Michezo na Afya Bora

MICHEZO KWA WOTE

SISU ina historia ndefu ya michezo. Kufikia leo tuna timu mbili za mabingwa na zingine kadhaa za kawaida. Hizi mbili ni Timu ya Besiboli na Timu ya Go. Zote zimepata mafanikio makubwa duniani. Timu yetu ya Go imeshinda katika mashindano mengi, kama vile Mashindano ya Kikombe cha Wanafunzi Tokyo, Mashindano ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Nchini China n.k. Aidha, timu yetu ya besiboli imejenga uhusiano wa ushirikiano na Umoja wa Besiboli ya Mabingwa wa Marekani (MLB). Tunashirikiana ili kukuza maendeleo ya mchezo huo hapa China.

Zaidi ya hayo, kila mwaka tuna Mashindano ya Michezo ya Chuo, Mashindano ya Kikombe cha Mkuu wa Chuo (ambayo yanahusu mpira tu) na harakati nyingine nyingi za michezo hapa SISU. Isitoshe, michezo hii pia inakuza tabia ya kushirikiana kati ya wanafunzi na kuendeleza kazi zetu za michezo na afya.

Chuo chetu kina vifaa vingi vya kujenga afya, vikiwemo: nyanja mbili za michezo, kituo kimoja cha kupumzikia,  bwawa moja la kuogelea kitaalamu n.k. Licha ya hayo, tuna vyombo vingi vya kuchezea mpira kama vile mpira wa vikapu, wa soka, wa besiboli na miingineyo. Kwa kusema kweli, wanafunzi na walimu wote wana nafasi kubwa ya kujijenga kiafya katika vifaa vya SISU.

Gawanya: