Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Bahati na Mumewe


06 August 2021 | By 宋艺婷Monika | SISU

Dibaji

Bahati na Mumewe ni hadithi nzuri niliyosoma katika kozi ya Tamthilia ya Kiswahili:
      Bahati ni msichana mzuri wa kupendeza, na aliishi pamoja na wazazi wake na binamu yake Sina-Kitu. Siku moja, mgeni aitwaye Tetemeko alikuja kusafiri katika nchi hiyo, na watu waliamini kuwa yeye ni kijana mcheshi na hodari. Tetemeko alieleza alitoka nchi ya Raha, kule jua linakopambazukia, yaani mwisho wa dunia. Alipendana na Bahati na kumchumbia. Watu wote waliwatakia heri vijana hao wawili, ila Sina-Kitu alionyesha kutofurahi. Baada ya kufunga ndoa, Tetemeko na Bahati walianza kurudi katika nchi ya Raha pamoja na Sina-Kitu. Baada ya siku saba ya safari ya kuchosha, walifika nyumba ya Tetemeko na kulakiwa na ndugu zake sita. Wakati Bahati na Sina-Kitu walipokaa nyumbani, Sina-Kitu aligundua siri ya Tetemeko. Kumbe yeye na ndugu zake wote ni wanyama wa kutisha, walitaka kuwala Bahati na Sina-Kitu baada ya kuwanenepesha. Sina-Kitu alimwambia Bahati kutoroka, lakini Bahati hakumwamini hata kidogo. Wakati wanyama walipotokea mbele ya Bahati na kutaka kumla, Bahati aliogopa sana na kuomba Sina-Kitu kumwokoa. Sina-Kitu alikuwa amesuka mkeka kwa majani ya ukindu ulioweza kuruka na kumwokoa Bahati, wakaponea chupuchupu. Mwishowe, walirudi nyumbani kwa usalama.

Nilitunga hadithi yangu kwa kutegemeana na msingi wa Bahati na Mumewe. Inabadilika kuanzia safari ya kwenda nchi ya Raha, na mambo yasiyotarajiwa yalitokea...

 

Onyesho la Pili

Tetemeko, Bahati na Sina-Kitu walianza safari ya kwenda nchi ya Raha. Walipita milima, mabonde, mito, na bahari. Bahati na Sina-Kitu walishangaa sana jinsi yule farasi alivyoweza kukimbia juu ya bahari bila kuzama, pia waliduwaa hawakukutana na wanyama wowote wengine safarini. Wakati wote huo wa safari, Tetemeko hakuwa anazungumza mengi. Hali hii ilimsikitisha Bahati kwani alishindwa kuelewa mumewe alikuwa anawaza nini. Sina-Kitu pia alikuwa ananyamaza tu. Lakini Bahati hakutaka kumjali na kuzungumza naye.

Wakati walipopita msitu mkubwa, alitokea simba mkubwa mkali. Tetemeko alisimamisha farasi yake mara moja. Simba alitembeatembea mbele yao na kunguruma kwa sauti kubwa. Ghafla alimrukia Tetemeko. Bahati alipiga kelele kwa hofu. Tetemeko, Bahati na Sina-Kitu walianguka kwenye ardhi. Simba aligongana na farasi, kumpiga makucha na kumwua. Halafu aligeuka nyuma, kutembeatembea na kunguruma kwa watu hao watatu tena.

Bahati: Tetemeko, mume wangu! Tutafanya nini sasa! Simba huyu ni mkubwa na mkali. Atatuua sisi sote! Mungu wangu eh!

Tetemeko: Mke wangu Bahati, utulie! Nitapigana naye. Nitakulinda wakati wowote kwa nguvu zangu zote. Usiwe na wasiwasi. (Alichomoa simi yake.)

Bahati: Oh mume wangu! Kweli wewe ni shujaa wangu! Naamini utashinda!

(Mara Tetemeko alitaka kwenda kwa simba na kupigana naye, mzee mmoja alitokea kutoka miti mingi.)

Mzee Hekima: Ngoja kwanza, kijana! Ngoja kidogo! (Alipapasa kichwa cha simba, na simba alitulia na kukaa. Kisha aligeuka kwa Tetemeko.) Habari za mchana, kijana maridadi? Na ninyi je, wasichana warembo?

Bahati: Mzuri sana, asante mzee. Je, mzee, ulimtambua simba huu mkali? Kwani inaonekana kwamba yeye ni mtulivu sana mbele yako!

Mzee Hekima: (kwa kucheka) Ndiyo, ndiyo. Jina langu ni Hekima. Simba huyu ni rafiki yangu. Tuliishi pamoja kwa muda mrefu sana. Ninapenda kutembelea nchi nyingine nikiwa na nafasi. Na kila ninapofunga safari, simba huyu anakwenda pamoja nami. Yeye ni mtundu sana, anapenda kufanya mzaha. Msidhuriwe naye? Kama mna hasara, naomba mmsamehe. Ninataka kumlipia hasara yenu.

Bahati: Sisi tuko wazima, ila farasi wetu aliuawa na simba... (Aligeuka kwa Tetemeko, lakini Tetemeko hakusema kitu. Bahati aliduwaa moyoni.)

Mzee Hekima: Pole! Kweli simba wangu alikosea sana mara hii. Bora mje nchi yangu kununua farasi mypa, si mbali kutoka hapa. Naona mna mizigo mingi, na haiwezekani kusafiri bila ya farasi. Ninasikitika sana kwa matendo ya simba wangu. Basi njooni nchi yangu ya Simba, inapendeza sana. Nitawatayarisheni chakula kitamu na malazi mazuri. Nitawanunulieni farasi mpya maridadi! Zaidi ya hayo, watu wa nchi yangu ni wakarimu na watawakaribisheni wageni kwa mikono miwili!

Sina-Kitu: (kwa sauti ndogo) Nchi ya Simba?

Bahati: Hivyo ni sawa, mzee. Mume wangu, unaonaje? (Tetemeko bado hakusema kitu. Ilionekana aliwaza kuhusu jambo fulani.) Mume wangu, uko sawa?

Tetemeko: Niko sawa, Bahati mpenzi wangu. Niliona huzuni kwa sababu ya kifo cha farasi wangu tu. Alifuatana nami kwa miaka mingi. Basi nafikiri ni afadhari twende nchi ya Simba kwanza tukanunue farasi mpya. Mzee, nashukuru wema wako. Hata mimi nataka kutembelea nchi yako yenye wenyeji wema. Tafadhali tuongozee njia basi.

Mzee Hekima: Hamna shida.

(Watu hao wanne walianza kupita msitu huo. Tetemeko alikokota gari lililobeba masanduku na mizigo yao. Bahati alifuta jasho la Tetemeko mara kwa mara. Hawakuona wanyama wengine tena. Walikuwa kimya tu mpaka Mzee Hekima aliongeana nao.)

Mzee Hekima: Sijapata majina yako! Ninyi mnatoka wapi? Na mtakwenda wapi?

Tetemeko: Jina langu ni Tetemeko. Huyu ni mke wangu Bahati. Niliposafiri nchi yake, nilimpenda tangu nianze kusikia sifa zake. Na mara nilimwona, niliamua kumwoa. Bahati ndiye anayekuwa taa njema linalomulika moyoni mwangu. Kwa bahati nzuri, alikubali kuchumbiwa nami. Sasa tunataka kurudi nyumbani kwangu baada ya kufunga ndoa. Na huyu ni dada ya Bahati, Sina-Kitu.

Bahati: Oh mume wangu, kweli wewe ni shujaa moyoni mwangu vilevile!

Mzee Hekima: Mapenzi yakoje!

Tetemeko: Mzee, familia zangu walitaka kumwona mke wangu. Basi tutafunga safari mara baada ya kununua farasi. Nilisikia kwamba huko nchi ya Simba waliishi wachawi walioweza kutumia uchawi, ama sivyo?

Mzee Hekima: Lo! Habari hii ni ya ajabu sana! Hata mimi sikupata kujua. Kweli kuna wachawi duniani? Lakini sisi ni watu wa kawaida tu, hatujui uchawi hata kidogo. Basi hii ni fununu tu, labda wachawi waliishi nchi nyingine? Sijui hahaha...

Tetemeko: Labda ni fununu tu.

(Kufumba na kufumbua walipita msitu na kuja katika nchi ya Simba. Wauzaji na wateja wengi wanatembea njiani na kuuza au kununua bidhaa. Maua mengi ya aina mbalimbali yanachanua.)

Bahati: Kweli nchi hii inapendeza sana! Maua mazuri!

Sina-Kitu: (kwa sauti ndogo) Inaonekana niliwahi kwenda hapa.

Bahati: Sina-Kitu, unasema nini?

(Mzee Hekima alipoingia nchini, watu wengi walikuja kusalimiana naye.)

Mwuzaji wa kwanza: Hujambo, mzee? Unarudi sasa hivi?

Mwuzaji wa pili: Habari za mchana, mzee? Ulisafiri wapi? Hukurudi kwa miezi mingi!

Mteja wa kwanza: Eh, kijana huyu maridadi ni nani? Ni wageni wetu? Habari zako?

Mteja wa pili: Wasichana hawa warembo pia ni wageni wetu? Habari za mchana?

Mzee Hekima: Sijambo, asanteni. Hawa ni wageni wangu. Wanataka kununua farasi nchini kwetu ili akokote gari ya kubebea mizigo.

Mwuzaji wa tatu: Nina farasi wengi! Farasi wema wenye nguvu! Bila shaka watakukokotea mizigo yenu na kwenda kwa kasi! (Alisema huku msaidizi wake akivuta farasi mmoja mweupe.)

Mteja wa tatu: Niliwahi kununua farasi wake pia. Kweli farasi wake anakwenda kasi kuliko farasi wengine.

Bahati: Mume wangu Tetemeko, farasi huyu anafanana na farasi wetu wa zamani! Tumnunue huyu basi!

Tetemeko: Sawa. Gharama yake ni kiasi gani?

Mwuzaji wa tatu: Huyu farasi ni zawadi tunayekupa. Tunakukaribisheni kuzuru nchi yetu!

Tetemeko: Asante sana! Tutafunga safari yetu sasa. Asanteni kwa ukarimu wenu.

Mzee Hekima: Usifunge safari harakaharaka, kijana. Usiku unakaribia na itakuwa vigumu kuviona vitu gizani. Ni vigumu kupita msitu! Basi mpumzike hapa leo. Mnaweza kuonja chakula kipekee hapa!

Watu wengine: Ndiyo, kaeni hapa. Chakula chetu ni kitamu sana. Manze safari kesho kutwa.

Bahati: Shujaa wangu Tetemeko, napenda nchi hiyo. Watu wote ni wakarimu tele. Tukae hapa leo, tukae hapa!

Tetemeko: Haya. Tupumzike hapa leo. Kesho kutwa mapema, tutafunga safari mara moja.

Bahati: Nzuri sana, mume wangu!

Mzee Hekima: Twende maskani yangu! Kwa herini nyote!

Watu wengine: Kwa herini!

Tetemeko, Bahari na Sina-Kitu: Kwa herini!

(Mzee Hekima aliwaongoza njia ya kwenda nyumba yake. Walipita kidimbwi kikubwa chenye maji maangavu na sarafu nyingi. Watoto wengi walicheza karibu nayo.)

Sina-Kitu: Mzee, hiki kidimbwi ni nini?

Mzee Hekima: (kwa kutabasamu) Kidimbwi hiki kinaitwa Kidimbwi cha Ndoto. Ukiwa na taraja fulani, basi utupe sarafu moja, ukafumbue macho na kujisema taraja yako. Labda kitakusaidia kulitimiza.

Bahati: Kweli? Ni jambo la mwujiza!

Mzee Hekima: Ni mchezo wa watoto tu! Watoto wanapenda kufanya hivyo na kucheza huko. Sisi watu wazima nani anaamini?

(Sina-Kitu alikuwa amenyamaza tena na aliona kidimbwi kwa muda mrefu. Mzee Hekima aliwaongoza mpaka maskani yake. Kuna vyumba vitatu vya kulala. Bahati na mumewe walikaa chumba kimoja. Na Sina-Kitu alikaa kingine. Baada ya kula chakula kitamu, walikwenda kupumzika kwani walikuwa wamesafiri kwa muda mrefu. Vyumba vyote vilikuwa kimya kwenye usiku wa manane. Wakati huo huo ilionekana wimbo wa ajabu uliimbiwa kwa sauti ndogo, lakini watu waliolala fofofo hawakuweza kusikia isipokuwa Sina-Kitu.)

Wimbo: 

Nchi ya Simba

Nchi yetu ya ajabu

Ukitaka basi uruka

Majani ya ukindu

Hadi mawinguni kukuta

Ukitaka basi uwe shujaa

Uchawi ukubwa

kuwashinda wabaya

iko siku

utarudi nchi yetu

iko siku

hutaitwa Sina-Kitu

Sina-Kitu: Lo! Niliwahi kusikia wimbo huo. Lakini niliusikia wapi? Ni ajabu sana!

(Sina-Kitu alikwenda nje, akafuatana na wimbo na kutaka kutafuta asili yake. Kisha alikuja kwa Kidimbwi cha Ndoto. Mzee Hekima aliimba wimbo mbele ya kidimbwi huku akiona Sina-Kitu kwa kutabasamu.)

Sina-Kitu: Mzee? Kwa nini uko hapa na kuimba wimbo usiku wa manane?

Mzee Hekima: Nakungojea.

Sina-Kitu: Mimi? Kwa nini? Unaningojea?

Mzee Hekima: Nakungojea, mtoto wangu, binti yangu.

Sina-Kitu: Binti? Unasema nini? Sielewi.

Mzee Hekima: Si unakumbuka wimbo huo?

Sina-Kitu: Ndiyo, niliwahi kuusikia, labda nilipokuwa mdogo...au kwenye ndoto. Siwezi kukumbuka vizuri.

Mzee Hekima: Kwa sababu nilikuimbia wakati ulipokuwa mdogo, mtoto wangu.

Sina-Kitu: Ehh? Lakini...sielewi...

(Mzee Hekima aligusa maji ya kidimbwi kwa mkono wake. Halafu aliweka mkono wake juu ya kichwa cha Sina-Kitu na kusema maneno.)

Mzee Hekima: Mababu zetu, mtoto wenu amerejea nyumbani. Tafadhali mpe uchawi, mpe uwezo wa kuwashinda wote wabaya! (Baada ya sekunde chache, aliangasa mkono wake chini.)

Sina-Kitu: Mzee, hivi sasa unafanya nini? Uchawi ni nini?

Mzee Hekima: Sasa unajisikia vipi?

Sina-Kitu: Najisikia...kama mkondo wa joto unafuatana na damu yangu.

Mzee Hekima: Ni kweli. Kwa sababu uchawi unaanza kuota mwilini mwako.

Sina-Kitu: Uchawi? Sielewi. Mzee, tafadhali nieleze.

Mzee Hekima: Usiwe na wasiwasi, Sina-Kitu. Nitakuambia kila kitu. Hii ni hadithi ndefu. Hapa uko nchi ya Simba, nchi ya uchawi. Wananchi wa nchi hiyo wanaweza kutumia uchawi. Lakini uchawi unarithiwa na wanaume tu. Hapo zamani, nchi hii ilitawaliwa na Mfalme mmoja. Alikuwa na wana saba na binti mmoja mdogo. Alimpenda binti yake sana hata kuzidi wana wote. Kwa kuwastaajabisha watu wote, Mfalme alimrithisha binti yake uchawi badala ya wana wake. Wana wake saba walikasirika sana na kuwachukia Mfalme na dada yao. Baada ya kuwaza na kuwazua na kuchungulia vitabu vingi, walipata njia walivyoweza kupata uchawi. Walikuwa wakimwua dada yao, wakamfunga kwa majani ya ukindu, kumchoma na kumla, basi walikuwa wanaweza kupata uchawi wake. Walifanya vivyo hivyo! Lo, balaa hilo! Kweli walipata uchawi lakini kila mmoja wao alikuwa mnyama wa kutisha mwenye miguu mitano, manyoya mwili wote, makucha marefu na mkia mrefu. Zaidi ya hayo, waliendelea maisha yao kwa njia ya kuwala wasichana. Lo, balaa kweli!

Sina-Kitu: Halafu je? Wako wapi?

Mzee Hekima: Halafu Malkia wa nchi hiyo aliona huzuni kubwa. Ingawa aliwapenda watoto wake, lakini alikuwa malkia mwema. Hakutaka wasichana wadhuriwe nao. Kwa hiyo alimwomba kaka yake kuwashinda wanyama hawa wabaya na kuwaua. Kaka yake akakubali na kupigana nao pamoja na Mfalme. Lakini wanyama walikuwa wakali sana na walimwua Mfalme! Kaka ya Malkia aliumizwa pia. Kwa ajiri ya kujilinda asitafutwe na wanyama hao, alibadilisha sura yake. Kwa bahati nzuri, aliona kwamba binti yake alikuwa na uchawi ukubwa na labda alikuwa awe na uwezo wa kuwaangamiza wanyama hao. Kwa ajiri ya kumlinda binti yake asipatwe na wanyama alipokuwa mdogo, alimtuma binti yake kwenda nchi ya mbali sana na kuwaaminisha bwana mmoja kwamba mtoto huyu alikuwa mpwa wa mkewe. Kwa hiyo, mtoto huyu alipata jina lake Sina-Kitu kwa kuwa hakuwa na kitu chochote wakati ule. Mtoto wangu, binti yangu, mimi ndiye kaka ya Malkia, na wewe ndiye binti yangu!

Sina-Kitu: Baba? Baba! Siwezi kuamini masikio yangu! Wewe ni baba yangu! (Mzee Hekima na Sina-Kitu walikumbatiana.)

Mzee Hekima: Ndiyo, binti yangu.

Sina-Kitu: Baba, lakini wanyama wote uko wapi sasa?

Mzee Hekima: Binti yangu, shemeji yako Tetemeko ndiye mmoja ya wanyama wale! Usidanganywe na sura yake sasa! Ndio maana nilikuongozeni hapa nchini kwetu na kutafuta nafasi ya kuwaokoeni!

Sina-Kitu: Ehh! Kumbe ni hivyo! Sikujisikia vizuri tangu nilipomwona! Bahati bado alikuwa pamoja naye. Siwezi kumwacha! Lazima nimwokoe mara moja!

Mzee Hekima: Nenda kumwangamiza mnyama huyu, binti yangu. Sasa mimi ni mzee, na uchawi wangu ndogo tu unabaki. Sasa unajaliwa kupata uchawi mkubwa, basi ni jukumu lako kuwaangamiza wanyama hao saba. Lakini ukumbuke kwamba utomvu wa majani ya ukindu unaweza kuwaonyesha sura yake, na bora uwashinde kwa akili yako! Simba huyu ni rafiki yangu. Anaweza kuhisi uhai wa wanyama wabaya na kuwarukia. Atakulinda na kukusaidia kuwashinda wote. Nenda, binti yangu!

(Sina-Kitu alirudi nyumba ya Mzee Hekima pamoja na simba. Lakini alipoongeana na Mzee Hekima, hawakuona kwamba Tetemeko alitokea nyuma ya Sina-Kitu. Tetemeko alitaka kusikia mazungumzo yao lakini hakuweza kwa sababu ya umbali mrefu. Kwa hiyo alirudi kabla Sina-Kitu kurudi. Tetemeko aliporudi, Bahati aliamshwa na kelele.)

Bahati: Mume wangu? Mbona unarudi kutoka nje? Ulikwenda wapi?

Tetemeko: Bahati, mke wangu. Sijui kukuambia nini... Sijui...

Bahati: Nini? Niambie. Ulikwenda wapi? Ilitokea nini?

Tetemeko: Mke wangu mpenzi, unajua ninavyokupenda. Kweli wewe unamulika moyoni mwangu kama taa jema!

Bahati: Ndiyo, najua. Nakupenda vilevile. Ilitokea nini?

Tetemeko: Nakushukuru sana. Mke wangu, hivi sasa nilikwenda nje kwa sababu... kwa sababu Sina-Kitu aliniita.

Bahati: Alikuita? Kwa nini?

Tetemeko: Aliniambia kwamba ananipenda na kutaka kuniolewa. Lakini nilimkataa moja kwa moja na kumwambia ninakupenda Bahati katika maisha yangu yote! Kisha aliondoka kwa kilio. Niliona kwamba alikwenda Kidimbwi cha Ndoto kutoa taraja lake...

Bahati: Namjua! Kweli namjua! Siku zote ninajua ananionea wivu na mume wangu! Tangu nilipokuwa nyumbani, nilijua alikuwa na nia mbaya! Madhumuni yake yalikuwa kuja kuvunja ndoa yetu, kisha anaweza kukuoa kwa furaha. Namjua!

Tetemeko: Mke wangu! Sitamwoa kamwe! Nakupenda tu. Lakini yeye ni binamu yako, kwa hiyo siwezi kumdhuru...

Bahati: Bwana wangu, wewe ndiye mwema sana! Alipokuambia kumwoa, hakukumbuka yeye ni binamu yangu! Basi... tuondoke! Tuondoke sasa! Twende kwa nchi yako! Atabakiwa hapa peke yake. Tuondoke!

Tetemeko: Haya, mke wangu.

(Ilipotimia alfajiri, Bahati na Tetemeko walifunga mizigo na kuweka masanduku na mizigo yote kwenye gari. Hapo Sina-Kitu alirudi.)

Sina-Kitu: Bahati, utakwenda wapi?

Bahati: Tunaanza safari yetu kwenda nchi ya Raha sasa, na wewe peke yako utabaki hapa. Najua wewe unanionea wivu na mume wangu! Ndio maana nikakataa usifuatane nasi, lakini wewe ukang'ang'ania tu. Sasa madhumuni yako yametokea. Nakuambia, mume wangu hatakuoa kamwe! Kata tamaa yako! Hata kidimbwi hakitatimiza tamaa yako!

Sina-Kitu: Hapana...Si kweli...Tetemeko alikuambia nini? Ulimwamini?

Bahati: Nyamaza, Sina-Kitu! Mume wangu hataki kukuoa, kwa hiyo sasa unavunja ndoa yetu? Bila shaka namwamini mume wangu wakati wote! Sitaki kusikia upuuzi wako. Mume wangu, tuondoke, tuondoke sasa!

Sina-Kitu: Lakini Bahati...

Bahati: Nyamaza! Sitakuwa na binadamu kama yeye.

(Bahati na Tetemeko wameshafunga mizigo yote. Walipopandisha farasi wao mpya, Sina-Kitu alitoa majani ya ukindu aliyoyachuma zamani. Aliyabana majani na kuuangusha utomvu majini. Alifanya hivyo kwa uchawi. Kwa hiyo watu wengine hawakuona. Bahati na Tetemeko walikunywa maji na wakafunga safari yao. Hawakusema chochote kwa Sina-Kitu. Pia Sina-Kitu alikuwa amenyamaza. Bahati na Tetemeko waliingia msituni na punde si punde, Tetemeko hakujisikia vizuri. Ghafla alianguka kwenye farasi na kubadilisha sura yake. Alikuwa mnyama kutisha mwenye miguu mitano, manyoya mwili wote, makucha marefu na mkia mrefu. Bahati alipiga kelele na kuanguka pia.)

Bahati: Te..te..meko... wewe si mume wangu! Wewe...wewe...

Tetemeko: Mke wangu mpenzi, mimi ndiye mume wako Tetemeko! Sasa sura yangu ni halisi.

Bahati: Haionekani...lakini...

Tetemeko: Unajua kwa nini nilisafiri mbali sana hadi nchi yako na kukuchumbia? Kwa sababu natafuta binti ya adui wangu! Baada ya kupata binti yake, nitafanya maarifa ya kumla. Nilifikiri wewe ndiye binti yake, lakini nimekosea. Kumbe Sina-Kitu ndiye binti ya adui wangu! Sasa amepata uchawi, kwa hiyo siwezi kumshinda mimi mwenyewe. Si kitu! Nitarudi nchi ya Raha na kuwaita ndugu zangu. Ama wewe, nilitaka kukula pamoja na ndugu zangu baada ya kukunenepesha. Lakini sasa umeona sura yangu na kujua siri yangu. Bora nikule hapa hapa! Hahaha...

Bahati: Siamini...kwa nini...hapana! Sina-Kitu, niokoe! Sina-Kitu, niokoe!

Tetemeko: Nyamaza wewe! Umesahau ulimbakisha Sina-Kitu katika nchi ya Simba? Hawezi kukusikia. Hakuna mtu yeyote atakayekuja kukuokoa! Acha tu!

Bahati: (kwa kilio) Sina-Kitu! Binamu yangu! Niokoe! Sina-Kitu! Tafadhali nisaidie!

(Wakati huo huo Sina-Kitu alitokea pamoja na simba. Simba alimrukia Tetemeko mara moja.)

Sina-Kitu: Nipo hapa. Usiwe na wasiwasi, Bahati. Nitamwangamiza mnyama huyu wa kutisha!

(Simba alipigana na Tetemeko. Sina-Kitu alitumia uchawi kumsaidia Simba na kumwumiza Tetemeko. Muda si muda Tetemeko alititigwa na uchawi wa Sina-Kitu na kugongwa na Simba, kisha alikuwa na vidonda vingi na kutokwa damu. Sina-Kitu aliona nafasi na kuchoma moyo wake kwa uchawi, Tetemeko akafa. Sina-Kitu alikwenda kwa Bahati.)

Sina-Kitu: Bahati, uko sawa? Mzima?

Bahati: Ni...niko sawa. Tete..mnyama huyu ni wa kutisha sana...sijui...... Samahani, Sina-Kitu.

Sina-Kitu: Si kitu, Bahati. Nikurudishe nchi ya Simba kwanza. Naona unatishwa mno na unahitaji kupumzika. Nitakusimulia kila kitu baada upate mapumziko ya kutosha.

Bahati: Asante, Sina-Kitu, asante sana. Lakini, alitaja ndugu zake...

Sina-Kitu: Ni wajibu wangu kuwaangamiza wanyama wote! Wanyama sita wakali wanabaki. Ninapaswa kuwashinda kwa akili yangu. Itanichukua siku kadhaa kufanya mpango utakaofaa kwanza. Turudi sasa basi. (Sina-Kitu na Bahati wanatoka.)

(Mwisho wa Onyesho la Pili)

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi