Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai Chafanya Sherehe ya Kutoa Medali za Kumbukumbu za Miaka 50 Mitukufu Kutumikia Chama


27 June 2021 | By 罗思颖Bahati | SISU

  • Miaka 50 Mitukufu Kutumikia Chama

Siku ya kuzaliwa ya Chama cha Kikoministi cha China ya umri wa miaka 100 inakaribia, sherehe ya kutoa medali za kumbukumbu ziitwazo Miaka 50 Mitukufu Kutumikia Chama ilifanyika kwenye Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU) asubuhi tarehe 18, Juni. Wawakilishi wanaotunukiwa medali za Miaka 50 Mitukufu Kutumikia Chama na wanachama wazee walishiriki katika sherehe hiyo. Jiang Feng (Katibu Mkuu wa chuo kikuu), Li Yansong (Naibu Katibu Mkuu wa chuo kikuu na Mwalimu Mkuu wa chuo kikuu), Wang Jing (Naibu Katibu Mkuu wa chuo kikuu) walihudhuria kwenye sherehe pia.

Katika sherehe hiyo, Jiang Feng, Li Yansong, Wang Jing, Qian Ling walitoa medali za kumbukumbu kwa wanachama wazee waliohudhuria sherehe hiyo. Katibu Mkuu wa chuo kikuu, Jiang Feng aliwaongoza wanachama wote waliohudhuria sherehe kurudia kiapo cha kujiunga na chama.

Jiang Feng aliwatolea wanachama wazee salamu za dhati na heshima kubwa. Alisema kwamba medali za kumbukumbu za Miaka 50 Mitukufu Kutumikia Chama ni utunzaji na sifa ambazo chama kinazitoa kwa wanachama wazee. Vizazi vya wahitimu wa SISU wanarithi roho ya mapinduzi ya chama na kufanya jitihada kubwa, wanawatayarisha watu wengi hodari kwa taifa. Jiang alitoa wito wa kurithi na kukuza roho ya kujitahidi ya mababu zetu kwa walimu, wanafunzi na wanachama wote wa chuo chetu.

Li Yansong alitoa pongezi kubwa na shukrani za dhati kwa wanachama wazee katika hotuba yake. Alisema kwamba miaka 50 waliyotumikia chama ni miaka ambayo walifanya bidii kwa chama na taifa, ni miaka ambayo walichangia SISU na maendeleo ya walimu na wanafunzi kadri wawezavyo. Aliwatarajia vijana wajifunze na warithi vizuri desturi nzuri za watangulizi.

Wang Jing alitangaza orodha ya wanachama 110 wa chuo chetu waliopewa medali za kumbukumbu za Miaka 50 Mitukufu Kutumikia Chama. Wanachama wazee watatu waliopewa medali hizo, Han Kun, Zhu Liyun na Yang Fan walitoa hotuba, wakionyesha upendo wao kwa chama na chuo kikuu chetu.

Wanachama wazee waliopewa medali ya kumbukumbu ya Miaka 50 Mitukufu Kutumikia Chama walisisimka sana, wakisema kwamba watashika amri ya chama na kufuatana na chama daima.

 

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi