Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China
Soma Zaidi
Uchambuzi wa Majukumu ya Mhusika Msaidizi Najum Ⅰ
15 April 2022 | By 罗思颖Bahati | SISU
Utangulizi
Mpelelezi ndiye mhusika mkuu katika riwaya ya upelelezi, lakini mwandishi anahitaji kubuni baadhi ya wahusika wasaidizi huku akibuni mhusika mkuu. Katika Mzimu wa Watu wa Kale, Najum ni mmojawapo wa wahusika wasaidizi. Ingawa Najum ni mhusika msaidizi, ana majukumu muhimu katika utunzi wa riwaya nzima. Katika Mzimu wa Watu wa Kale, mhusika Najum ana majukumu mawili makuu hasa: moja ni kukuza maendeleo ya ploti za hadithi, na lingine ni kusaidia kumjenga mhusika mkuu Bwana Musa.
1. Majukumu ya Mhusika Najum katika Ploti
Riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale inachukua njia ya utunzi inayozingatia ploti, na hivyo mpangilio wa wahusika hutumikia ploti zenyewe. Katika Mzimu wa Watu wa Kale, mwandishi hutumia wahusika wengi kutimiza madhumuni ya kupanga ploti, na Najum ni mmojawapo wa wahusika hayo. Jukumu la mhusikaNajum katika ploti linaonyeshwa hasa katika sehemu tatu zifuatazo:
1.1 Jukumu la Kutoa Kesi ya Jinai Mwanzoni mwa Hadithi
"Kutoa kesi ya jinai → Kuchunguza kesi→Kutatua kesi” ni muundo wa kawaida wa riwaya za upelelezi. Riwaya nyingi za upelelezi zinahitaji kwamba mwandishi anatega mafumbo upesi na kuwaletea wasomaji shaka mwanzoni mwa hadithi. Katika Mzimu wa Watu wa Kale, mwandishi anamtumia mhusika msaidizi Najum kukamilisha kazi hii.
Najum karudi jana kutoka shamba na Bwana Musa, baada ya kukunjwa tanga la Bwana Ali, na wamemwacha Ahmed mfiwa, huko shamba akitengeneza zaidi mambo yaliyomhusu maiti, baba yake. (uk. 1)
Katika sura ya kwanza ya riwaya hii, Najum alikuja nyumbani kwa Bwana Musa katika siku ya pili baada ya kuhudhuria mazishi ya Ali. Kupitia kubuni ploti ya “Najum kuja nyumbani kwa Bwana Musa”, mwandishi analeta mazungumzo kati ya Bwana Musa na Najum, na analeta kisa cha msingi cha riwaya hii, mauaji ya Ali. Hivyo, wasomaji wanaweza kuingia katika hadithi ya riwaya hii kwa haraka.
1.2 Jukumu la Kuongeza Uwezekano Tofauti wa Ploti
Wakati wa kubuni matatanisho ya hadithi, mwandishi huweka madokezo tofauti. Miongoni mwao madokezo hayo, meingine yanawaelekeza wasomaji wapate ukweli wa kesi wa jinai, na mengine yanavuruga fikra ya wasomaji kuhusu kesi hiyo.
Najum alipotazama, alimwona yule kijana anakimbia mbio, na hivi sasa kaisha fika mlango wa Mzimu wa Watu wa Kale, anaingia na kanzu yake begani. Kuona vile, Najum alimsuta Bwana Musa, “Je, mimi sikukuambia? Yawezekana kuwa yule ndiye aliyeua; sasa si yule anakimbia? Anakimbia nini hasa kama si yeye aliyeua?” (uk. 47-48)
Dondoo hili inatoka kwa Sura ya Tisa ya riwaya hii. Najum na Bwana Musa walimwuliza Boi wa Baniani nyumbani kwa Baniani, mara baada ya wao kufika mahali ambapo kunguru wengi walitua, wakamwona Boi akikimbia. Najum alidhani kwamba huenda Boi ndiye muuaji, kwa sababu Najum aliona kwamba Boi alikuwa amejua watu kadhaa walikuwa wakichunguza mauaji ya Ali, na Boi alikimbia kwa kuwa aliogopa kukamatwa. Sababu hiyo ya Najum ina mantiki fulani. Wasomaji wanaposoma haya, wao hufuata mawazo ya Najum na kufikiri kwamba huenda Boi ndiye muuaji. Lakini kulingana na tamati ya riwaya hii, Boi si muuaji, Mwarabu mgeni ndiye muuaji halisi.
Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China