Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Ujumbe wa SOAS, Chuo Kikuu cha London, Wafanya Ziara katika Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai


04 April 2024 | By 宋艺婷 Monika | SISU

Mnamo Machi 4, mwaka 2024, Profesa Adam Habib, Rais wa SOAS, Chuo Kikuu cha London, na ujumbe wake ulifanya ziara katika Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU). Profesa Li Yansong, Rais wa SISU, aliwakaribisha wageni katika kampasi ya Songjiang.

Profesa Li Yansong alijulisha maendeleo mapya ya SISU katika ujenzi wa makozi, ukuaji wa wanafunzi, na elimu yenye mwelekeo wa kimataifa miaka hivi karibuni. Huku Profesa Li akirudia historia ya mashirikiano baina ya SISU na SOAS, alisisitiza uhuhimu wa kuimarisha mashirikiano kati ya pande hizi mbili baada ya janga la virusi, ili kuboresha mawasiliano katika masomo ya isimu, kisiasa, kikanda na kitaifa, hasa katika masomo ya Asia na Afrika.

Profesa Adam Habib alisema kwamba SISU ni rafiki wa kwanza wa kimataifa ambayo alifanya ziara baada ya janga la virusi. SOAS inatarajia kushiriki pamoja na SISU, ili kuvumbua mfumo wa kuwakuza wanazuoni wa kimataifa, na kutafuta uwezekano wa kuwafundisha wanafunzi wa shahada ya tatu kwa pamoja. Vyuo vikuu viwili vinatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa kiwango cha juu zaidi katika utafiti wa kikanda na kitaifa, ukiwemo utafiti wa Asia na Afrika na wa Mashariki ya Kati.

Baada ya mkutano huu, Profesa Adam Habib na ujumbe wake ulikwenda Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika, na kujadiliana kuhusu shughuli za ushirikiano.

Profesa Cheng Tong, Mkuu wa Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika, aliwakaribisha kwa mikono miwili wageni waliotoka mbali, na kuwajulisha ujenzi wa makozi, vipengele vya masomo, faida za ufundishaji na hali ya mawasiliano ya kimataifa katika Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika. Alisisitiza kwamba kitivo chetu kinazingatia mkakati wa maendeleo ya SISU, na kinatia maanani mabadilishano ya kimataifa na ukuaji wa wanafunzi. Chini ya fursa ya ujenzi wa “Vyuo Vikuu vyenye Ngazi ya Juu na Masomo Mazuri Kabisa Duniani” nchini China, kitivo chetu kinatumai kuboresha mawasiliano katika utafiti na nyanja nyingine, na kuvumbua mfumo mpya wa kuwakuza wanafunzi pamoja na SOAS.

Profesa Adam Habib alitoa shukrani kwa mapokezi mazuri ya kitivo hiki. Alisema kwamba miaka hivi karibuni, SOAS imepanua upeo wa masomo na utafiti, na imewavutia wanafunzi na wasomi wengi zaidi wa kimataifa. Pamoja na mahitaji ya ujuzi wa kimataifa na ya kienyeji katika enzi mpya, Profesa Adam Habib alidokeza kwamba SOAS inatarajia kuanzisha ushirikiano wa kirafiki na kimataifa katika nyanja mbalimbali kwa pamoja na Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika, ili kuanzisha mradi wa kuwakuza wanafunzi wenye ustadi nyingi.

Ziara huu ya SOAS iliimarisha zaidi uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya vyuo viwili, na kuweka msingi imara kwa kupanua nyanja za ushirikiano wa kitaaluma na kiwango cha mawasiliano ya walimu na wanafunzi siku zijazo.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi