UPOKEE ULIMWENGU

Kikiwa kama kimojawapo cha vyuo vikuu vya kwanza vya China, ambavyo vilizingatia ushirikiano wa kimataifa na kubadilishana kwa mawazo, SISU ina maarifa mengi ya kuwapokea wataalamu wa kigeni tangu mwanzo wa chuo hiki. Walimu na wanafunzi wote kwa pamoja huzoea kushirikiana katika mazingira ya kimataifa.

Tumejiunga katika ushirikiano na vyuo vikuu, taasisi na mashirika ya kimataifa 330 katika mikoa mingine na katika nchi 56 . Tena tunashirikiana ili kukuza mafunzo yetu ya lugha na tamaduni za kigeni. Kila mwaka tunawapokea wanafunzi wa kigeni wapatao 4000, ili kutimiza vizuri wito wetu wa kukuza kubadilishana kwa tamaduni kati ya China na ulimwengu wote. Zaidi ya hayo, tumeanza taasisi 10 za Confucius (Kǒngzǐ xuéyuàn) ili kujiunga na kukuza mafunzo ya Kichina katika nchi zingine.

KUVUKA MIPAKA

Miradi ya ubadilishaji wa kimataifa imeanzishwa katika nchi zinazolengwa, kama vile katika mikoa iliyo na nia inayolingana katika mifumo ya alama za elimu za wanafunzi wa SISU katika masomo msingi, lugha zisizopewa umuhimu katika dunia nzima na vilevile masomo yanayojumuisha mseto wa nyanda.

Wakati huo huo, wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanapewa msaada wa kifedha kila mwaka kutoka Baraza la Udhamini wa Masomo la China na wafadhili wengine ili kufanya utafiti katika nchi za kigeni, ambao unaongeza zaidi wigo wao wa kitaaluma na ufikiaji wa kiwango cha kimataifa.

Pia tumechukua hatua za kuwahamasisha wafanyakazi wafundishao wawe na mazoea ya kutembelea vyuo vikuu bora nchini China na katika nchi zingine ili kusoma uzoefu wa wenzao katika elimu ya juu. Kwa mfano, katika miaka ya hivi karibuni, wanachama kadhaa wa vitivo vya SISU wamepokea misaada ya kifedha kutoka kwa wafadhili ikiwa ni pamoja na Baraza la Udhamini wa Masomo la China na Programu ya Fulbright Scholar, ambapo waliweza kushiriki kama wasomi wa kutembelea katika mipango ya kubadilishana masomo iliyokuwa imeandaliwa na vyuo vingine vikuu vya dunia.

Aidha, tangu mwanzo wa miaka ya 1970, SISU imekuwa ikiwajumuisha wanafunzi wa kimataifa. Sasa kila mwaka, wanafunzi wengi wanaotoka nchi tofauti huja kujifunza hapa SISU kwa kipindi cha muda mfupi au mrefu. Hii imeboresha uelewa wao wa tamaduni za Kichina, imekuza mawasiliano ya njia mbili kupishana na kuongeza ushirikiano wa kimataifa kwa SISU. Hadi leo chuo hiki kimesajiri zaidi ya wanafunzi 30,000 wa kimataifa kutoka zaidi ya nchi 90, hivyo kina sifa ya kuwa na mojawapo ya makundi makubwa zaidi ya wanafunzi wa kimataifa nchini China.

“KUTANDAWAZI”

Kuenea kimataifa kwa SISU kumeimarishwa zaidi na ziara za wakuu wa serikali, viongozi wa mbalimbali wa balozi za kigeni, wawakilishi wa juu wa mashirika ya kimataifa, wasomi wa kimataifa na wajumbe na washauri wengineo wa  China..

Kila mwaka, SISU inahudhuria mikutano mingi ya kitaaluma ya kimataifa au ya kitaifa ambayo wataalam na wasomi wanaotoka duniani kote wanatoa maoni juu ya masuala makubwa yanayojitokeza katika maeneo yao ya kitaaluma, na hivyo wanausukuma mbele uwezo wa SISU, ambao unahusu kubadilishana na kushirikiana kimataifa katika nyanda za juu za tafiti za taaluma.

Gawanya: