Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China
Soma Zaidi
Habari ya Marejeo (Reference News) x SISU: Ushirikiano wa Chuo Kikuu na Vyombo vya Habari katika Sekta ya Elimu
21 June 2024 | By 宋艺婷 Monika | SISU
Tarehe 10 Mei, harakati ya “Shirika la Xinhua na Habari ya Marejeo (Reference News) ya Kidigitali ziingia chuoni” ilifanyika katika Kituo cha Elimu ya Kimataifa katika Kampasi ya Songjiang ya Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU). Zhou Xiaozheng, Katibu wa Kamati ya Chama cha Kikomunisti na rais wa Habari ya Marejeo, na ujumbe wake waliipa SISU Habari ya Marejeo ya Kidigitali na kutoa hotuba chuoni. Wang Jing, Naibu Katibu wa Kamati ya Chama cha Kikomunisti ya SISU, wakuu wa idara zinazohusika, na wakilishi wa walimu na wanafunzi walishiriki na harakati hii.
Wang aliwajulisha wageni hali ya kazi za mafunzo katika SISU na jinsi SISU ilivyowapanulia wanafunzi upeo wa kimataifa. Miaka hivi karibuni, kwa ajili ya kuhudumia maendeleo ya kimkakati ya kitaifa, SISU imekuwa ikitekeleza Mpango wa “Lugha nyingi +”, kujenga mfumo wa mawasiliano wa kimataifa wenye vipimo vingi juu ya msingi wa mazoezi, na kuvumbua njia ya kukikuza kizazi cha Z kwa kupitia miradi tofauti. Katika siku zijazo, SISU na Habari ya Marejeo zitaendelea kuimarisha ushirikiano baina ya chuo kikuu na vyombo vya habari katika ukuzaji wa wanafunzi na kushikana mkono ili kuboresha maelewano na mabadilishano kati ya China na nchi za nje.
Zhou alirudia historia tukufu na jadi la Habari ya Marejeo, na kujulisha maendeleo mapya zaidi kuhusu kundi la vyombo mypa vya habari na ujenzi wa tanki ya wanachuoni. Aliamini kwamba Habari ya Marejeo ina uwezo wa kuimarisha ushirikiano wa vyuo vikuu katika kuboresha elimu ya siasa, maendeleo ya makozi, hasa makozi ya lugha za kigeni na utafiti wa tafsiri, na mawasiliano ya kimataifa.
Asubuhi hiyo, hotuba kuhusu “Kutumia Habari ya Marejeo katika Madarasa ya Hali na Sera” ilitolewa katika Kituo cha Elimu ya Kimataifa. Chen Xiangyang, mhariri mkuu wa Habari ya Marejeo, alitoa hotuba maalumu ili kutambulisha vipengele vya uhariri, na pia alionyesha mabadiliko ya kimataifa na mwelekeo wa maendeleo ya China kwa kutumia mifano ya nakala zilizochaguliwa.
Halafu wanafunzi walijadiliana na Chen kwa kina kuhusu mada mbalimbali, zikiwemo jinsi AI inavyoathiri tafsiri na upekee wa Habari ya Marejeo ni nini likilinganishwa na magazeti mengine.
Wang Mengyuan, mwanafunzi wa daraja la pili, aliona mabadiliko ya kidigitali ya vyombo vya habari vya kiasili kupitia hotuba. “Kwa kukabiliana na Enzi Mpya, Habari ya Marejeo inafuatana na habari katika mtandao kwa haraka. Zaidi ya hayo, Habari ya Marejeo ni gazeti yenye ubora, huku likitoa taarifa sahihi na aminifu kwa umma, na kuwaonyesha dunia na mawazo yake kuhusu China.”
Chen Yanqi, mwanafunzi wa shahada ya pili kutokana na Kitivo cha Mawasiliano na Uandishi wa Habari, alisema kwamba Habari ya Marejeo ilimpa mitazamo ya kipekee ya kuelewa dunia, ili aweze kuendelea sambamba na mwelekeo wa kimataifa na kupanua upeo wake wa kimataifa. Kama mwanafunzi wa Kitivo cha Mawasiliano na Uandishi wa Habari, pia atachukua jukumu la kuboresha uwezo wa nyanja mbalimbali, ustadi wa kitaaluma na unyeti wa habari, ili sauti ya China isilikizwe vizuri zaidi.
Kong Xiangrui, Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Kozi ya “China na Dunia” katika Kitivo cha Utafiti wa Marx, alikuwa mwenyeji wa hotuba. Wakilishi wa walimu na wanafunzi walihudhuria hotuba hii.
Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China