Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Uhakiki wa Mabadiliko na Changamoto za Hatua dhidi ya COVID-19 nchini Tanzania


02 September 2021 | By 罗思颖Bahati | SISU

[Muhtasari] Nchi za Afrika Mashariki zinakabiliwa na wimbi la tatu la COVID-19, miongoni mwao, hali ya janga la Tanzania inastahili kuzingatiwa. Nakala hii italinganisha hatua za kupambana na COVID-19 zilizotekelezwa na Rais Samia na Rais mtangulizi Magufuli, na pia kuchunguza shida halisi zinazokabili Tanzania wakati wa kuchukua hatua za kupambana na COVID-19 kutoka pande za ufichuzi wa data, upatikanaji wa chanjo, mgawanyo wa chanjo na kupiga kwa chanjo.

[Maneno Makuu] hali ya COVID-19 ya Afrika Mashariki, Tanzania, suala la chanjo

Baada ya mlipuko wa COVID-19 ulimwenguni, nchi za Afrika Mashariki zimeathiriwa moja baada ya nyingine. Hadi Tarehe 16 Julai, 2021, Kenya imekuwa na watu 190,000 walioambukizwa na COVID-19, na Rwanda iliyo na idadi ndogo ya watu zaidi kuliko nyingine zote barani Afrika Mashariki pia imekuwa na watu 50,000 walioambukizwa na virusi hivyo. [] 

Kati ya nchi hizo, inaonekana kwamba Tanzania imesahauliwa na watu wa sehemu nyingine za dunia tangu Rais wa zamani Magufuli alipotangaza ushindi katika vita dhidi ya janga la COVID-19 mnamo Tarehe Juni, 2020. Lakini, kutokana na uteuzi wa Rais mpya Samia, hali ya kuzuia kwa janga la COVID-19 Tanzania imezingatiwa tena. Kwa hivyo, nakala hii italinganisha hatua za kuzuia kwa COVID-19 zilizotekelezwa na Rais Samia na Rais mtangulizi Magufuli, na kutoa maoni yangu kuhusu hatua mpya zilizochukuliwa na Rais Samia.

1. Hali ya Jumla ya COVID-19 ya Tanzania

Mnamo Tarehe 19 Machi, 2020, Tanzania ilitangaza kesi ya kwanza ya maambukizo ya COVID-19. Mwanzoni mwa mlipuko, Tanzania, kama nchi nyingine jirani za Afrika Mashariki, ilichukua hatua za kisayansi kujikinga na COVID-19. Lakini, kadiri idadi ya watu walioambukizwa inavyoendelea kuongezeka, hatua za kuzuia virusi hivyo zimepata mabadiliko makubwa. Rais Magufuli alihoji ufanisi wa chanjo na barakoa, na akaanza kutekeleza hatua mbili kuu, yaani kuomba Mungu na kutumia dawa za miti shamba. Isitoshe, alikuza njia kama vile tiba ya mvuke na kula limau na tangawizi kupambana na janga hilo. Tanzania iliacha rasmi kusasisha hali ya COVID-19 kila siku tangu tarehe 8 Mei, 2020, na mwezi mmoja baadaye ikatangaza kuwa Tanzania imeshinda mapambano dhidi ya janga hilo.

Walakini, baada ya Samia kuwa rais mpya mnamo Machi mwaka huu, alichukua hatua tofauti kabisa na rais wa zamani ili kupambana na COVID-19. Rais Samia aliwaambia wananchi kuwa virusi vya Korona bado vipo nchini Tanzania, na akatoa wito kwa watu kunawa mikono mara kwa mara, kuvaa barakoa na kuweka umbali wa kijamii kwenye Twitter.

Viwanda nchini Tanzania pia vimeongeza uzalishaji wa vifaa vya kinga. Mnamo taerehe 16 Aprili, Rais Samia alitangaza rasmi kuanzishwa kwa kamati ya wataalam ili ishauri kazi ya serikali kupambana na COVID-19[]; katika tarehe 17 Mei, kamati hiyo ya wataalam iliwasilisha ripoti ya tathmini ya janga hilo kwa Rais Samia, na kusisitiza umuhimu wa kupata chanjo.[]

Mnamo tarehe 28 Juni, Tanzania ilitangaza rasmi kushiriki katika mpango wa COVAX na kuwekeza dola milioni 470 kununua chanjo. Rais Samia pia alitangaza kwa mara ya kwanza kwamba kumekuwa na wagonjwa wapatao 100 walioambukizwa na COVID-19 nchini Tanzania, miongoni mwao watu asilimia 70 ni wagonjwa mahututi[]; mnamo tarehe 8 Julai, Tanzania ilitangaza rasmi kuwa watu 408 walioambukizwa na COVID-19, kati yao watu 284 ni wagonjwa mahututi.[] Katika siku 10 tu, idadi ya maambukizo mapya imeongezeka kwa karibu 300%, tena idadi ya wagonjwa mahututi imefikia asilimia 70. Takwimu hizi zimeonyesha ukali wa hali ya COVID-19 nchini Tanzania. Inaonekana kwamba kuna hatari ya mlipuko mkubwa wa Korona nchini Tanzania.

Kwa kulinganisha hatua za zamani na za sasa za kuzuia COVID-19 nchini Tanzania, ni dhahiri kwamba Rais Samia amechukua hatua za kisayansi zaidi kuliko Rais Magufuli. Ingawa Rais Samia na Rais Magufuli wana mitindo tofauti kabisa ya kuzuia janga, lakini hawa wawili hawajachukua hatua kali za kupambana na COVID-19. Nafikiri kwamba hii inaonyesha mantiki yao katika maamuzi wa kupambana na COVID-19, yaani kuhakikisha uchumi na amani ya nchi. Hatua kali za kuzuia janga, kama vile kufungwa kwa miji mikubwa na kufungwa kwa maduka anuwai, zote zinawezekana kusababisha ugumu wa kiuchumi na machafuko ya kisiasa nchini Tanzania. Kumekuwa na mfano hapo awali. Mnamo tarehe 23 Machi, 2020, baada ya mamlaka nchini Niger kufunga msikiti na kumkamata mchungaji ambaye alikiuka marufuku ya kinga za COVID-19, ghasia zilizuka katika eneo hilo; na pia katika Machi mwaka huu, baada ya miji mingi kufungwa huko Kenya, madereva wa teksi walipinga na kusema kwamba hatua za kufunga miji kumeleta athari mbaya kwa maisha yao. []

Kwa maoni yangu, hatua kadhaa za kupambana na COVID-19 za Rais Samia zinajaribu kutafuta maendeleo wakati wa kuhakikisha uchumi wa usalama wa Tanzania, ambazo kwa ujumla zinalingana na hali ya msingi ya taifa la Tanzania.

2. Changamoto za Hatua za Kupambana na COVID-19 Tanzania

Ikilinganishwa na hatua za kipekee za Rais mtagulizi Magufuli, hatua zilizochukuliwa na Rais Samia zimesifiwa na Shirika la Afya la Dunia. Lakini, ufanisi wa hatua zinazotekelezwa nchini Tanzania hautegemii sifa zilizotoka kwa mashirika na nchi nyingine duniani. Ingawa Samia amechukua hatua anuwai ambazo zinakidhi matarajio ya kimataifa, lakini ningependa kuuliza, je, hatua hizi kweli zinaweza kudhibiti COVID-19 Tanzania kama tulivyotarajia? Katika yaliyomo ifuatayo, nitachunguza shida halisi zinazokabili Tanzania wakati wa kuchukua hatua za kupambana na COVID-19 kutoka pande za ufichuzi wa data, upatikanaji wa chanjo, mgawanyo wa chanjo na kupiga kwa chanjo.

Kwanza kabisa, kukosekana kwa ufichuzi wa hali ya kila siku ya COVID-19 kunawezekana kusababisha kupotoka kwa uelewa wa umma juu ya hali ya kudhibiti ya COVID-19. Kwa upande mmoja, Rais Samia hajatumia njia ya kusasisha hali ya COVID-19 kila siku. Tangu Machi mwaka huu, serikali ya Tanzania ilifichua hali ya janga hilo mara mbili tu katika tarehe 28 Juni na tarehe 8 Julai. Hii haisaidii kutoa miongozo ya kudhibiti Korona kwa umma. Kwa upande mwingine, raia hupata habari kupitia njia anuwai, zikiwemo kupata habari kwenye mtandao wa kijamii, kusimuliwa na watu wengine na kadhalika. Raia hawana uwezo wa kutosha kuthibitisha ukweli wa habari baada ya kuzipata, na kisha kusambaza habari hizo tena. Kwa hivyo, watu huchanganyikiwa na "habari za uwongo”. Nadhani utaratibu wa kutoa habari uliochukuliwa na Rais Samia katika kipindi hiki bado una hatari kubwa. Hivyo inawezekana kwamba Tanzania itakosa fursa muhimu ya kuzuia Korona na hata kukabiliwa na kulipuka kwa COVID-19 kwa kiwango kikubwa nchini Tanzania.

Pili, wakati wa chanjo kuwasili Tanzania haujakuwa na uhakika, na shinikizo la la Tanzania kupambana na COVID-19 bado ni kubwa wakati chanjo bado hazijapatikana. Mnamo tarehe 28 Juni, Tanzania ilisaini mkataba wa agizo la chanjo wa COVAX, kwa kufuata utaratibu wa mgawavyo wa chanjo wa COVAX, katika hali nzuri kabisa, Tanzania itapata chanjo hiyo mwisho wa Januari 2022[]. Lakini hali halisi siyo nzuri kama tulivyoona. Ingawa makubaliano ya agizo ya chanjo yamefikiwa, inawezekana chanjo hazitafika Tanzania kwa wakati. Mnamo Mei mwaka huu, mlipuko mpya wa COVID-19 ulitokea nchini India. India ilitangaza kusitisha kusafirisha chanjo kwa nchi za nje, na kupanga kurejesha usambazaji wa chanjo baada ya mwaka 2021. India, kama muuzaji mkuu wa chanjo ya COVAX, imesababisha moja kwa moja upungufu wa usambazaji wa chanjo ulimwenguni. Mwelekeo wa janga hilo ulimwenguni bado haujafahamika, na hatuwezi kuhakikisha kuwa hakutakuwa na visa kama "janga lisilodhibitiwa nchini India" ambalo litazuia usambazaji wa chanjo siku zijazo. Je, kweli Tanzania itapata chanjo iliyopangwa mnamo Februari mwakani? Kabla ya watu nchini Tanzania kupewa chanjo, bado kuna pengo kubwa katika kuzuia COVID-19.

Tatu, baada ya chanjo kufikwa Tanzania, kutoa na kupiga kwa chanjo bado kutakabiliwa na ugumu mkubwa. Kwa upande mmoja, uwezo wa sasa wa kuhifadhi na kusafirisha chanjo nchini Tanzania ni dhaifu, ambayo inawezekana kuzuia usambazaji wa haraka wa chanjo. Mfumo wa usafirishaji wa Tanzania sio mzuri, na uhifadhi wa chanjo una mahitaji makubwa juu ya halijoto na muda. Hii inafanya usafirishaji wa chanjo kwenda kwenye vitongoji na vijiji nchini Tanzania kuwa na shida kubwa. Kwa upande mwingine, Watanzania huenda hawataki kupata chanjo. Rais wa zamani Magufuli alikuwa mkosoaji wa chanjo. Uamuzi wake juu ya chanjo umeathiri mitazamo ya idadi kubwa ya Watanzania kuhusu chanjo hadi sasa. Mashaka ya muda mrefu juu ya ufanisi wa chanjo hayawezi kubadilishwa kwa haraka, kwa hivyo ni vigumu kutimiza lengo la watu kupata chanjo kwa kiasi kikubwa. Katika kipindi hiki, ikiwa mamlaka ya Tanzania inayoongozwa na Samia hayana uwezo wa kutosha kujenga utaratibu wa kushughulikia shida zitakazokuwepo katika kutoa na kupiga kwa chanjo, inawezekana kwamba chanjo zitaharibiwa kwa sababu ya kuisha muda kwa chanjo.

Kutokana na mambo nilivyoeleza hapo juu, tunaweza kuelewa kwamba chini ya hali mpya ya sasa ya COVID-19 nchini Tanzania, kuna njia mbili kuu kutatua shida hizo. Moja ni kuamsha ufahamu wa wananchi juu ya kinga ya Korona, na nyingine ni mageuzi katika utawala wa serikali.

Kwanza, sasa jambo muhimu zaidi ni kwamba serikali inahitaji kuongeza utangazaji wa mbinu za kuzuia Korona na umuhimu wa chanjo. Kwa mfano, katika jamii wafanyakazi wa jamii wanapaswa kuelezea umuhimu wa chanjo kwa wakaazi wa eneo hilo; katika vyombo vya habari, serikali inapaswa kutangaza maarifa ya kuzuia janga kwenye tovuti rasmi za habari, majukwaa ya kijamii, na vipindi vya runinga, ili raia wawe na mtazamo sahihi juu ya kuzuia Korona hatua kwa hatua.

Pili, kwa Tanzania ambayo haina fedha za kutosha, ni muhimu kutafuta ushirikiano wa kimataifa na kupandikiza uzoefu wa hali ya juu kutoka nchi zingine, ili kuboresha uwezo wa serikali kupinga janga hilo kwa kasi. Kwa mfano, Tanzania inaweza kutafuta msaada wa fedha kutoka kwa mashirika ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia kununua vifaa ambavyo vinakidhi mahitaji ya uhifadhi wa chanjo; pia inaweza kufanya majadiliano ya kiufundi na nchi ambazo zinamiliki teknolojia ya chanjo, na kujaribu kuifanya Tanzania iwe na uwezo wa uzalishaji wa chanjo kadri iwezavyo.

Hitimisho

Kwa muhtasari, naamini kwamba ingawa Tanzania imechukua hatua za kisayansi kudhibiti janga hilo baada ya Rais Samia kuingia madarakani, ufanisi wa hatua zake unabaki kupimwa katika siku za mbele, na matayarisho yake ya kukabiliana na "shida za chanjo" pia yanahitaji kuchunguzwa zaidi. Walakini, sasa iko katika hatua za mwanzo za kuzuia na kudhibiti Korona Tanzania, ni mapema sana kutabiri athari ya mwisho ya hatua hizo. Ufuatiliaji zaidi wa muda mrefu wa COVID-19 Tanzania unahitajika ili kuchanganua ufanisi wao.

COVID-19 imekuwa ikiendelea duniani kote, na nchi zote duniani zinahitaji kufikiria jinsi ya kuishi na janga hilo. Kwa kifupi, hali ya COVID-19 ya Tanzania na vitendo vya kuzuia janga hilo nchini Tanzania, zote zimeonyesha changamoto zilizofichika za COVID-19 Tanzania. Katika kipindi hiki, inaibidi Tanzania ijiandae vizuri kwa hali mbaya zaidi wakati rasilimali za matibabu za nchini ni za hali ya chini.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi