Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China
Soma Zaidi
Uchambuzi wa Majukumu ya Mhusika Msaidizi Najum Ⅲ
15 April 2022 | By 罗思颖Bahati | SISU
Najum aliwaza, “Maana yake nini?” Lakini tangu alipoona uhodari wa Bwana Musa wa kuweza kuchungua asili ya mambo, kama uhodari aliouonyesha katika kufahamu nani aliyemwua Bwana Ali, na kumkata kichwa namna ile, na akajua kwa nini alikatwa--jambo ambalo liliwakanganya Polisi kwa muda- Najum alikuwa tayari kumwamini kwa lolote atakalosema, ingawa alikubali kuwa ni vigumu wakati mwingine maneno yake kufahamika. (uk.2-3)
Dondoo hili linatokana na sura ya kwanza ya riwaya hii. Katika dondoo hili Najum ansamini kila kitu alichosema Bwana Musa. Kutokana na maelezo ya Najum, wasomaji wanaweza kuelewa mara moja uwezo bora wa upelelezi wa Bwana Musa na taswira ya Bwana Musa mwenye busara.
Wakati huo huo katika sura ya kwanza, maelezo mengine ya Najum pia yanaweza kuwafanya wasomaji wajue kwamba Musa ni mtu anayepata elimu bora na aliye na ujunzi mwingi. Kwa mfano, Najum anafikiri kwamba ujuzi wa Bwana Musa unapatwa kutoka katika kitabu cha Kinyume cha Mambo, Najum aliona daftari la Bwana Musa linaloandikwa maneno ya kichina ambayo hakuweza kuyaelewa na kadhalika.
1.1 Kujenga Mhusika Bwana Musa kwa Ulinganisho wa Najum na Bwana Musa
Katika riwaya hii, mara nyingi Bwana Musa na Najum hujadili kesi pamoja, lakini mawazo ya Bwana Musa ni sahihi, ila mawazo mengi ya Najum si sahihi. Kwa mfano, katika Sura ya Nane, Bwana Musa na Najum waligundua risiti katika mfuko mweusi mzimuni, na wawili hao hawakukubaliana juu ya uhalali wa risiti. Najum anafikiri kwamba risiti hii haina saini wala wakati, kwa hivyo risiti hii ni batili; lakini Bwana Musa anaamini kwamba lazima kuna sababu maalum ya risiti hii isiyo ya kawaida, kwa hivyo anadhani kuwa risiti hii ndio ushahidi muhimu wa kutatua kesi hiyo. Mwisho wa riwaya hii unathibitisha kwamba risiti hii ni muhimu sana kwa uchunguzi wa kesi hiyo.
Mjadala huu juu ya uhalali wa risiti unaonyesha njia tofauti za kufikiri za Najum na Bwana Musa, na unaangazia mtazamo wa kufikiri wa kipekee na busura ya Bwana Musa. Isingalikuwa na ulinganisho kati ya Najum na Bwana Musa, taswira ya busara ya Musa isingajengwa izuri kama hiyo.
Hitimisho
Kwa ujumla, katika Mzimu wa Watu wa Kale, majukumu ya mhusika Najum yanaonyeshwa haswa katika sehemu mbili: kusukuma maendeleo wa ploti na kujenga mhusika Bwana Musa. Hata hivyo, dhima ya wahusika wasaidizi ni nyingi zaidi ya hiyo. Wakati mwingine wahusika wasaidizi hata huwa na kazi ya kudokeza mazingira ya kijamii, ambalo ni muhimu sana kwa kufasiri riwaya. Ingawa wahusika wasaidizi sio kiini cha riwaya, lazima wawe na majumuku yao wakati mwandishi anawaweka katika hadithi. Kwa hivyo, katika uchambuzi wa fasihi, uelewa wa wahusika wasaidizi unapaswa kuimarishwa huku tukizingatia wahusika wakuu.
Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China