Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Jumba la Makumbusho ya Lugha la SISU linaasisiwa!


12 December 2019 | By 斯瓦希里语(sw) | SISU

Lugha ni kiini cha jamii yetu, ambayo inatumika kama kifaa cha mawasiliano ya binadamu, cha kusafirisha ujuzi tena kuonesha hisia zetu za asili kabisa. Watu husema lugha kweli ni mbalozi wa makabila na mataifa yote. Siku hiyo tunafurahi kukuambia kuwa, Jumba la Makumbusho ya Lugha na Historia ya SISU linafungua kwa wageni wote!

Jumba la Makumbusho ya Lugha la SISU lina sehemu 3 tofauti: “Kuwasiliana na Ulimwengu”, “Kuandika Ulimwengu” na “Kueleza Ulimwengu”. Sehemu hizo zikiwemo sekta tofauti tofauti kama vile “Kuzaliwa kwa Lugha”, “Familia ya Lugha”, “Vipengele vya Lugha”, “Uandishaji wa Lugha”, “Utamaduni wa Lugha” na kadhalika. Kwa ujumla kuna sekta 8 ambazo zinazingatia pande tofauti za lugha.

Jinsi tunavyotunza lugha ambayo inafanya kazi ya kuzidisha na kuhifadhi fikra na falsafa inatuletea changamoto. Jumba la Makumbusho ya Lugha la SISU ni hatua zetu za kukuza ubora wetu wa lugha na tamaduni za kimataifa. Tunatumai makumbusho haya yatakuwa eneo la wanazuoni na wanafunzi wote ili waweze kufanya utafiti na kusoma kwa urahisi.

Baada ya miaka 70, toka kozi za lugha za kigeni hadi kozi za lugha za mkakati, toka fasihi za kigeni hadi sayansi ya lugha, kiini cha SISU kilikuwa lugha na kitakuwa lugha kabisa. Tuko pamoja kwa kuzunguka na lugha; tuwasiliane na ulimwengu kwa misaada ya lugha.

Lugha ni nini? Jinsi tulivyopata lugha? Tutatumiaje lugha? Tunatumai kuwa Jumba la Makumbusho ya Lugha la SISU litawaletea watu wengine wengi ujuzi na uzoefu mpya. Zaidi ya hayo, tunatumai kazi zetu pia zitasaidia kuwaeleza wageni wetu hadithi mpya za China.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi