Desturi na Shughuli

SISU ni chuo kinachosifika kwa utamaduni wa kila aina, kwa sababu kinatia maanani athari ya utamaduni kuwawezesha wanafunzi kukuza tabia nzuri. SISU hupanga shughuli mbalimbali kwa kufuata wito wa “Dhamira yenye Mawazo, Taaluma yenye Ustadi”. Hapa chuoni kuna mihadhara ya mada tofauti, sherehe za kuvutia za kitamaduni na mashindano yanayofanywa na vyama mbalimbali. Chuo kizima kimejaa uchangamfu na ujana.

TAMADUNI ZA AINA MBALIMBALI

Kila mwaka kuna mfululizo wa shughuli kama vile Sherehe ya Kitamaduni ya Lugha za Kigeni, Sherehe ya Utamaduni wa Kichina, sherehe ya Kukaribisha Wanafunzi Wapya na sherehe nyingine zanazozua hali ya kufurahisha. Aidha, kila kitivo kina sherehe yake maalum, kama vile Sherehe ya Tamthilia za Shakespeare ya Kitivo cha Kiingereza, Wiki ya Kitamaduni ya Kitivo cha Kijerumani, Maonyesho ya Utamaduni wa Kidesturi ya Kitivo cha Lugha za Asia na Afrika na kadhalika.

SANAA NA BURUDANI

Elimu za kisanii na burudani tofauti pia zinapendeza hapa chuoni. Mfululizo wa “Sanaa Yaja Chuoni (Fine Art into Campus)” unawapa wanafunzi uwezo wa kuzijongea, kutambua na kufahamu sanaa za kisasa. Masomo ya sanaa na vyama vinavyohusika pia vimeanzishwa, kwa mfano SISU Finalmente Troupe iliyopewa Tuzo la Utendaji wenye Ustadi Kabisa, Chama cha Ala za Muziki za Kichina, Kwaya ya Acappella inayovutia na Mashindano ya Waimbaji Kumi Hodari yanayofanywa kila mwaka. 

Gawanya: