Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Mbio ya Furaha ya SISU ya Awamu ya Kwanza Tarehe Nne Mei: Maadhimisho ya Vijana na Afya


11 June 2024 | By 宋艺婷 Monika | SISU

  • Mbio ya Furaha ya SISU ya Awamu ya Kwanza

  • Mbio ya Furaha ya SISU ya Awamu ya Kwanza

  • Mbio ya Furaha ya SISU ya Awamu ya Kwanza

  • Mbio ya Furaha ya SISU ya Awamu ya Kwanza

 

Tarehe 26 Aprili, kwa ajili ya kusherehekea Siku ya Vijana Tarehe Nne Mei na kusifia nguvu za vijana, Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU) kiliandaa Mbio ya Furaha ya SISU ya Awamu ya Kwanza Tarehe Nne Mei kwa mafanikio. Harakati hii ilipangwa na Kamati ya Michezo ya SISU. Ofisi ya Shughuli za Wanafunzi, Idara ya Elimu ya Kimwili, Kamati ya Wafanyakazi wa SISU, Kamati ya Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa China ya SISU pia zilishirikiana kuandaa harakati hii. Wanafunzi na walimu zaidi ya 300 walishiriki na mbio.

Kabla ya mbio, Katibu wa Kamati ya Chama cha Kikomunisti ya SISU Yin Dongmei alitunukia bendera kwa Kundi la Mbio la Wanafunzi la SISU, ambacho kinaashiria uzinduzi wa kundi hili. Mbio ilianzwa baada ya amri kutolewa na Katibu Yin Dongmei, Mwalimu Mkuu wa SISU Li Yansong, Naibu Katibu wa Kamati ya Chama cha Kikomunisti ya SISU Wang Jing. Washiriki walifanya mazoezi kidogo chini ya uongozi wa walimu Si Yanran na Wang Wei kabla ya mbio. Timu ya wanafunzi wanaotokana na Umoja wa Wanafunzi ilipeperusha bendera na kuwaongoza washiriki mbele.

Hatua nyepesi za washiriki ziliambatana na muziki kutokana na Kundi la Muziki Huria la X, na muziki wao uliongeza hali ya kusisimua kwa harakati hiyo. Timu ya wajitolea ilitoa misaada katika mbio wote, kama vile kuwaambia washiriki upande na kuwapa vinywaji vyenye lishe, ili kuhakikisha tukio hili lipangwe vyema.

Baada ya mbio, maadhimisho ya kutoa tuzo ilifanyika kwa wakimbiaji watano bora zaidi wa kiume na wa kike katika kundi la wanafunzi na la walimu kwa kumaliza mbio za 10.5 km na 5.4 km. Zaidi ya hayo, washiriki wote wengine walipata medali nzuri za kukumbuka kama alama ya kumaliza mbio zao.

 

Sauti kutokana na uwanjani:

Lin Minghong, mshindi wa 5.4 km katika kundi la wanafunzi wa kiume (Kitivo cha Utafiti wa Urusi na Urasia) alisema kwamba, “Nilikuwa nimechoka kidogo katika mzunguko wa pili. Ilikuwa azma ya kushinda medali ambayo ilinisukuma kukimbia hadi mstari wa mwisho!”

Wang Fang, mshindi wa 10.5km katika kundi la walimu wa kike (Kitivo cha Biashara za Kimataifa) alisema kwamba, “Nilianza kukimbia baada ya kuja SISU, na imekuwa tabia yangu kwa miaka minane. Tukio hili liliandaliwa vizuri. Ninafurahi zaidi kukimba pamoja na wakimbiaji wengine kuliko mimi mwenyewe.”

Katibu Yin Dongmei alisema kuwa, “Ninafurahi kuona kwamba wanafunzi wetu wanashiriki na michezo chuoni kwa shauku. Ninatumai kila mmoja anaweza kupata mchezo atakaopenda katika maisha yake yote wakati wanapokuwa SISU.”

 

Maneno ya Mwisho:

Harakati hii ilionyesha nguvu na uzuri wa washiriki wa SISU ambao walijitoa changamoto na kuvuka mipaka. Tukio pia lilionyesha nguvu za vijana na michezo, huku likisisitiza umuhimu wa afya za mwili na jamii.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi