Matawi ya Chuo Kikuu

TAWI LA HONGKOU

Tawi la Hongkou liko karibu na Bustani ya Lu Xun, eneo lake ni kama 0.169 kilomita za mraba hivi. Wakati unapotembea chuoni utavutiwa na mandhari nzuri ya humo ndani. Chuo chetu kiliitwa Chuo Kikuu cha Chizhi (ambacho kiliasisiwa mnamo 1924 na kubadilishiwa jina kuwa Kitivo cha Chizhi), nacho kimewahi kuwa Tawi la Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Jinan. Mnamo mwezi wa Februari, mwaka 1950, tawi lenyewe lilihamia kuja katika anuani mpya na majengo makongwe yakafanyiwa ukarabati.

Sasa tawi hili limekuwa kituo cha mafunzo cha wanafunzi wa shahada ya uzamifu, wanafunzi kutoka nchi za ng’ambo na kadhalika.

TAWI LA SONGJIANG

Tawi la Songjiang ni mojawapo ya vyuo vikuu vilivyo mtaani Songjiang, eneo lake ni kama kilomita 0.578za mraba  hivi. Katika tawi hili kuna wanafunzi wa shahada ya kwanza na wanafunzi wa shahada ya uzamili.

Tawi hili linajulikana kwa mandhari yake nzuri na majengo yenye miundo ya nchi za kigeni. Kwa mfano, jumba la Kitivo cha Lugha za Asia na Afrika lina usanifu wa Kiislamu, jumba la Kitivo cha Kiingereza lina umbo la Kiingereza na jumba la Kitivo cha Kijapani lina usanifu wa Kijapani … hivyo katika chuo chetu unaweza kuona ujenzi wa ustadi wa aina na asili nyingi.

Tawi letu la Songjiang lenye majengo ya mitindo ya aina mbalimbali ni la kipekee hapa nchini, tena inapendeza zaidi na kufaa kwa sherehe na mihadhara mbalimbali.

Gawanya: