Uchapishaji wa Chuo

Shirika la Uchapishaji la Elimu ya Lugha za Kigeni la Shanghai (SFLEP Shanghai Foreign Language Education Press) ambalo liko chini ya utawala wa Wizara ya Elimu na SISU lilisajiriwa katika mwaka 1979. Baada ya maendeleo ya miaka 30 hivi, SFLEP imekuwa mojawapo wa mashirika makubwa tena maarufu kabisa yanayozingatia sekta ya uchapishaji wa lugha za kigeni nchini China.

Sasa, SFLEP imechapisha vitabu 6000 vya karatasi na vya nakala za kielektroniki vya lugha zinazofikia 30 Idadi ya nakala zilizochapishwa ina ujumla unaokaribia milioni 600. Miongoni mwao, kuna vitabu zaidi ya 600 ambavyo vimesifiwa mara nyingi na serikali na kushinda tuzo za aina hii na aina ile.

SFLEP inatambulikana kwa kiwango chake cha juu katika uchapishaji wa vitabu vya mafunzo, ambavyo vinaingia darasani mwa vyuo zaidi ya 1000 nchini China.

SFLEP inazingatia sana kazi za kuchapisha vitabu vya masomo na uhariri wa makala maalumu ya utafiti. Hali kadhalika, linapanua eneo lake la uchapishaji katika vitabu vya vifaa vya elektroniki, vya media anuai, filamu na picha, vitabu vya utafiti wa lugha za kigeni, n.k.

Katika Marejeleo ya Vitabu vya Kiutafiti vya Kichina (CBKCI) ya mwaka 2015, SFLEP ilikuwepo na kuwasilisha sehemu ya kwanza ya aina ya fasihi katika lugha za kigeni, ambayo ilisababisha sauti kubwa katika jamii.

Ukipenda kujua zaidi, tafadhali tumia http://www.sflep.com

Gawanya: