Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Uchambuzi wa Uhuru na Muungano wa Tanzania


14 July 2021 | By 罗思颖 曹羽晗 宋艺婷 肖宸臻 | SISU

 

 

Muhtasari: Huko Afrika Mashariki, hasa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uhusiano kati ya Tanzania Barana Kisiwa cha Zanzibar umekuwa na utata. Matini haya yanatumia mitazamo tofauti ya watu wa Tanzania Bara na Kisiwa cha Zanzibar kuelekea Siku ya Uhuru wa Tanzania kama msingi, ikielezea historia ya Tanganyika na Zanzibar kabla ya uhuru na muungano. Inazingatia historia na matokeo ya kuzuka kwa Mapinduzi ya Januari huko Zanzibar na jaribio la Nyerere la kujumuisha Afrika Mashariki. Ikilinganishwa na maoni ya wanazuoni wa Kichina, Ulaya, Marekani na Kiafrika juu ya sababu za umoja wa maeneo hayo mawili kuunda jamhuri, nakala hii inachambua uhusiano wa pamoja wa Tanzania na mafanikio na makosa yaliyofanywa chini ya mfumo wa Tanzania ili kutafuta njia inayowezekana kwa ujumuishaji wa Kiafrika.

Maneno Makuu: siasa za Afrika Mashariki, Pan-Africanism, Nyerere

 

1 Utangulizi

Tarehe 9 Desemba ni Siku ya Uhuru wa Tanzania. Ingawa nchi nyingi zinachanganyika siku ya taifa na siku ya uhuru duniani kote, inasemekana kuwa watu wa Tanzania Bara na Wazanzibari wana maoni tofauti kuhusu changanyiko hili. Watu wa Tanzania Bara huona "siku ya uhuru" ni "siku ya taifa", na Wazanzibari hufikiri "siku ya muungano" ni "siku ya taifa". Lakini, katika utafiti wetu wa vyombo vya habari vya Tanzania, tuligundua kuwa hakuna sikukuu moja maalumu ambayo inaitwa siku ya taifa. Watu wanapotaja “siku ya taifa”, hawaimaanishi siku maalumu, ila ujumla wa siku zote maalumu zinazowapumzisha watu. Na katika habari moja ya IPPmedia, ilipotaja sherehe muhimu kama vile Siku ya Uhuru, Siku ya Jamhuri, na Siku ya Muungano, huzisifia "siku ya taifa".(Kyle,1999) Tuna nadhariatete mbili: 1. "Siku ya taifa" si sherehe maalum bali ni sikukuu za taifa za kisheria katika muktadha wa Tanzania. 2. Sikukuu muhimu, kwa mfano Siku ya Uhuru, Siku ya Jamhuri, na Siku ya Muungano zinaweza kuitwa siku za taifa katika muktadha wa duniani kote.  

Zaidi ya hayo, kwa mujibu wa serikali ya Tanzania, Zanzibar pia ilikubali kuwa Siku ya Uhuru wa Tanzania ni tarehe 9 Desemba. Kama tunavyojua, Zanzibar na Tanganyika zilikuwa nchi mbili huru kabla ya muungano. Walipata uhuru katika nyakati tofauti. Basi kwa nini Zanzibar inakubali kwamba Siku ya Uhuru wa Tanganyika ni Siku ya Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Nchi hizi mbili ziliungana vipi? Tulifanya utafiti juu ya historia chini ya swali hili ili kutoa marejeo kwa wasomaji. 

 

2 Mchakato wa Kupata Uhuru wa Zanzibar

Zanzibar iliwahi kutawaliwa na nchi nyingi zamani, na mwishowe ikawa nchi lindwa ya Uingereza mnamo 1890. Ijapokuwa Uingereza ilikuwa na athari kubwa katika siasa na diplomasia ya Zanzibar, kadhalika, ilitia maanani na kuwategemea watawala wa Waarabu kutokana na sababu za kihistoria na mahitaji ya utawala. Mambo mawili waliweza kuonyesha hali hiyo: Kwanza, Sultani wa Zanzibar na uchaguzi wake wa mrithi ulihifadhiwa chini ya maangalizi ya serikali ya Uingereza. Pili, Waingereza walifundisha na kuchagua Waarabu kama maafisa wakuu wa serikali ya kikoloni kwa mpangilio. Katika hali hiyo, hadhi ya kijamii ya Waarabu ikaimarishwa. Kwa hiyo, uhusiano kati ya Waingereza na Waarabu ulitimiza urari mzuri.

Wakati wa miaka ya 50, karne 19, harakati za kujipatia uhuru duniani kote zilizidi kushamiri, na matumaini ya Wazanzibari ya kupata uhuru yaliongezeka siku hadi siku. Uingereza ilipaswa kutekeleza sera ya kidemokrasia, na kuongoza nchi lindwa Zanzibar kupata uhuru. Baadaye, uchaguzi mkuu ulifanyika kwa mara tatu huko Zanzibar, katika Januari 1961, Juni 1961, na Juni 1963. Katika kipindi hiki, vyama vya kisiasa vilivyoibuka Zanzibar vilikuwa vinne:

Wakati wa mwisho wa karne 19 na mwanzo wa karne 20, wamiliki Waarabu wa utumwa na wafanyabiashara wa utumwa walianzisha Arabu Association, nayo ilikuwa ZNP baadaye. Chama hiki kilipanga “kushika mamlaka kutokana na Waingereza kabla ya harakati za kujipatia uhuru katika bara la Afrika” ili kuhakikisha “Waarabu wachache wawe watawala wa kijamii, kisiasa na kiuchumi juu ya Waafrika wengi huko Zanzibar.” 

Waafrika wa Zanzibar walianzisha Jumuiya ya Waafrika (African Association) mwaka 1934 kwa ajili ya kuanzisha serikali ya Waafrika. Na WaShirazii waligawanywa katika kundi mbili katika swala la uhusiano baina ya Waarabu na Waafrika. Jumuiya ya WaShirazii (Shirazii Association) iliyoanzishwa na Unguja Shirazii mwaka 1939 ilikubali msimamo wa Jumuiya ya Waafrika. Jumuiya hizi ziliungana na wajibu wake ulikuwa ni kuwaongoza Wazanzibari kupigana na Wakoloni kwa njia zote, kupigania uhuru, na mwishowe kuanzisha serikali ya Kiafrika. 

Zanzibar and Pemba People’s Party ilianzishwa na Pemba WaShirazii ambao hawakupinga utawala wa Waarabu. Lengo lao ni "kudumisha uhuru wa WaShirazii na kutoathiriwa na kambi zilizoongozwa na Waarabu au Waafrika."

Ndani ya ZNP, viongozi kadha wa WaShirazii walitaka kuasisi jamii ya kidemokrasia yenye makabila mengi yaliyoweza kuishi kwa usawa na amani. Kwa hiyo, WaShirazii hawa waliokuwa na mawazo tofauti walijiondoa ZNP na kuanzisha Umma Party baada ya uchaguzi wa Zanzibar. Umma Party ilikubali msimamo wa ASP baadaye.

Chini ya uthibiti wa wakoloni, Muungano wa ZNP na ZPPP ulishinda katika chaguzi mkuu na kutangaza rasmi kuanzisha “Serikali ya Muungano”. Tarehe 10 Desemba, 1963, Zanzibar ilitangaza uhuru wake na ikawa nchi huru chini ya Jumuiya ya Madola, ila ikamdumisha Sultani. “Serikali ya Muungano” ilianzishwa na ZNP na ZPPP. Tarehe 12 Januari, 1964, ASP na Umma Party walipindua ufalme wa Sultani na Serikali ya Muungano, wakaanzisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Abeid Amani Karume, kiongozi wa ASP, alikuwa rais wa kwanza wa Zanzibar. Kwa nini mapinduzi yalitokea mwezi mmoja tu baada ya Zanzibar kutangaza uhuru? 

 

3 Sababu Tatu Kuu Zilizosababisha Mapinduzi 

3.1 Mzozo wa kikabila wa muda mrefu kati ya kikundi cha Kiafrika na kikundi cha Kiarabu

Kama ilivyotajwa, wakati wa utawala wa ukoloni wa Uingereza, Waarabu ambao walichukua idadi chache walikuwa tabaka la utawala kwa muda mrefu, walakini weusi ambao waliochukua idadi kubwa walikuwa pembeni mwa jamii. Wengine walikuwa wafanyakazi, wengine walikuwa wakulima, na wengine walipata uhuru tu kutoka utumwani. Watu hawa walikuweko tabaka la chini. Zamani sana kumekuwa na mzozo na uhasama kati ya vikundi vya weusi na vikundi vya Waarabu kwa sababu ya ukosefu wa usawa.

 

3.2 Mashindano baina ya vyama vya Zanzibar

Chama cha Afrika-Shirazi kililenga kuanzisha mamlaka kwa nguvu za Waafrika wenyewe, wakati Chama cha Wazalendo cha Zanzibar kinatumai kudumisha tabaka la Waarabu ambalo waliendelea kuwatawala Waafrika. Mzozo ulikuwa ulidumu kati ya pande hizo mbili. Katika uchaguzi mkuu wa Januari 1961, hakukuwa na chama kilichopata zaidi ya nusu ya viti katika Bunge. Katika uchaguzi mkuu wa Juni 1961, Chama cha Wazalendo cha Zanzibar (ZNP) na Chama cha Watu wa Zanzibar na Pemba (ZPPP) viliunga mkono na kushinda Chama cha Shirazi cha Afrika. Halafu vyama hivi viwili viliunda Serikali Inayowajibika (Responsible Government). Baada ya kuanzishwa kwa Serikali Inayowajibika, vikundi vya watawala wa Kiarabu vilitekeleza sera za ubaguzi. Kwa mfano, maafisa wa serikali lazima waweze kuzungumza Kiarabu. Sera hizi zilizidisha zaidi mizozo kati ya Waarabu na Waafrika. Katika Uchaguzi wa Uhuru wa Julai 1963, ZPPP na ZNP viliungana tena na kupata viti vingi bungeni. Baada ya uchaguzi huu, Chama cha Muungano wa ZPPP na ZNP kilikuwa chama cha kitawala na kikaunda serikali ya Muungano. Baadaye Serikali ilikuwa inakizuia chama cha upinzani (ASP) kushughulikia harakati zake za kisiasa.

Tarehe 10, mwezi wa 12, mwaka 1962, Zanzibar ilitangaza kupata uhuru, lakini serikali ya muungano haikufuatwa na idadi kubwa ya watu wa Afrika ambao walifikiri huu ulikuwa uhuru wa Waarabu.

 

3.3 Mapolisi waliochangia katika mapinduzi

Serikali ya muungano ilishuku kwamba mamia ya mapolisi waliotoka Bara walikuwa wameshirikiana na Chama cha Shirazi cha Afrika na hawakuaminika, kwa hivyo waliwakataza mapolisi hawa. Kitendo hiki cha serikali kilisababisha kupoteza mamia ya mapolisi wenye uzoefu na kiliwakasirisha mapolisi wengi ambao baadaye wakawa nguvu muhimu katika mapinduzi ya Januari.

Asubuhi na mapema ya Januari 12, 1964, mapinduzi yalianza. Karibu wanachama 600 wa Chama cha Shirazi cha Afrika na wanachama 200 wa Chama cha Umma, pamoja na polisi wa bara ambao walikuwa wamepoteza kazi zao. Walianza kushambulia vituo vya polisi, vituo vya redio, na wakala wa serikali.  Kufikia jioni ya siku hiyo, serikali ya muungano wa ZNP na ZPPP ilitangaza kubomoka na Sultan alikimbilia bara.

Kuna makadirio kuhusu idadi ya wahasiriwa katika siku hiyo, kuanzia mia chache hadi 20,000, lakini vurugu dhidi ya Waarabu na Waasia zilidumu kwa wiki kadhaa, na idadi ya waliotoroka baada ya ghasia hiyo haikuhesabika. Mnamo Februari 1964, Kamati ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoundwa na Chama cha Afrika-Shirazi na Chama cha Umma ilitangaza kuwa Zanzibar ilikuwa nchi yenye mfumo wa chama kimoja na Chama cha Umma kiliunganishwa na Chama cha Afrika-Shirazi. Wakati huo huo, serikali mpya pia ilikuwa itataifisha ardhi yote na mashamba na mali isiyohamishika ya Waarabu bila fidia.

Baada ya kuanzishwa kwa Jamuhuri ya Watu wa Zanzibar, viongozi wa ASP na viongozi wa TANU walikutana. Kutokana na hali ya nchini na ng’ambo, viongozi waliamini kuwa ni muhimu kuungana na nchi hizi mbili. Kwa hivyo, mnamo Aprili 26, 1964, Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliasisiwa.

 

3.4 Mchakato wa Kupata Uhuru wa Tanganyika

Mwaka 1951 katika eneo la Meru, maelfu ya wakulima walifukuzwa na idadi ndogo ya walowezi wazungu. Tukio hilo lilisababisha harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika, wazalendo wa Tanganyika walianzisha maandamano makubwa ya kisiasa. Wakati huo TAA (Tanganyika African Association) iliunga mkono na wazalendo hawa(王磊, 2014)

Mwezi Aprili, mwaka 1953 Nyerere alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa TAA. Tarehe 07 Julai, mwaka 1954, kwa sababu TAA haikutosha kukidhi mahitaji ya kupinga ukoloni, ilipangwa upya kuwa TANU(Tanganyika African Nation Union). Nyerere alikuwa mwenyekiti wa chama hiki. Mwaka huu Nyerere alitoa mtazamo kuwa Tanganyika ilihatji kupigania uhuru kwa njia isiyo na vurugu. Alitumai kujenga nchi yenye makabila mengi ambapo Waafrika, Waasia na Wazungu waliaminiana na kushirikiana.(Daniel, 2000)

Mwezi Februali, mwaka 1955 Nyerere aliamini kuwa Tanganyika inaweza kupata uhuru kupitia Umoja wa Mataifa, kwa hivyo aliiwakilisha TANU huko New York kuomba uhuru kutoka kwa Baraza la Wadhamini la Umoja wa Matifa kwa mara ya kwanza. Mwaka 1956, Nyerere alienda tena katika Umoja wa Mataifa kutoa hotuba juu ya ombi la uhuru, akifunua unyanyasaji na ukandamizaji wa kikatili kutoka kwa ukoloni. Ziara hizi mbili za Nyerere katika Umoja wa Mataifa kutetea uhuru wa kisiasa kupitia njia za amani zilimpatia kutambuliwa kimataifa.

Mwaka 1958, kwa sababu ya juhudi za TANU, Baraza la Wadhamini la Umoja wa Matifalilikubali rasmi kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza wa Baraza la Kutunga Sheria nchini Tanganyika. Mwezi Januari, mwaka huu TANU iliitisha mkutano maalum wa kitaifa kuwachagua kabisa wawakilishi wa chama kushiriki katika uchaguzi, ili iweze kushika madaraka kwa njia ya bunge. TANU ilipata ushindi mkubwa katika uchanguzi wa Bunge la Kutunga Sheria, na wagombea waliopendekezwa na TANU wote walichaguliwa kuingia kwenye bunge. Jambo hili likakatisha njama za mamlaka ya kikoloni, ambazo zilitaka kuwazuia Waafrika washiriki kwenye bunge kupitia mageuzi ya katiba.(Daniel, 2000)

Mwanzoni mwa mwaka 1960, kwa msaada wa Umoja wa Mataifa TANU ilianza mazungumzo na Uingereza, na mwishowe ikathibitisha mchakato uliofuata, ambao ni kujenga Serikali Inayowajibika (Responsible Government) kwanza, halafu kujitawla ndani ya nchi (Domestic Autonomy), na mwishowe kupata uhuru kamili. Mwezi Septemba, mwaka 1960 TANU ilishinda viti vingi vya ubunge katika uchaguzi wa Bunge la Kutunga Sheria. Nyerere aliteuliwa kama Waziri Mkuu wa Serikali Inayowajibika (Responsible Government) ya Tanganyika na alianza kuunda baraza la mawaziri. Hii ilikuwa hatua muhimu katika mapambano ya uhuru wa Tanzania.

Tarehe mosi Mei, mwaka 1961 Tanzania ilifanikiwa kupata haki ya kujitawala ndani ya nchi. Nyerere akachaguliwa waziri mkuu wa awamu ya kwanza. Tarehe 22 Novemba, mwaka 1961, Tanganyika ilipitisha Hati ya Uhuru ya Tanganyika (Tanganyika Independence Act). Hii ilieleza wakati rasmi wa uhuru wa Tanganyika.(Daniel, 2000)

Tarehe 9 Desemba, mwaka 1961 Tanganika ilitangaza uhuru, na Nyerere aliendelea kutumikia kama waziri mkuu. Baada ya kujipatia uhuru kutoka Uingereza, Tanganyika ilipitisha katiba ya kwanza yaani Katiba ya Uhuru (Independece Constitution). Katiba hii ilisema kuwa Malkia wa Uingereza Elizabeth II aliendelea kutumikia kama Mkuu wa Nchi wa Tanganika. Gavana Mkuu ambaye alikuwa mwakilishi wa Malkia alikuwa na uwezo wa kutumia nguvu nyingi za Malkia na kuongoza Tangayika.(Kyle, 1997)

Katika Januari 22, mwaka 1962 Nyerere alijiuzulu Uwaziri Mkuu.(Daniel, 2000) Kuna maoni mawili tofauti juu ya sababu ya Nyerere kujiuzulu Uwaziri Mkuu. Katika rekodi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Kitaifa ya TANU kilichofanyika mwaka 1962 iliandikwa kwamba, sababu ya Nyerere kujiuzulu Uaziri Mkuu ni kuwa Nyerere hakuridhika na hali ambayo Elizabeth II alikuwa bado mkuu wa nchi, na aliamua kuushiriki katika uongozi wa TANU tena na kujitahidi kupata uhuru kamili wa taifa.

Walakini, wasomi wengine wa Ulaya na Marekani wanaamini kuwa sababu ya kujiuzulu kwa Nyerere ni mgongano wa mawazo kati ya wanachama wengine wa serikali na Nyerere. Wanachama wengi walipinga sera kadhaa za serikali ya Nyerere, zikiwemo masuala mawili ya uhusiano kati ya Tangayika na Uingereza, na Africanization ya watumishi wa serikali.(Randal,1999)

Mwaka 1962 Tanganyika ilipitisha Katiba ya Jamhuri iliyokomesha Mfumo wa Ufalme. Bunge la Taifa lilipitisha katiba mpya ili kujenga Mfumo wa Urais. Mnamo Desemba 9, 1962, Jamhuri ya Tanganyika iliasisiwa, na Nyerere akachaguliwa rais. Mfumo wa Gavana Mkuu ukakomeshwa. Malkia wa Uiingereza sio tena Mkuu wa Nchi wa Tanganyika. 

Mwanzoni mwa miaka ya 60 karne iliyopita, upepo wa uhuru wa kitaifa ulivuma kila kona ya Bara la Afrika. Nyerere alisema, "Kuanzishwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki ni muhimu sana. Ikiwa ni lazima, Tanganyika iko tayari kuahirisha uhuru wake ili kutangaza uhuru pamoja na Kenya na Uganda na kuunda shirikisho nao mara moja."

Katika mwezi Julai 1963, kiongozi wa Tanganyika, Kenya na Uganda walikutana katika mji wa Nairobi. Walizungumza kuhusu uwezekano wa kuunganisha nchi zote na Zanzibar pamoja ili kuwa na nchi kubwa. Walikubaliana kukamilisha jambo hili kabla ya mwisho wa mwaka 1963, na baada ya mkutano kulikuwa na mipangilio kuhusu kuanzisha shirikisho rasmi. Lakini kwa kweli, mbali na hayo, mazungumzo ya nchi tatu juu ya unganisho hayakupiga hatua yoyote katika miaka iliyofuata. 

Tarehe 10 Julai, 1963 chombo cha kitaifa cha huduma ya vijana kinachoitwa Jeshi la Kujenga Taifa kilianzishwa, ili kuhamasisha vijana kushiriki katika kazi za umma na mafunzo ya kijeshi. Tarehe 12 Januari Mwaka 1964, watu wa Zanzibar walipindua utawala wa Sultani na Jamhuri ya Watu ya Zanzibar iliasisiwa. [1]P26 Siku nane baadaye, mnamo tarehe ishirini, uasi ulitokea katika jeshi la Tanganyika (Tanganyika Rifles). Waasi walidai kutimizwa kwa "Africanization ya Jeshi" na kupandwa kwa mapato, huku wakitayarisha kukabidhi serikali. Kiongozi wa chama cha upinzani aliwasiliana na wanajeshi waasi wakati wa uasi ili kupindua serikali ya Nyerere na kuanzisha utawala mpya. Uasi huu pia uliziathiri Uganda na Kenya, na kuvuruga hali ya kisiasa katika Afrika Mashariki. Walakini, muda mfupi baadaye, kwa ombi la Nyerere, Waingereza waliwatuma wanajeshi wa Uingereza kuingilia tukio hilo, halafu uasi huu uligandamizwa kwa haraka.

Kulingana na maoni ya bodi ya wahariri ya "Historia Kubwa ya Matukio ya Kitaifa", waasi hawa walikuwa watu wasio na elimu kabisa, pia wasio na lengo waziwazi la kisiasa. Aidha uasi huu haukupata ufahamu na msaada kutoka wananchi, ambayo walidhani ni sababu ya kuu ya kutofaulu kwa uasi huo.Katika Aprili 26, mwaka 1964, Tanganyika na Zanzibar ziliunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. 

Baada ya kuanzishwa kwa nchi mpya, Katiba ya Muda ya Muungano ilianzishwa. Sifa inayojulikana zaidi ya Katiba hii ni muundo wa serikali mbili, pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Serikali ya Zanzibar ina bunge na rais wake, na rais wa Zanzibar pia anafanya kazi kama makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano.

 

4 Maoni ya Sababu za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Njia mbili tofauti za Tanganyika na Zanzibar kupigania uhuru zinatofautiana sana. Walakini, nchi hizo mbili ziliungana mnamo Aprili 26, 1964, na kubadilisha jina la nchi yao kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" Mnamo tarehe 29 Oktoba, mwaka huu". Julius Nyerere alichaguliwa Rais Mwanzilishi. Hivi kwa nini Tanganyika na Zanzibar ziliungana? Wasomi kutoka Ulaya, Afrika na China wana maoni tofauti juu ya sababu za muungano wa Tanganyika na Zanzibar. 

Amrit Wilson ambaye ni msomi wa Kizungu alidhani kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa zao la Vita Baridi. Uingereza na Marekani zilitaka kushinda msaada wa Zanzibar katika kambi yao ya kibepari kwa sababu huko Zanzibar wananchi wengi walitegemeza Socialism. 

Msomi wa Kiafrika Godfrey Mwakikagile aliamini kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni matokeo ya Pan-Africanism. Umoja wa watu wa Kiafrika ungesaidia kupinga ukandamizaji wa wakoloni. Kwa hivyo, anaamini kwamba muungano huo haukusababishwa na Uingereza na Marekani, lakini ilikuwa matokeo ya hiari ya Waafrika. (William, 1973)

Walakini, Wang Lei, wasomi wa China anadhani kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sio matokeo ya Pan-Africanism tu. Licha ya athari ya Pan-Africanism, muungano huu ilikuwa hitaji la maslahi ya pande zote mbili. 

Kabla na baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, Karum alikabiliwa na mashinikizo makubwa kutoka kwa makabiliano kati ya Kambi za Ubepari na Socialism, yakiwemo mashambulizi kutoka jeshi la bahari ya kizungu, na ukandamizwaji wa kiuchumi. Pia Karum alikabiliwa na mapambano ya vyama ndani ya nchi. Wakati huo serikali ya Karum ilikuwa bado haijajenga jeshi lake lenyewe, kwa hiyo ilipaswa kuomba Tanganyika kuitolea msaada, ambayo iko karibu zaidi na Zanzibar kijiografia. Rais Karum alitaka kutuliza shinikizo la nje na upinzani wa ndani kupitia muungano na Tanzania. 

Kwa kuzingatia hali ngumu ya Zanzibar, Nyerere alikuwa na wasiwasi kuwa Zanzibar ingekuwa mahali pa mabishano kati ya kambi za ubepari na socialism. Isitoshe, kwa sababu Tanganyika na Zanzibar zilikuwepo karibu sana, Nyerere alikuwa na wasiwasi zaidi kwamba majeshi ya kigeni yatavamia kisiwa cha Zanzibar na kutisha salama ya Tanganyika. Kwa hiyo Nyerere alitumai kuungana na Zanzibar mara baada ya serkali mpya ya Karum ilipozaliwa ili wajikinge na hatari ya nje pamoja katika Vita Baridi. 

 

5 Hitimisho

Ili kuhitimisha, makala hii ilichagua Siku ya Uhuru wa Tanzania, na ikaelezea kwa ufupi historia ya Tanganyika na Zanzibar kabla ya uhuru na umoja. Inaeleza juu ya vyama vikuu vya kisiasa vilivyoibuka Zanzibar katika karne ya ishirini, Mapinduzi ya Januari ya Zanzibar, jaribio la Nyerere la kujumuisha Afrika Mashariki, uasi uliolipuka katika jeshi la Tanganyika, na muungano wa Tanganyika na Zanzibar. 

 

 

Marejezo

Kyle, K.(1997). The Politics of the Independence of Kenya Contemporary British History, 11(4),     42-65

Ltd, T. (2021). Mwalimu Nyerere’s resignation as Prime Minister, January, 1962. Retrieved 22 June 2021, from https://www.dailynews.co.tz/news/2019-01-315c529e59d2d0b.aspx

Daniel, T.(2000). Compatible cultural democracy: the key to development in AfricaUniversity of Toronto Press12(7), 167.

Randal, S.(1999). Tanzanian Journey to Republic The Radcliffe Press, 7(1), 252.

Tovuti Kuu ya Serikali: Sherehe za Maadhimisho ya Uhuru. (2021). Retrieved 22 June 2021, from        https://www.tanzania.go.tz/home/pages/233

William, E.(1973). Nyerere of Tanzania. London: Victor Gollanz, 4(1), 24.

王磊(2014). 尼雷尔与坦桑尼亚国家建构研究.上海:华东师范大学博士论文, 24-26, 30-33.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi