Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Uchambuzi wa Majukumu ya Mhusika Msaidizi Najum Ⅱ


15 April 2022 | By 罗思颖Bahati | SISU

Hapo badala ya kutoa dalili moja kwa moja kuhusu muuaji halisi Mwarabu mgeni, mwandishi, kupitia kuandishi mawazo ya mhusika Najum, anatoa sababu yenye mantiki lakini iliyo mbali na ukweli wa kesi hiyo, kwa sababu anataka kuongeza uwezekano tofauti ambao unatofautisha na ukweli atakaosema Bwana Musa mwishowe. Kwa njia hii, wasomaji watashangaa na kufurahia kupata ukweli katika mwisho wa riwaya.

1.1 Jukumu la Kupanga ploti za Hadithi

Mtazamo wa mhusika Najum katika uchunguzi wa kesi ya jinai unafanana na ule wa wasomaji, kwa sababu mwandishi anampa Najum mipaka ya mtazamo, yaani Najum hawezi kuelewa kila kitu kuhusu kesi hiyo. Mwandishi anamfanya mhusika Najum aulize maswali kuhusu kesi hiyo, ili kukuza uibukaji wa habari muhimu zinazosaidia kutatua kesi hiyo.

Najum naye alijitia akasema, “Ndiyo, nakubali aliuza mali yake kutaka kusafiri; lakini kwa nini alifanya hayo kwa siri yake na hofu yake iliyomjia kwa ghafula?” (uk. 73)

Dondoo hili inatokana na Sura ya Kumi na Nne ya riwaya hii. Kabla ya Najum kuuliza swali hili, Musa alikuwa ameeleza kikamilifu kwa nini Baniani hakuwa muuaji, na akasema kwamba Mwarabu mgeni ndiye muuaji halisi. Katika ploti inayofuata, Musa anahitaji kueleze waziwazi sababu ya Mwarabu mgeni kumwua Ali.

Kwa ajili ya kupanga ploti, mwandishi alimfanya Najum aulize swali wakati wa ufafanuzi wa Bwana Musa. Hapa kupitia swali hili lililoulizwa na Najum, mwandishi anabadilisha sisitizo ya maelezo ya Bwana Musa. Kwa njia hii, Bwana Musa anaweza kubadilika kutoka kueleza kwamba Baniani hakumwua Ali, hadi kutoa sababu ya mauaji ya Mwarabu mgeni.

 

Hali kadhalika, Najum pia aliuliza maswali mara kwa mara wakati wa kuchunguza kesi pamoja na Bwana Musa. Kwa mfano, katika Sura ya Saba ya riwaya hii, Najum na Bwana Musa walipogundua mfuko mweusi pamoja, aliuliza maswali yafuatayo kwa mfululizo:

Najum alisema, “Unajua, we! Hapana shaka huu ni mfuko wa Bwana Ali na hii hasa ndiyo hati yake. Lakini umefikaje hapa?”

Najum aliuliza, “Vema, lakini wao wameupata wapi?”

Najum aliuliza, “Kitu gani? Mfuko tumeuokota vivi hivi hali umefungwa. Kama mlikuwa na kitu ndani yake, basi kimekwenda wapi?” (uk. 29-30)

Maswali haya yaliyoulizwa na Najum ndio maswali ambayo wasomaji watakuwa nayo wakati wa kusoma, kwa hivyo wasomaji watajiingiza katika ploti hizi, kufuata maswali ya Najum ili kuelewa hali katika eneo la uhalifu na uhusiano kati ya wahusika waliomo riwaya hii. Aidha, mfululizo wa maswali aliyouliza yatajibiwa moja baada ya jingine wakati wa kutatua kesi hiyo, ambayo pia huweka msingi wa maelezo ya Bwana Musa na kufanya maelezo yake kuwa yaliyo na mantiki zaidi.

 

2. Majukumu ya Mhusika Najum katika Kumjenga Mhusika Mkuu Bwana Musa

Katika Mzimu wa Watu wa Kale, mhusika Najum alitokea tangu mwanzo wa riwaya pamoja na Bwana Musa, lakini ni dhahiri kwamba mwandishi hatii mkazo katika ujenzi wa taswira ya mhusika Najum, anazingatia taswira ya mhusika mkuu Bwana Musa kupitia mhusika huyu msaidizi Najum.

2.1 Kujenga Mhusika Bwana Musa kwa Kueleza Vitu Najum Anavyoona na Anavyofikiri

Katika riwaya za upelelezi, mwandishi humsawiri mpelelezi kuwa mtu mwenye ujuzi mwingi na uwezo mkubwa. Katika mwanza wa riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale, mwandishi anatumia vile Najum anavyoviona na anavyofikiri ili kumjenga mhusika Bwana Musa.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi