Maktaba

SISU ina matawi mawili, yaani, Hongkou na Songjiang. Kwa jumla kuna eneo la hekta 74.7. Ingawa matawi haya ni chuo kimoja chenye uhusiano wa karibu sana, kila tawi lina sifa zake maalum na maarufu.

Maktaba ya SISU ni mmoja wa wanachama watatu wakuu wa CALIS (China Library Consortium of Foreign Studies). Maktaba hii inahifadhi vitabu zaidi ya milioni moja – zaidi ya nusu yake vikiwa katika lugha za kigeni- na zaidi ya nyaraka milioni 1.4 za elektroniki.

SISU inamiliki vifaa vya hali ya juu vya utafiti. Hivi ni pamoja na mitambo ya kipekee duniani ya ukalimani, vifaa vya setiliti vya kupokea habari na maabara ya lugha na isimu. Rasilimali tajika za elektroniki zenye midia anuwai ya taaluma za kimataifa inapatikana SISU ili kutumikia mahitaji ya kufundisha na kufanya utafiti katika nyanja husika. 

Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai kina matawi mawili yaani tawi la Hongkou na tawi la Songjiang.Eneo la SISU ni jumla ya kilomita za mraba 74.7 hivi, kampusi hizi mbili zina asili ya aina moja lakini sifa za kipekee. Maktaba yetu ni mojawapo kati ya maktaba tatu muhimu za Muungano wa Maktaba za Vyuo Vikuu vya Lugha za Kigeni, imetenganishwa kuwa sehemu mbili, yaani Maktaba ya Run Run Shaw iliyopo Hongkou na Maktaba ya Kituo cha Habari iliyopo Songjiang.

Maktaba inahifadhi vitabu vipatavyo milioni 1.087 na aina 2366 za majarida ya Kichina na ya lugha za kigeni. Licha ya hayo, humo ndani kuna bitabu pepe zaidi ya milioni 1.45, majarida pepe zaidi ya 20 elfu, database zaidi ya 50 na database 9 maalumu za kujijenga, Kituo cha Lugha na Fasihi za Kiingereza (ELLMC) kinachofadhiliwa na Wizara ya Elimu kinajulikana nchini kote kwa kuwa na hazina kubwa. Unaweza kutumia VPN ili kutumia  mtandao wa maktaba mahali popote na wakati wowote.

Kazi za maktaba zinaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa, wasomaji wanaweza kutafuta habari za vitabu kwa kutumia kompyuta ya kuhudumu, wale wanaochukua kompyuta za kibinafsi zinaweza kuunganishwa na WI-FI kama wanavyopenda. Zaidi ya vyumba vya kusomea na vyumba vya majadiliano, maktaba imeandaa Mahali Maalumu pa Kujifunzia Pamoja (Learning Commons) ili kutoa huduma za kila aina mwafaka kwa wasomaji kuweza kusoma pamoja.

Aidha, idara za chuoni na taasisi za utafiti pia zina vyumba maalumu vya vitabu vinavyozingatia zaidi lugha zao na utafiti wao.

Gawanya: