunga kazi wa metro hizi.

Mabasi

Mabasi yanayoelekea Hongkou Campus: Nambari 937, Nambari 959, Nambari 70, Nambari 853, Nambari 933, Nambari 222, Nambari 79, Nambari 875 n.k.

Mabasi yanayoelekeza Songjiang Campus: Songjiang Nambari 5, Songjiang Nambari 3, Songjiang Nambari 9 n.k. Pia kuna Tram Nambari T2 Mji wa Vyuo Vikuu wa Songjiang mpaka Barabara ya Wenhui.

Gharama ya mabasi au Tram: yuan 1 au 2.

Basi la SISU

SISU ina mabasi yanayounganisha Hongkou na Songjiang Campus, ambayo yana huduma kwa wanafunzi, walimu na wageni wa chuo chetu tu.

Gawanya: