Kuwasiliana nasi

Karibu SISU!

Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU) kipo tangia mwaka 1949, umri wake ni sawa na uwepo wa Jamhuri ya Wananchi China. Sote, walimu kwa wanafunzi tunafuata mila na desturi za watu wa China tukiwa na nia na matumaini kuhudumia mikakati ya maendeleo ya nchi; sisi tukijikita kwenye nyanja za lugha na tamaduni tofauti, ambako tunajaribu kutoa mchango wetu; tunatumai wanafunzi wetu watakuwa nguzo kuu za jamii.

SISU hutajika na kusifiwa kwa majina mazuri kama “kimojawapo cha vyuo asili vya ngazi ya juu kabisa vinavyofundisha lugha za kigeni nchini China” na “shule ya kwanza ya lugha za kigeni ya sehemu ya Jiangnan”. Baada ya kujiendeleza kwa miaka ipatayo 60, sasa SISU imekuwa ni chuo kikuu maarufu sana kinachozingatia mafunzo ya lugha za kigeni na taaluma za kimataifa.

Kwa kusoma habari zilizo hapa katika tovuti hili, utapata historia yetu na kuwajua walimu wa zamani waliofunza kwa kiwango cha juu sana. Pia unaweza kusoma matokeo yetu ya taaluma na mafunzo, kujua zaidi kuhusu mawasiliano yetu ya kimataifa, na maisha ya wanachuo wetu yanayojawa na mambo tele tofauti tena ya kimataifa.

Kwa ujumla, tovuti hii inatoa habari nyingi unazohitaji kujua kuhusu SISU. Tunakutakia furaha nyingi unaposoma na kutujua.

Anwani

Hongkou Campus: Barabara ya Dalianxi, 550, Shanghai, China (200083)

Songjiang Campus: Barabara ya Wenxiang, 1550, Shanghai, China (201620)

Namba za Simu

Namba ya Maelezo kwa wageni: +86 (21) 35372867

Namba ya Ofisi ya Habari: +86 (21) 35372577

Kwa Baruapepe

Ofisi ya Mawasiliano ya Kimataifa: fao@shisu.edu.cn

Ofisi ya Wanafunzi wa Kigeni: oisa@shisu.edu.cn

Gawanya: