Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Uhakiki wa Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo I


15 April 2022 | By 宋艺婷 Monika | SISU

 

Sehemu ya Kwanza: Kujulisha Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo

1. Utangulizi

Mji wa Bagamoyo ulijengwa na wafanyabiashara Waarabu zaidi ya miaka 1,000 iliyopita, na baadaye ulikuwa bandari ya biashara ya watumwa. Mwanzoni mwa utawala wa Waarabu na Wajerumani nchini Tanzania, Bandari ya Bagamoyo ilikuwa nguzo muhimu wa uchukuzi wa Afrika ya Mashariki.

Kutokana na msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam na ongezeko la mahitaji ya huduma na teknolojia za kisasa za meli, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ilipendekeza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, ili Tanzania iendelee kuwa kitovu cha usafiri wa maji katika eneo la Afrika ya Mashariki. Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ulianzishwa na pande tatu, yaani serikali ya Tanzania, Kampuni ya China Merchants Holdings International (CMHI) na State General Reserve Fund (SGRF) kutokana na Oman. Mradi huo ulilenga kuanzisha Ukanda Maalumu wa Uchumi (Special Economic Zone) kando ya bandari hii, zikiwemo bustani za viwanda, bustani za utalii, eneo la biashara huria, bustani za kisayansi na kiteknolojia na zinginezo. Baada ya kukamilika, Bandari ya Bagamoyo itakayogharimu dola bilioni 10 itakuwa na uwezo wa kupokea mizigo zaidi ya mara 20 ya Bandari ya Dar es Salaam, hivyo ndivyo itakuwa mmojawapo kati ya miundombinu mikubwa kuliko yote iliyoendeshwa na serikali ya Tanzania.

2. Utaratibu wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Mkataba wa mfumo wa mradi huo ulisainiwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete wa Tanzania tarehe 24, Machi, mwaka 2013, wakati Rais Xi Jinping wa China alipofanya ziara nchini Tanzania. Mkataba wa kuanza ujenzi wa bandari ulitiwa saini mnamo Oktoba, mwaka 2015, na Rais Kikwete alitangaza kuwa ujenzi wa hatua ya kwanza ya mradi huo ulikuwa utakamilika mwaka 2017. Lakini, hayati Rais John Magufuli aliposhika wadhifa wa urais mwaka 2015, mradi wa Bagamoyo ulisimamishwa kwa kuwa serikali iliweka kipaumbele cha uboreshaji wa bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga na miradi mingine iliyonufaisha taifa. Aidha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alieleza kwamba ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo utakaogharimu mabilioni ulikuwa mkubwa sana, na ulihitaji mipango mingi, mazungumzo ya umakini na vyanzo vikuu vya ufadhili. Hadi mwisho wa mwaka 2017, mazungumzo ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo yalionyesha dalili za kufikia muafaka. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alibainisha kwamba ujenzi huo ulitarajiwa kuanza Januari mwaka 2018.

Mwaka 2019, mradi huo ulisimamishwa tena kwa sababu China na Tanzania hazikukubaliana kuhusu masharti ya uwekezaji. Hayati Rais Magufuli alitoa ufafanuzi katika kikao maalumu kilichowakutanisha wafanyabiashara mbalimbali kutoka Tanzania nzima kwamba mashari yaliyotolewa na wawekezaji ni magumu na kichaa pekee ndiye anaweza kuyakubali. Masharti hayo ni pamoja na kuwa wawekezaji wanatakiwa kupewa muda wa miaka 33 bila kuwauliza chochote watakapokuwa wamewekeza hapo, na Tanzania isiruhusiwe kukusanya kodi katika bandari hiyo. Isitoshe, baada ya ujenzi huo wa bandari hiyo, Tanzania haitaruhusiwa kujenga na kuendeleza bandari nyingine yoyote kuanzia Tanga mpaka Mtwara.

Mnamo Aprili, mwaka huo, Waziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, Geoffrey Mwambe aliambia bunge kuwa serikali mpya chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inataka kuendelea na mradi huo ikiwa masharti magumu yabadilishwe. Tarehe 26, Juni, Rais Samia ametangaza kuwa wameanza mazungumzo ya kufufua mradi wa Bandari ya Bagamoyo pamoja na ule wa chuma na makaa ya mawe wa Mchuchuma na Liganga kwa faida ya Tanzania.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi