Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Ufundishaji wa Mtandaoni wa SISU | Hans: Maoni kuhusu Usambazaji wa Ujuzi Duniani katika Hali ya Virusi vya Korona


21 April 2022 | By 宋艺婷 Monika | SISU

Mwandishi: Hans-Jörg Luitgar Weber, mwalimu wa kigeni wa Kitivo cha Elimu ya Kimataifa

Kwa sababu ya changamoto ya ufundishaji wa mtandaoni duniani, mageuzi ya elimu yanatokea katika nchi mbalimbali za duniani, jambo ambalo halikufikirika miaka mitano iliyopita. Sasa ninarudia hatua ya kwanza ya ufundishaji wa mtandaoni hapa Shanghai kama ningerudi mwaka 2020. Lakini ufundishaji wa mtandaoni mwaka 2022 umeonyesha kiwango cha juu zaidi cha kitaaluma na matatizo machache.

Mijadala ya kitaaluma ilidhani kwamba aina maalumu za ufundishaji wa mtandaoni hazitekelezeki miaka mitano iliyopita, na kusisitiza upungufu wa elimu kwa mtandao. Hata hivyo, siku hizi walimu wengi wanaamini aina maaluma za ufundishaji zinaweza kufanyika kwa ufanisi kwenye mtandao. Hoja inayotajwa mara kwa mara katika mijadala ni wanafunzi na walimu watakosa mawasiliano ya moja kwa moja. Walimu wenye maarifa walitoa maoni kwamba maadamu “uhusiano wa mtandaoni” unaanzishwa, utaendelea kuwa “mali ya kihisia” katika ufundishaji wa mtandaoni. Hoja nyingine ni matokeo ya utafiti wa sayansi ya neva kwamba ubongo hauwezi kutofautisha kati ya hali ya mtandaoni na ukweli. Kwa hiyo, changamoto ya kweli ya elimu ya mtandaoni ni nini?

Kwa maoni yangu, kuna hatari ya “kutengwa kwa kidigitali” wakati wa kujifunza mtandaoni. Hatari hiyo imejulikana katika taasisi nyingi na kuhitaji kupewa tahadhali, kwa sababu matokeo yake yataathiri moja kwa moja mfumo wa neva ya binadamu, na kusababisha mabadiliko makubwa ya hisia. Walimu wanapaswa kuzingatia hatari hii pia, kwa kuwa usambazaji wa ujuzi tu hautoshi kwa ufundishaji wa kidigitali.

Kwa upande mwingine, tabia ya kijadi ya kujifunza inakatazwa. Sasa njia ya ufundishaji tunayotumia ni tofauti na ufundishaji wa uso kwa uso. Mfumo wa kujifunza wa kijadi umebadilishwa hafla, njia ya kujifunza imepitwa na wakati kwa kiwango fulani, na ufahamu wa darasa pia ulikabiliwa na changamoto.

Walimu na wanafunzi wanaweza kuthibitisha kutokana na maarifa yao kwamba: udhaifu wa jamii ya kisasa pia unaonyeshwa katika ufundishaji wa kidigitali, kwa sababu tunategemea kwa kiwango kikubwa mfumo tata wa kidigitali na rasilimali za kijamii, ili kupatisha ujuzi kwa kizazi kijacho.

Je, tunaweza kukabiliana na mabadiliko haya vipi? Swali hili linahitaji muda, mawasiliano ya wazi na juhudi za kutafuta masuluhisho yanayofaa.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi