Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

SISU Yaongeza Kozi Mpya ya Kikambodia! Mawasiliano ya Utamaduni baina ya China na Asia ya Kusini Mashariki Yaanza Safari Mpya


31 March 2024 | By 宋艺婷 Monika | SISU

  • SISU Imeongeza Kozi Mpya ya Kikambodia

Huku ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Muungano wa Mataifa ya Asia ya Kusini-Mashariki (Association of Southeast Asian Nation, yaani ASEAN) ukiimarika, uhusiano wa kirafiki baina ya China na Kambodia unaendelea motomoto. Hivi karibuni, ombi la SISU la kuanzisha kozi mpya ya Kikambodia limeidhinishwa. Kozi mpya ya Kikambodia inapatikana katika Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika, na inapanga kuwaajiri wanafunzi wanane hadi kumi kila baada ya miaka minne.

Kwanza, kwa pamoja tuangalie lugha hii ya ajabu. Kikambodia, ambacho pia kinajulikana kama Kikhmeri, ni lugha rasmi ya Kambodia, nchi ya Asia ya Kusini-Mashariki. Lugha hii inatumiwa na watumizi zaidi ya milioni 16. Kikambodia kinahusiana na lugha ya Kithai na Kilao kwa kina, na kimetimiza jukumu muhimu katika nyanja nyingine za ASEAN kama vile utamaduni, biashara, utalii n.k. Huku mawasiliano ya kisiasa, kiuchumi na kibiashara, kiutamaduni, yakiongezeka kwa siku kati ya China na Kambodia, soko la wafanyakazi litakuwa na hitaji kubwa la kuwaajiri wanafunzi wanaojua Kikambodia na wenye stadi mbalimbali za kiwango cha juu. Kwa hiyo, wanafunzi watakuwa na kazi-maisha ya kuridhisha na machaguo mengi zaidi baada ya kumaliza masomo yao.

Ikilinganishwa na lugha nyingine, sarufi ya Kikambodia ni rahisi bila mabadiliko magumu ya kimofolojia. Fonolojia ya Kikambodia pia inafahamika kwa urahisi.

Kuanzia miaka ya hamsini karne iliyopita, China na Kambodia zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia, na zilikuwa marafiki ambao walisaidiana na kupatiana maendeleo ya pamoja. Hata miaka karibuni, ushirikiano wa kiuchumi, kiutamaduni, kielimu na kitiba baina ya China na Kambodia umeimarika, umezidi kuboresha ufahamu na urafiki baina ya watu wa nchi hizi mbili. Kwa hiyo, uhusiano wa China na Kambodia unajulikana kama “Chuma cha Pua cha Kambodia”, inaashiria kuwa uhusiano wa nchi hizi mbili ni imara kama chuma cha pua.

Kozi ya Kikambodia katika SISU inalenga kuandaa wanafunzi wenye ustadi wa hali ya juu. Mtaala yakiwemo matamshi, sarufi, usomaji, usikilizaji, tafsiri na nyinginezo. Hali kadhalika, kwa kuandaliwa walimu wataalamu na nyenzo bora za kufundishia, wanafunzi wanaweza kujipatia namna ya kufanya utafiti katika masomo yao, ili wawe na uwezo wa kushiriki katika kazi za kutafsiri, kufanya utafiti, ufundishaji na usimamizi. Zaidi ya hayo, SISU itaandaa mihadhara na mawasiliano ya kiutamaduni na Kambodia, ili wanafunzi wawe na fursa za mabadilishano na mazoezi. Baada ya kuhitimu, wanafunzi wa Kikambodia wanaweza kujipatanisha na mahitaji kazini bila ya kukawia. Wanaweza kutumia Kichina, Kikambodia na Kiingereza kwa ustadi, na kufanya kazi mbalimbali za ukalimali na tafsiri kwa rahisi.

Kwa upande wa ushirikiano wa kimataifa, kwa kutegemea sifa za kimataifa za chuo kikuu, SISU itashirikiana na kuwasiliana na vyuo vikuu maarufu vya Kambodia na vya nchi nyingine za Asia ya Kusini-Mashariki. Kozi ya Kikambodia itawaalika wataalamu wa kigeni wawe walimu wa SISU. Mara kwa mara, itawapeleka walimu waende Kambodia, nchi za Ulaya na Marekani, ili wapate mafunzo ya muda mfupi au muda mrefu pia, au kushiriki katika semina ya utafiti ya kimataifa. Kwa ajili ya kuboresha zaidi kiwango cha ufundishaji wa kimataifa, SISU itawapeleka ng’ambo wanafunzi wanaofadhiliwa na serikali kwa kupitia miradi ya ukuaji wa wanafunzi iliyofadhiliwa na Baraza la Udhamini la China. Hali kadhalika, SISU pia itawapeleka wanafunzi kwa Kambodia ili wapate mafunzo ya muda mrefu au muda mfupi kwa kupitia mabadilishano ya vyuo au njia nyinginezo.

Huku pendekezo la wa “Ukanda na Njia” likiimarika siku hadi siku, China na Kambodia zimepata maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali. Ingawa dunia inaathiriwa na virusi vya korona, China bado ni rafiki kubwa kabisa wa Kambodia katika biashara na uwekezaji. Sasa China inatakiwa kuboresha kiwango na kupanua upana wa kuwafunza wanafunzi wa Kikambodia, pia ni muhimu kuwatolea mafunzo ya Kikambodia, kuwafahamisha tamaduni za Kambodia na za nchi nyingine za Asia ya Kusini-Mashariki, ili waweze kujenga daraja la mawasiliano kati ya China na Kambodia. Kozi ya Kikambodia (ya shahada ya kwanza) itajifunza maarifa ya kozi nyingine za lugha za kigeni, kunufaika na faida zake na kurekebisha mapungufu yake, ili kuanzisha kozi yenye sifa maalumu za SISU.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi