Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

SISU Ipata Tuzo Sita katika Mashindano ya Ubunifu wa Ufundishaji wa Shanghai


11 June 2024 | By 宋艺婷 Monika | SISU

Tarehe 28 Aprili, Tume la Elimu la Kiserikali Mjini Shanghai lilitangaza washindi wa Mashindano ya Ubunifu wa Ufundishaji wa Shanghai ya Awamu ya Nne. Walimu kutokana na Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU) walipata tuzo moja ya kwanza, tuzo mbili za pili, na tuzo mbili hodari kwa jumla. Kwa hiyo, SISU ilishinda Tuzo ya Shirika Bora. Katika mashindano ya mwaka huu, walimu wa SISU wanaotokana na idara na vitivo tofauti, vikiwemo Kitivo cha Elimu, Kitivo cha Uhusiano na Siasa za Kimataifa, Kitivo cha Uchumi na Biashara za Kimataifa, Kitivo cha Mawasiliano na Uandishi wa Habari, waliwashinda washiriki wengine katika nyanja za elimu ya siasa, ufundishaji wa vipindi vya kimsingi, elimu mpya ya masomo ya usanii na utamaduni, ushirikiano wa uzalishaji na elimu, huku wakionyesha uwezo mzuri wa ufundishaji wa SISU katika makozi mbalimabli.

Mnamo Desemba, mwaka 2023, SISU iliandaa shindano la awali chuoni ili kuchagua washiriki kutokana na walimu wote wa vitivo vyote. Baada ya orodha ya washiriki ilipoamuliwa, Ofisi ya Maendeleo ya Walimu na Ofisi ya Shughuli za Taaluma ziliandaa semina nyingi za mafunzo kuhusu ubunifu wa makozi, falsafa ya ufundishaji, uandishi wa ripoti, uboreshaji wa PPT, mbinu za kuripoti, ambazo zililenga kuwatayarisha walimu hawa katika shindano. Semina hizi zilifanyika kwa njia tofauti za mafunzo, kama vile mashauriano kwa kundi, maarifa kutokana na mifano, mashauriano ya mmoja-mmoja na majaribio ya maonyesho.

Tangu Mashindano ya Ubunifu wa Ufundishaji wa Shanghai ya awamu ya kwanza yalipofanyika, SISU imeshinda tuzo ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo. Miaka hivi karibuni, kwa kukabiliana na mwelekeo wa mabadiliko ya kidijitali katika elimu, SISU imekuwa inawahimiza walimu kubuni njia zao za kuwafundisha wanafunzi na imeanzisha vipindi vingi kwa ajili ya maendeleo ya wanafunzi katika pande zote. Kupitia “Mpango wa Kuboresha Uwezo wa Kufundishia”, utaratibu mzuri umewekwa ili kuwawezesha walimu wa ngazi zote wa SISU kuboresha uwezo wao na kuvumbua mbinu zao za kufundishia. Juhudi hizi zinaonyesha azma thabiti ya SISU ya kuwakuza walimu ambao wanaweza kuongoza katika kuwezesha elimu kwa mabadiliko ya kidijitali, kuwapa wanafunzi fikra za akili na maadili, na hivyo kuwakuza wanafunzi wanaohitajika kwa maendeleo na ustawi wa taifa la China.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi