Ujumbe wa Muungano wa Kisheria wa China na Afrika Wafanya Ziara katika SISU
Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China
Soma Zaidi
Ujumbe wa Muungano wa Kisheria wa China na Afrika Wafanya Ziara katika SISU
05 December 2024 | By 宋艺婷 Monika | SISU
Tarehe 1 Novemba 2024, mwaka 2024, Ujumbe wa Muungano wa Kisheria wa China na Afrika (Africa-China Legal Alliance) ulifanya ziara katika Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai, na kujadiliana kwa kina pamoja na walimu na wanafunzi kutoka Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika na Kitivo cha Sheria. Wageni walikuwa pamoja na Bibi Mary Muthoni Gichohi, mwenyekiti wa upande wa Kenya wa Muungano wa Kisheria wa China na Afrika na balozi mstaafu wa Kenya nchini China, wakili WU Jun, mwenyekiti upande wa China, wakili XU Dandan, katibu mkuu, wakili ZHANG Hui, mwenyekiti mtendaji wa China, na CHEN Li, wakili wa Ofisi ya Biashara ya Kimataifa ya Kampuni ya Sheria ya Beijing Hengdu (Shanghai). WANG Zheng, naibu katibu wa Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika, MA Jun, mkurugenzi wa Idara ya Kiswahili, NING Yi na Fredrick Maiso Bosire, walimu wa Kiswahili, ZHANG Qi, profesa msaidizi wa Kitivo cha Sheria, na wawakilishi wa wanafunzi wa Kiswahili walishiriki katika majadiliano.
Wang Zheng aliwakaribisha wajumbe kwa mikono miwili, akaeleza kwa kina historia ya maendeleo na sifa za Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika, hasa mipango ya ujenzi wa utafiti wa Afrika na ukuzaji wa wasomi wa Kiswahili. Alitazamia kushirikiana na Muungano wa Kisheria wa China na Afrika, kuvumbua mtindo wa ukuzaji wa wasomi kama “lugha na sheria” katika taaluma mbalimbali, ili kusaidia kukuza mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na Afrika na ujenzi wa mpango wa “Ukanda na Barabara”.
Bibi Mary alitoa shukrani kwa SISU kwa mapokezi hayo mazuri, na kusisitiza umuhimu wa Kiswahili barani Afrika na jukumu muhimu la Kiswahili katika kukuza uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika. Alisema Muungano wa Kisheria wa China na Afrika utasaidia kikamilifu ujenzi na maendeleo ya kozi ya Kiswahili katika SISU.
Wakili Wu Jun alijulisha hali ya msingi ya Muungano wa Kisheria wa China na Afrika, mazingira ya kisheria katika nchi za Afrika, na hitaji la dharura la wasomi wa Kiswahili katika utendaji wa sheria kati ya China na Afrika. Alisema Muungano wa Kisheria wa China na Afrika uko tayari kutoa fursa mbalimbali za mazoezi kwa wanafunzi wa Kiswahili wa SISU nchini Kenya, ili kukuza wasomi wenye stadi ya hali ya juu na mtazamo wa kimataifa ambao wanajua utamaduni wa jamii za Afrika.
Baada ya majadiliano hayo, wajumbe wa Muungano wa Kisheria wa China na Afrika waliwasilisha vitabu vya Kiswahili kwa wanafunzi wa Kiswahili na kuzumgunzana nao. Ziara hii iliimarisha maelewano kati ya Muungano wa Kisheria wa China na Afrika na Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai, pia iliweka msingi wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika siku zijazo.
Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China