Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Uhakiki wa Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo II


15 April 2022 | By 宋艺婷 Monika | SISU

 

Sehemu ya Pili: Uhakiki wa Mkondo wa Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo

1. Mchakato Uliojipinda-pinda

Miaka minane imepita tangu mkataba wa mfumo wa mwanzo uliposainiwa, lakini mradi wa Bagamoyo bado unaendelea polepole. Hata ulisimamishwa mara mbili katikati na wabia kutokana na pande tatu, hasa China na Tanzania, hawajafikia muafaka hadi leo. Hata hivyo, inafahamika kwamba ushirikiano baina ya nchi zote duniani unahitaji mashauri, mapendekezo na mawazo katika sekta mbalimbali, na viongozi wa taifa watafanya mabadiliko na marudio baada ya kuwaza na kuwazua katika nyakati tofauti kwa miradi mikubwa ya miundombinu kama ulivyo ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ambayo athari yao inahusiana na tija ya nchi nzima.

2. Maoni Tofauti Kuhusu Mradi wa Bagamoyo

Mradi wa Bagamoyo haujakosa kupokea hoja tangu utolewe. Wananchi na viongozi nchini Tanzania na wanaofuatilia mradi huo katika nchi za ng’ambo wanatoa maoni tofauti. Kauli kutoka kwa hayati Rais Magufuli kwamba uwekezaji wenye masharti magumu hautakuwa na tija kwa taifa zaidi ya kuwaumiza Watanzania, iliongeza mkanganyiko miongoni mwa wananchi. Watu wote wanagawanyika katika makundi mawili, yaani Bandari ya Bagamoyo ijengwe au isijengwe. Watu wa kundi la kwanza walimkubali Kiongozi Mkuu wa nchi na kuamini masharti hayo magumu hayakubaliki. Aidha, walitoa hoja kuhusu maana na umuhimu wa bandari kubwa ya Bagamoyo kwa kuwa kumekuwa na bandari kadhaa kando ya ujenzi huo, kama vile bandari ya Dar es Salaam, ya Zanzibar na ya Tanga.

Na wengine wa kundi la pili hawakuridhishwi na mchakato wa mradi wa Bagamoyo na walifikiri bora bandari ijengwe kwa sababu italeta maslahi kubwa kwa Tanzania. Miongoni mwao, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai aliwahi kulalama mara kadhaa kwamba serikali inafanya makosa kutoendelea na mradi huo kwa vile una faida kubwa, pia alieleza kwamba sasa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) nchini Tanzania bila ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ni sawa na kuweka mkokoteni mbele halafu ng’ombe nyuma, kwa sababu wengine huanza kujenga bandari, ndiyo halafu wanajenga reli.

3. Kiini cha Mkanganyiko: Maslahi

Kiini cha mkanganyiko baina ya China na Tanzania ni maslahi, ambayo pia ni ufunguo wa mawasiliano na ushirikiano wa nchi zote duniani. Masharti ya wawekezaji yalitolewa kama fidia ya fedha kwa China. Tangu China ilipopiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi, ilianza kufanya jitihada ili kuongeza sauti katika jukwaa la kimataifa, na njia mojawapo ni Pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja, ambalo linaunganisha dunia na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi zote duniani kupitia njia ya maji. Tanzania ni kituo muhimu katika Pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja. Kwa hiyo, wawekezaji kutoka China waliona fursa ya Eneo la Uwekezaji wa Biashara katika mji wa Bagamoyo kwa sababu ya urahisi wa kusafirisha bidhaa kutoka eneo la Maziwa Makuu kwenda kwingineko duniani. Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo bila shaka utaleta faida kubwa kwa Tanzania, lakini Tanzania pia italipa fidia na deni kubwa. Ingawa miradi mikubwa ya miundombinu huwavutia viongozi wa Kiafrika, uchumi wa nchi na hali ya kimataifa inawabidi wawe waangalifu zaidi kukubali miradi ya aina hii ili kuhakikisha uwiano kati ya deni na maendeleo ya kweli. Tanzania ilikuwa na deni kubwa kutoka China na nchi za magharibi. Ni dhahiri kwamba fursa huenda sambamba na changamoto. Viongozi wa Tanzania wanapaswa kutafakari kama watapokea misaada.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi