Muhtasari wa Shughuli za Utafiti
KUTAYARISHA FIKIRA
Kwa kufuata lengo letu la "kuutambulisha ulimwengu mzima China" na "kuitambulisha China kwa dunia yote", tumejitokeza kama mojawapo ya taasisi kuu za utafiti zinazoongoza katika kufundisha lugha, taaluma za kitamaduni na siasa za kimataifa.
Kutokana na miradi mbalimbali ya lugha na taaluma za kila aina, huku tukiitikia mikakati ya kitaifa na ya kikanda, tuna taasisi tele na vitovu vingi vinavyotumika kama asili ya mawazo ya kitaaluma.
Katika miaka ya hivi karibuni, tumeanzisha utafiti maalumu unaozingatia Taaluma za Kanda. Kwa kufadhiliwa na Wizara ya Elimu, vitovu vyetu vya Taaluma za Umoja wa Ulaya, Taaluma za Kirusi na Taaluma za Kiingereza vinajulikana sana, na isitoshe vina majukumu muhimu katika uamuzi wa kidiplomasia nchini China.
Wengi wa wahadhiri wetu hawafundishi tu, bali pia wanatoa mchango mkubwa katika utafiti wa kitaaluma. Wanafanya uchunguzi katika masomo yao na kufanya uvumbuzi kibunifu unaojumuisha mafunzo na ujuzi wa kimataifa.
Wanafunzi wetu wanahimizwa kushiriki katika miradi mbalimbali ya utafiti. Mashindano ya Tuzo la Mhadhiri Mkuu ni mashindano ya kitaaluma yanayofanyika kila mwaka miongoni mwa wanafunzi wa shahada ya kwanza. Miradi mingine ni kama vile programu inayohusu uandishi na uboreshaji wa tasnifu, Chama cha Kusoma, Makabati ya Vitabu Kwa Wanafunzi Wapya, na mfululizo wa hotuba na mihadhara. Shughuli hizi zote huwasaidia wanafunzi kukuza tabia fanisi za kujifunza kwa kufuata utaratibu, kusoma kwa kina na upana, kuandika na kufanya majadiliano ya utafiti wa kina.
Mfululizo wa Seminaa za Wahitimu unayoandaliwa na wanafunzi wa shahada ya pili imetoa jukwaa la ufanisi wa kubadilishiana maoni. Lugha za Kigeni, Taaluma za Tamaduni na Mfululizo wa Tasnifu za Kitaaluma yote yanaonyesha jitihada zetu za utafiti na wanafunzi wenye uwezo na ujuzi wa hali ya juu.