Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai Chafanya Hafla ya Kuwakaribisha Wataalamu Wapya wa Nchi za Kigeni wa Mwaka 2021-2022


30 September 2021 | By 宋艺婷 Monika | SISU

Tarehe 17, Septemba, Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU) kilifanya hafla ya kuwakaribisha wataalamu wapya wanaotoka nchi za kigeni wa mwaka 2021-2022 katika kampasi ya Hongkou. Kwa jumla, wapo wataalamu kumi na moja waliotokana na nchi 10 za kigeni, ambao wanafanya kazi katika vitivo saba walihudhuria hafla hii. Wataalamu kadhaa ambao hawajaja China au walikuwa wanakaa karantini kwa sababu ya athari ya janga la korona walihudhuria hafla kwenye mtandao.

Mkuu wa Ofisi ya Mawasiliano na Ushirikiano wa Nje Zhang Hongling alitoa hotuba kwa niaba ya SISU. Alieleza hali ya jumla ya SISU na malengo ya kimaendeleo, pia aliwakaribisha wataalamu wa kigeni waliochagua kushiriki katika SISU kwa mikono miwili. Zhang Hongling alisema kwamba katika mchakato wa kujenga chuo kikuu maarufu cha lugha za kigeni duniani, wataalamu wa kigeni wametoa mchango mkubwa kwa ujenzi wa kozi za chuo na ukuaji wa wanazuoni. Wataalamu wa kigeni wanatarajiwa kutumia faida ya kitaalamu na ya utamaduni, ili kushiriki katika shughuli za ufundishaji na utafiti kwa shauku kubwa na kuzidisha mawasiliano ya kitamaduni baina ya China na nchi za ng’ambo. Baada ya hotuba hii, Zhang Hongling aliwatunukia wataalamu watano wapya wa kigeni nishani na kumbukumbu za SISU.

Wataalamu wapya wa kigeni walijijulisha kwa utaratibu kwenye hafla na kutoa matarajio yao kuhusu kuishi na kufanya kazi katika SISU. Mwakilishi wa vitivo na naibu mkuu wa Kitivo cha Elimu ya Kimataifa Tian Xiaoyong alisema kwamba anatumai wataalamu wa kigeni washirikiane na walimu wa China katika ufundishaji, utafiti na mawasiliano ya utamaduni na sehemu nyingine, ili kusaidia kuboresha kazi za kimataifa za vitivo. Ofisi ya Mawasiliano na Ushirikiano wa nje pia ilitoa mafunzo kwa wataalamu wapya wa kigeni kwa ajili ya kuwasaidia kufanya kazi, na kuwajulisha zana, rasilimali, utamaduni wa chuo, na sera zinazohusika na kadhalika kwa undani katika hafla hiyo.

Tangu muhula mpya ulipoanza, vitivo mbalimbali viliwasalimu wataalamu wa kigeni waliopo Shanghai, na kutoa salamu kwa wataalamu waliopo nchi za ng’ambo kwa mtandao. Vitivo kadhaa viliwaalika wataalamu wa kigeni kushiriki katika harakati za vitivo kwa njia ya mkutano baina ya walimu na wanafunzi, kutembelea chuo na kujaribu kutumia zana za kufundishia, ili kuwasaidia kujua hali ya chuo na vitivo, kuzidisha ujumuishaji wao na kuboresha ujenzi wa kozi za chuo na mafunzo kwa wanazuoni.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi