Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Peng Liyuan na Mke wa Rais wa Ufaransa Bregitte Watembelea Shule ya Lugha ya Kigeni ya Shanghai


13 November 2019 | By 罗思颖Bahati | SISU

  • Katika Darasa la Kifaransa

Tarehe 5, mke wa Rais Xi Jinping Peng Liyuan alimwalika mke wa Rais wa Ufaransa, Brigitte, kutembelea Shule ya Lugha ya Kigeni ya Shanghai pamoja.

Wake wa marais wa nchi hizo mbili walipofika, wanafunzi walisimama wima kwa mistari na wakapeperusha bendera za China na Ufaransa kuwakaribisha kwa ukarimu, pia wakawapa rundo la maua kama zawadi.

Peng Liyuan na Bregitte kwanza walisikiliza utangulizi kuhusu uendeshaji wa shule na hali ya mawasiliano ya kimataifa, ambao uliwasilishwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo. Halafu, katika darasa la lugha ya Kifaransa, mwalimu alikuwa anafundisha tamaduni za chakula cha China-Ufaransa. Wakati huo, wake wa marais wa nchi hizo mbili walisikiliza masomo kwa makini na wakajibu maswali ya wanafunzi kwa furaha.

Katika darasa la urithi wa utamaduni usioonekana wa China, waliwatazama wanafunzi wakijifunza sanaa za jadi za China. Wanafunzi waliwasilisha kazi zao za sanaa kwa wake wa marais wa nchi mbili kama zawadi.

Zaidi ya hayo, walitazama uwasilishaji wa Pipa la Kuainisha Takataka ambao ulitengenezwa na wanafunzi.

Wanafunzi waliwaimbia nyimbo na kuwachezea dansi wake wa marais wa nchi hizo mbili. Peng Liyuan alisema, “Utamaduni unaweza kuondoa vizuizi na kujenga mawasiliano. Ninatarajia vijana wa nchi hizo mbili wataweza kuunganisha tamaduni za nchi hizo mbili na kuendeleza kuzidi urafiki baina ya China na Ufaransa.” Brigitte alisema, “Ninafurahia sana kuwa wanafunzi wa China wanapenda utamaduni wa Ufaransa, na utamaduni wa China pia unanishangaza kweli. Nafikiri wanafunzi kutoka China na Ufaransa wanatakiwa kuzidi kuwasiliana na kufanya urafiki zaidi.”

 

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi