Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Uhakiki wa Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo III


15 April 2022 | By 宋艺婷 Monika | SISU

Sehemu ya Tatu: Dalili na Ishara za Kufufua Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo

1. Changamoto ya Virusi vya Korona

Mlipuko wa virusi vya korona uliathiri uchumi wa nchi na maisha ya wananchi duniani kote kwa kiwango tofauti. Hasa nchi za Afrika na nchi nyingi za Ulaya zilikubwa na changamoto kubwa, na zilifanya maarifa ili kuinua uchumi. Hivi sasa China ina uwezo mkubwa zaidi wa kutoa misaada kwa nchi za Afrika ikilinganishwa na nchi za Ulaya huku ikijulikana kama uchumi pekee ulimwenguni uliopata ukuaji katika janga la virusi vya korona mwaka uliopita. Kwa hiyo, ikiwa Tanzania inataka kuboresha uchumi na kuomba misaada, uwekezaji wa China utakuwa chanzo muhimu chenye nguvu.

2. Ongezeko la Mahitaji ya Huduma za Bandari

Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizotazamana na bahari. Lakini, kufuatana na utandawazi wa duniani na maendeleo ya kiuchumi ya haraka, huduma zilizotolewa na bandari zilizopo hazijakidhi haja ya mahitaji ya usafiri. Mradi wa Bandari ya Bagamoyo utasaidia maendeleo ya taifa wakati ujao, pia itachangia kutimiza lengo kwamba Tanzania iwe nchi ya kisasa.

Zaidi ya hayo, ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ukisimamishwa kwa muda mrefu, usafiri, uchumi na biashara za kienyeji zitaathiriwa, na matayarisho yaliyofanywa yatakuwa bure, yakiwemo ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaohamishwa kupisha ujenzi wa bandari.

3. Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)

Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) unaendelea kimotomoto nchini Tanzania na sasa umeingia kipande cha tano. Kama alivyotaja Spika Ndugai, ujenzi wa reli ya kisasa na ujenzi wa bandari ni sawa na mkokoteni na ng’ombe. Kwa hiyo, inafaa reli na bandari zifanye kazi pamoja ili thamani zao kubwa kabisa zitolewe.

4. Tumaini la Kufufua Mradi la Rais Samia

Baada ya kushika wadhifa wa urais, Rais Samia hakupinga mradi wa Bandari ya Bagamoyo hadharani, bali alitangaza kuwa serikali itake mazungumzo pamoja na wawekezaji ili kufufua mradi huo kwa maslahi ya taifa. Tangu hayati Rais Magufuli alipolaumu masharti magumu ya wawekezaji, mradi wa Bagamoyo ulifuata ukingo wa barafu kwa kipindi fulani. Maelezo ya kufufua mradi ya Rais Samia yalivunja mkwamo.

5. Mkondo wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Ingawa mchakato wenye kupinda-pinda na mkanganyiko wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo unaongeza tashwishi kwa mustakabali wa mradi huo, dalili zilizopo sasa zinachangia kusukuma mbele mazungumzo na makubaliano juu ya mradi wa Bagamoyo. Ni vigumu kubashiri kuwa upande upi utafanya suluhu kwanza na mkataba utarekebishwa vipi, lakini pengo lililopo baina ya pande hizi mbili linatarajiwa kuondolewa, na mradi huu unapaswa kupata maendeleo wakati wa uongozi wa Rais Samia.

Kwa upande mmoja, msingi wa ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi ni kila upande uchague na upokee vitu uhitajivyo kwa kutoa ulivyo navyo, na ubadilishaji huo hutokea kati ya maliasili na mtaji. Sasa Tanzania ndiyo nchi ambayo inajaliwa na utajiri mkubwa wa rasilimali, na China ina upendeleo na uwezo wa kuziwekeza nchi za kigeni. Kwa upande mwingine, nchi hutimiza ustawi na ufanisi wa uchumi katika jiwe la miundombinu bora. Bandari ya kisasa inachangia maendeleo ya jumla ya taifa wakati ujao. Kwa hiyo, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo unatazamiwa kuendelea kwa mafanikio.

 

Hitimisho

Tofauti kati ya Serikali ya Tanzania na China umesababisha kukwama kwa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani, na kifunguo kikuu ni swala la maslahi. Watu mbalimbali wanatoa maoni na hoja tofauti juu ya swala hili na mradi huo, na wanajadiliana kama bandari ijengwe au isijengwe. Kutokana na changamoto ya virusi vya korona, ongezeko la mahitaji ya huduma za bandari, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na sababu nyingine, Rais Samia ameonyesha tumaini la mazungumzo pamoja na wawekezaji ili kufufua mradi huu kwa tija ya wananchi. Inaonekana kwamba ingawa ni vigumu kubashiri jinsi makubaliano yatakavyosainiwa kwa kina, mkondo wa ujumla wa mradi utaelekea ufanisi. Inatarajiwa kuwa pande zinazohusika zitaweza kukunjua moyo na kumaliza tofauti ili mradi uendelee kukiwa na makubaliano kwenye mambo ya msingi wakati wa uongozi wa Rais Samia.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi