Mkurugenzi wa Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Nairobi Prof. Dr. Iribe Mwangi Afanya Ziara katika SISU na Kuwasilisha Mhadhara
Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China
Soma Zaidi
Mkurugenzi wa Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Nairobi Prof. Dr. Iribe Mwangi Afanya Ziara katika SISU na Kuwasilisha Mhadhara
05 December 2024 | By 宋艺婷 Monika | SISU
Tarehe 5 Novemba, mwaka 2024, Prof. Dr. Iribe Mwangi, Mkurugenzi wa Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya, alifanya ziara katika SISU na kuwasilisha mhadhara. Profesa CHENG Tong, Mkuu wa Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika, alikutana na Profesa Iribe. Walijadiliana kwa kina kuhusu kuanzisha ushirikiano kati ya SISU na Chuo Kikuu cha Nairobi, wakafikia kiwango cha juu cha makubaliano. Harakati hii iliweka msingi imara wa kukuza mawasiliano ya kitaaluma kati ya vyuo vikuu viwili, ili kukuza zaidi ufundishaji wa lugha za Kiafrika katika SISU na kuimarisha ushirikiano wa elimu baina ya China na Afrika.
Kabla ya mkutano huo, Profesa Iribe aliwasilisha mhadhara wa “Muhtasari wa Lugha na Fasihi ya Kiswahili: Jana, Leo na Kesho” kwa walimu na wanafunzi wa Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika. MA Jun, mkurugenzi wa Idara ya Kiswahili ya SISU, aliandaa mhadhara huo.
Profesa Iribe alithibitisha kwamba Kiswahili ni lugha ya Kiafrika inayotokana na Kibantu kwa kutaja nyaraka za kihistoria na ushahidi kama vile sifa zilezile za kisarufi kati ya Kibantu na Kiswahili. Aidha, Profesa Iribe alisema kuwa nyaraka za kale za Kichina Yu Yang Tsa Tsa na Chu Fan Chi pia zina maelezo muhimu kuhusu lugha na utamaduni wa Afrika Mashariki, ambayo inaonyesha uhusiano wa awali kati ya Asia na Afrika mamia ya miaka iliyopita.
Halafu, Profesa Iribe aliwafafanulia wanafunzi kuhusu lahaja za Kiswahili na mchakato wa Usanifishaji wa Kiswahili, akazingatia matumizi ya Sheng nchini Kenya.
Mwishoni mwa mhadhara, Profesa Iribe alijulisha maendeleo ya fasihi simulizi na fasihi andishi ya Kiswahili, na akaeleza kwa ufupi mabadiliko ya tanzu na mada ya fasihi ya Kiswahili. Mabadiliko haya yanaonyesha mabadiliko ya kihistoria ya jamii ya Kenya na Afrika Mashariki, pia yanaonyesha haiba na sifa za kipekee wa fasihi ya Kiswahili ulimwenguni.
Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China