Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China
Soma Zaidi
Uchunguzi wa Mabavu ya Ushindani wa Serikali ya Tanzania katika Tukio la CMG
28 May 2022 | By 斯瓦希里语(sw) | SISU
1. Utangulizi
1. 1 Uhakiki wa Fasihi
Oktoba 28, 2020, Tanzania ilifanya uchaguzi mkuu wa awamu ya sita. Rais wa Tanzania wa wakati huo, Marehemu John Pombe Joseph Magufuli aliongoza katika uchaguzi huo kwa asilimia 84, akaanza kipindi chake cha pili cha urais. Aliwekea Chama cha Mapinduzi (CCM) rekodi ya kiwango cha umaarufu katika ushindani wa uchaguzi tangu nchi hiyo ilipoanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992. Uchaguzi huu pia ni uchaguzi wa kwanza uliofadhiliwa kikamilifu na serikali ya Tanzania.
Tofauti na vipindi sita vya CCM kushinda tangu mwaka 1992, ripoti iliyotolewa na Wanahabari Wasio na Mipaka (RSF), ilionyesha kuwa kiwango cha uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania kimeshuka kwa pointi 25; Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) ilitoa uamuzi kuwa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ilikiuka Mkataba wa Katiba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sababu ya kuzuia uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari. Uhuru wa kujieleza wa raia na nafasi ya upinzani vilikuwa vikibanwa, na udhibiti mkali dhidi ya vyombo vya habari. Yote yalionekana kukinzana na taratibu za kidemokrasia za uchaguzi
Demokrasia ni mojawapo ya mada kuu katika uwanja wa utafiti linganishi juu ya siasa. Tangu miaka ya 1950, pamoja na maendeleo ya siasa za kimataifa, mada katika utafiti zilionyesha mwelekeo wa kubadilisha kati ya tawala za kidemokrasia na tawala za kimabavu. Pamoja na maendeleo ya siasa za dunia katika miaka ya 1970, mada ya utafiti wa demokrasia iligeuka kuzingatia mifumo ya kimabavu. Tangu miaka ya 1990, mojawapo ya sifa kuu za maendeleo ya dunia ni kuwa mifumo ya mchanganyiko ya kisiasa ilizuka na kustawi, ambayo ilijumuisha demokrasia na utawala wa kiimla kwa viwango tofauti.
Juan Linz alidokeza dhana ya "mfumo wa kimabavu" kwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1963 alipofanya utafiti juu ya serikali ya Uhispania(Linz, Spain 36). Linz alifafanua kuwa mifumo ya kimabavu kwa jumla ina uwepo mdogo kisiasa na uwajibikaji usio wazi. Isipokuwa kwa kipindi fulani cha maendeleo, katika mifumo ya kimabavu, kubadilika kwa uongozi wa kisiasi hakufanyiki.
Kiongozi wa mifumo ya kimabavu huwa mtu binafsi, na wakati mwingine ni vikundi vya watu wachache. Wanaweza kutumia madaraka yao bila ya vikwazo, lakini ukweli ni kuwa madaraka hayo hutabirika sana (Linz, Spain 45).
Linz alieleza kwamba katika nchi nyingi ambazo hazifuati mfumo wa demokrasia, watawala wao walitumia udanganyifu wa demokrasia ili kuficha utawala wa kimabavu. Nchi hizi hata hazifikii viwango vya chini vya demokrasia. Alitumia "mabavu ya uchaguzi" kueleza utawala huo(Linz, Totalitarian 25).
Andreas Schedler alisema kuwa wale walioshika madaraka katika mamlaka ya mabavu ya uchaguzi hutarajia kuchuma matunda ya uhalali kupitia uchaguzi ambao unafanyika kwa muda maalumu na unadhibitiwa vikali (Schedler 48).
Kama aina moja ndani ya mabavu ya uchaguzi, "mabavu ya ushindani" ulionekana kwa mara ya kwanza katika utafiti linganishi uliofanyika na Steven Levitsky na Lucan Way, juu ya rushwa nchini Ukraine na Peru mwanzoni mwa miaka ya 2000. Levitsky na Way walisema kuwa katika tawala zenye mabavu ya ushindani, taasisi rasmi za kidemokrasia huchukuliwa kuwa njia kuu ya kupata na kutumia mamlaka, na wale walio madarakani wanaweza kuendesha kanuni za kidemokrasia, lakini hawawezi kuondoa mifumo ya demokrasia. Hata hivyo, viongozi walio madarakani mara nyingi na kwa ukali walikiuka demokrasia, ambayo huleta ushindani usio wa haki baina ya chama tawala na chama cha upinzani (Levitsky na Way, Rise 25).
Levitsky na Way waliamini kwamba katika utawala wenye mabavu ya ushindani, kwa sababu ya kuwepo kwa mifumo ya kidemokrasia, basi ni hakika kuna uwanja wa ushindani baina ya chama tawala na chama cha upinzani. Kupitia uwanja huu, wapinzani wana fursa ya kuwapinga, kuwapunguza nguvu, au hata kuwashinda viongozi walio madarakani. Nyanja zake nne muhimu ni uchaguzi, mahakama, sheria na vyombo vya habari. Miongoni mwa nyanja za vyombo vya habari, wale walio mamlakani katika tawala za mabavu ya ushindani, mara nyingi hutumia mbinu za hila kukandamiza vyombo huru vya habari, ikiwa ni pamoja na sheria za vyombo vya habari zinazowezesha kufunguliwa mashtaka kwa wanahabari huru wa upinzani .
Levitsky na Way walitumia mfano wa utafiti kuelezea Tanzania kama nchi yenye "uhusiano mdogo, uwezo wa tawala wa kiwango cha juu (low linkage, medium high ognizaitonal power)", na hivyo inaashiria kuwa Tanzania ni utawala thabiti wa kimabavu(Levitsky na Way, Patronage 35).
Chini ya hali kama hii, uwanja wa michezo uliendelea kuelea kwa chama tawala. Uwanja huu potofu unafafanuliwa na Levitsky na Way kama:matumizi mabaya ya mamlaka ya serikali na wale walio madarakani, na husababisha tofauti katika upatikanaji wa rasilimali, vyombo vya habari au taasisi za serikali, wakati vyama vya upinzani unaathiriwa sana katika mashindano ya nyadhifa za serikali (Levitsky na Way 36).
Morse alidokeza kuwa tawala za mabavu ya ushindani zinaweza kushinda uchaguzi kwa kura nyingi (Morse 658). Kupitia utafiti juu ya CCM na Chadema, Morse alidhani kuwa ushindani wa Tanzania ulitokana na muundo wa chama tawala kwa mfumo wa ushirikiano wa kijamii ulioanzishwa wakati wa utawala mrefu wa chama kimoja.
Ndamungu alichambua jinsi mamlaka ya matawi matatu nchini Tanzania yalivyogawa, akasema kwamba kuwa mamlaka yako mikononi mwa rais, na madaraka ya utekelezaji wa kiserikali na madaraka ya urais nchini Tanzania hayatengani (Ndamungu 82).
Paget (Opposition 158) anasema pamoja na kwamba Tanzania ilianzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, ingali ina muundo wa utawala wa kimabavu.Kiwango cha kukubalika kwa CCM kulishuka kutoka 68% mwaka 2005 hadi 18% mwaka 2015. Inamaanisha kuwa uwiano kati ya chama tawala na chama cha upinzani umebadilika. Alisema kuwa tangu mwanzoni mwa 2015, mabavu ya CCM imelekea kuudhibiti uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kukusanyika na kudhibiti nafasi ya kuwepo kwa vyama vya upinzani. Paget anahusisha ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2020 na "udanganyifu usio na kifani " wa uchaguzi huo (Paget, Landsilde 65).
Utafiti wa Levitsky na Way ulithibitisha mabavu ya ushindani iko nchini Tanzania. Nadharia yao ya nyanja nne za "uchaguzi, mahakama, sheria, na vyombo vya habari" katika tawala za mabavu ya ushindani ilitoa msingi wa utafiti huu. Tafiti za Morse, Ndamungu, na Paget zilionyesha chanzo cha mabavu ya ushindani nchini Tanzania, vipengele vya kimuundo, na mienendo ambayo imeongezeka katika uchaguzi wa hivi karibuni. Tafiti zilizotajwa zilitoa msingi thabiti wa utafiti huo.
1.2 Motisha ya Utafiti
Tukio la kusimamishwa kwa CMG ni tukio maalum ambapo utawala wa Tanzania ulitumia madaraka kudhibiti vyombo vya habari wakati wa uchaguzi mkuu wa 2020. Tukio hilo lina athari kubwa na liliripotiwa na idadi kubwa ya vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi na hata mashirika ya kimataifa. Utafiti huu ulichukua tukio la kusimamishwa kwa CMG kama kisa maalum, kisha ukatoa maoni juu ya vipengele vya vitendo vilivyochukuliwa na CCM katika uchaguzi mkuu wa 2020, na kuchungua mababu ya ushindani katika ya tukio hilo.
Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China