Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China
Soma Zaidi
Ufafanuzi wa Riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale III
15 April 2022 | By 褚予钦 Jamila | SISU
III. Ujumla wa Majukumu ya Bwana Musa na Inspekta Sefu
Kwa kutegemea utambulisho wake usio rasmi au kiserikali, Bwana Musa alifanya uchunguzi na upelelezi wake kwa hiari kuhusu kesi hiyo, na mwishowe kumfungia mwuaji halisi kwa upesi sana. Ni muhimu kuzingatia kwamba alipata habari nyingi muhimu kwa njia maalum ya kuzungumzana na mashahidi. Kwa mfano, alimwambia Boi wa Baniani kuwa kuna damu kwenye nyumba, ambayo ilimwogopesha sana; alimwuliza Mmanga kwa ghafla kwamba “mgeni wako naye hajambo?”, na akapata kujua kuwa yule mgeni alikuwa mzima na mwenye nguvu sana; alimwuliza Baniani kama anapenda pesa, na kisha kumlazimisha aseme ukweli wa siku ile ya kesi.
Inspekta Sefu naye alisaidia sana katika upelelezi wa kesi hiyo. Alikuwa polisi hodari sana, hata alipanda kutoka askari polisi hadi inspekta miaka mitatu tangu kuingia kazi ya polisi. Katika hali ya kukosekana kwa ushahidi muhimu, pia alitoa makisio mengi sahihi, kama alivyosema baada ya kuchunguza palipo kichwa na maiti kuwa, lazima Baniani yumo katika mambo haya. Pia alithibitisha kutokana na jeraha kwamba mwuaji lazima awe na nguvu sana, na ingawa kulikuwa na washirika wengine, lazima kuwe na mwuaji mmoja tu. Hatimaye, kwa msaada wa mwanafunzi mwenzake wa zamani Musa, alimkamata mwuaji kwa wakati.
Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China