Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Muziki Wa Bongo Fleva: Kizazi Kipya Chajieleza Kwa Utamaduni


30 October 2020 | By 宋艺婷 Monika | SISU

  • Bongo Fleva

  • Bongo Fleva

  • Bongo Fleva

  • Bongo Fleva

  • Bongo Fleva

Mwandishi: SONG Yiting           Wahariri:  MA Jun  NING Yi

Muziki wa Bongo Fleva (au Bongo Flava) unachukuliwa kama “Hip-Hop katika Bara la Afrika Mashariki”, nao umeshamiri huko Tanzania tangu miaka ya themanini karne iliyopita. Neno “Bongo” linatokana na neno “Ubongo”, ambalo linamaanisha akili, na “Fleva” inatokana na matamshi ya neno lingine la Kiingereza “Flavour”. Kwa hiyo, fasili ya “Bongo Fleva” ni viburudisho vitokanavyo na matumizi ya akili. Zaidi ya hayo, Bongo inaashiria jiji la Dar es Salaam au Tanzania katika miktadha maalumu. Watu hukabiriwa na matatizo mengi wakati wanapoishi katika jiji kubwa. Kufuatana na hali zao ngumu, vijana wanapaswa kujifunza jinsi wanavyotumia busara na maarifa ya mtaani ili waendelee na maisha yao. Kwa hiyo, fasili ya pili ya Bongo Fleva ni kuwa ukitaka kuishi katika jiji la Tanzania, ni lazima uwe na busara hata ujanja .[1] Kwa mujibu wa ufafanuzi huo, kizazi kipya kinaanza kujieleza kwa utamaduni maisha yao ya halisi huko Tanzania kwa njia ya muziki wa Bongo Fleva.

Wakati wa miaka ya themanini karne iliyopita, kufuatana na mageuzi ya kisiasa ya Tanzania na maendeleo ya mfumo wa soko huria, Sanaa za Kimarekani kama vile muziki wa Hip-Hop, graffiti mitaani na sanaa nyinginezo ziliingizwa Tanzania, nazo zilikaribishwa na kupendwa na hadhira, hasa vijana, kwa njia mpya ya vyombo vya habari. Mwanzoni, waimbaji wa Tanzania waliigiza muziki wa Hip-Hop na kutunga nyimbo, wengi wao walikuwa vijana wa tabaka la katikati ambao waliweza kugusa tamaduni za kigeni kwa rahisi.[2] Baadaye, muziki wa Hip-Hop ulishamiri hadi kufikia vijana wote kwa sababu ya mapendekezo ya DJ na MC wa redio na kuongozeka kwa mahali pa kuburudishia. Pamoja na maendeleo hayo, wanamuziki wengi wapya waligundua uwezo mkubwa wa utungaji wa Kiswahili. Lakini kwa sababu ya ukosefu wa vifaa vya rekodi na mfumo rasmi wa utungaji wa muziki, Bongo Fleva ilikuza kwa upole hadi mwaka wa 2000.[3] Wakati huo huo, elementi nyingi za muziki wa kienyeji, kama vile taarab, soukous na ngoma, ziliunganishwa na elementi za kigeni, kama reggae, R&B, disco na Zouk, majaribio haya yalipata mafanikio makubwa katika utungaji wa Bongo Fleva. Kisha Bongo Fleva ilikuwa muziki mwenye mtindo wa kipekee wa Tanzania pamoja na michango ya wanamuziki wengi maarufu. Nyimbo za Bongo Fleva ambazo ziliandikwa kwa Kiswahili na pia kuchanganywa na Kiingeraza au lugha zingine za kikabila, zilipendekeza sana huko Afrika Mashariki.

Zaidi ya kuwaburudisha watu, Bongo Fleva inaweza kuwafunza wananchi na kudhihirisha matatizo ya kijamii vilevile. Maudhui ya nyimbo hizi hugusa kila upande wa maisha ya kijamii, kama vile umaskini, kujikinga na UKIMWI, ufisadi, hata maisha ya wanamuziki wenyewe.[4] Kwa mfano, mwanamuziki maarufu Jay Moe alitunga wimbo wake maarufu Ndio Mama kwa ajili ya kutoa heshima kwa hayati mama yake. Thang Solo alionyesha hali tete ya maisha yake katika nyimbo zake. Na Kwetu ni wimbo ambao Rayvanny alimjulisha mpenzi wake hali ngumu ya familia yake na kumwelezea hisia zake halisi.

Aidha, Bongo Fleva inawatolea vijana wa Afrika Mashariki njia ya kusawiri mawazo huria. Maneno yenye sitiari na kejeli yanayotumiwa katika nyimbo hizo huwavutia watu wa kila aina. Kwa mfano, wimbo wa Utanipenda unasimulia jinsi mwanamuziki Diamond Platnumz anavyofikiria ugeugeu katika maisha yanayojawa na uchungu mkubwa wa kihisia, na pia anatoa wasiwasi juu ya maisha ya usoni:

Nimeshindwa Kulipa BiMA Nimeuza Madalee

Radio Nyimbo Wamezima Tv Ndio Hataree

Umeneja Umebaki Jina

Hanitaki Hata Talee

Oooh Wale Mashabiki Walionisifu Kwa Maneno Matamu

Leo Maadui Zangu Ni Mitusi Tu Kwa Instagram

……

Ooh Ninayosema Yana Maana

Sababu Hakuna Anaejua Kesho

Anaepanga Ni Rabana Ila Ameificha Ni Confidential

Ukisali Omba Sana Mumeo Nisije Kuwa Kichekesho

Maana Rafiki Wa Jana Ndio Adui Mkubwa Wa Kesho

Bongo Fleva ni chombo kinachotumiwa na vijana wa Tanzania kutuonyesha hisia zao. Muziki huu wenye upekee huchanganya matumaini, ndoto, taabu na juhudi zao. Wanaonyesha roho na matumaini yao hadharani kwa njia ya muziki unaopendeza. Hisia na tamko lao bila shaka vitawagusa wasikilizaji kwa kina.

 

Marejeleo

[1] Kadallah, R.T., 2017. Muziki wa Bongo Fleva na Changamoto za Kimaadili katika Jamii. Mulika: Toleo Maalumu la Muziki wa Kizazi Kipya, Vol. 29 & 30.

[2]Fergus Ainsworth (2020) Bongo Flava : Tanzania’s home grown Hip Hop. [THE BEST OF AFRICA] 27th March. Available from: https://thebestofafrica.org/content/bongo-flava-tanzanias-home-grown-hip-hop [Accessed 11/10/20].

[3] Mahenge, E., 2011. Chimbuko la Muziki wa Hip hop ni Uasi au Sanaa za Maonesho. Mulika: Toleo Maalumu la Muziki wa Kizazi Kipya, Vol. 29 & 30.

[4] Suriano, M., 2011. Hip-hop and Bongo flavour music in contemporary Tanzania: youths' experiences, agency, aspirations and contradictions. Africa Development, 36, pp. 113-126.

 

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi