Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Kuendeleza Utafiti ya Maeneo ya Afrika kwa Upesi: SISU Chaanza Idara ya Kiswahili na Taasisi ya Taaluma za Afrika ya Mashariki


17 October 2019 | By Jamila | SISU

Katika tarehe 19, mwezi Mei, mwaka 2019, Kongamano la Utamaduni wa Kiswahili na Taaluma za Maeneo ya Afrika Mashariki, Uzinduzi wa Idara ya Kiswahili wa SISU zimefanyika katika chuo cha Songjiang. Diwani wa utamaduni na biashara wa ubalozi wa Tanzania katika China Bwana Lusekelo Gwassa, katibu wa Chama cha Kikoministi cha China cha SISU Bwana Jiang Feng na wataalamu wengi wa Kiswahili na taaluma za Afrika Mashariki walihudhuria kongamano hili.

Kabla ya kongamano, katibu Jiang Feng na diwani Gwassa walishauriana sana kuhusu ushirikiano na mawasiliano katika elimu na utamaduni baina na China na Tanzania. Bwana Jiang Feng alimjulisha diwani Gwassa hali ya SISU na alitoa shukrani kwa uangalifu na misaada kwenye ujenzi wa idara ya Kiswahili ya SISU kutoka ubalozi wa Tanzania. Mkurugenzi wa Kitivo cha Lugha za Asia na Afrika bwana Cheng Tong, katibu wa Kitivo cha Lugha za Asia na Afrika bwana Chen Xiaoli na mkurugenzi naibu wa mawasiliano bibi Ma Sang walihudhuria mazungumzo yao vilevile.

Katika Uzinduzi wa Idara ya Kiswahili, katibu Jiang Feng aliwakaribisha wageni wote kwa mikono miwili, pia aliwajulisha juhudi za SISU kuhudumia mpango wa “Utanda na Njia” wa China. Wakati huo, diwani Gwassa alitoa pongezi kwa uanzishaji wa Taasisi ya Taaluma za Afrika Mashariki na alitumai kuwa wanafunzi wa awamu ya kwanza wa Kiswahili watapata maendeleo makubwa katika masomo yao na watatoa mchango mkubwa katika urafiki wa China na Tanzania.

Lugha ya Kiswahili inatumiwa na watu kiasi cha milioni mia moja hivi. Ni mojawapo ya lugha tatu kubwa katika Bara la Afrika, kinazungumzwa katika nchi nyingi za Afrika ya Mashariki kama vile Tanzania, Kenya, Uganda n.k. Pia ni lugha ya taifa ya Tanzania na Kenya.

Inasemekana kuwa licha ya kusoma masomo ya lugha, wanafunzi wa Kiswahili pia watasoma masomo ya fasihi, historia, siasa, uchumi, diplomasia na utamaduni wa Afrika Mashariki.

 

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi