Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Uzoefu wa Kumpokea na Kumsindikiza Mgeni


16 November 2019 | By 罗思颖 Bahati | SISU

 

Kila siku tunawapokea na kuwasindikiza wageni wengi maishani mwetu, kwa hivyo ni muhimu kwetu kufahamu vizuri uzoefu juu yao.

Wakti wa likizo iliyopita rafiki yangu kutoka Uingereza alinitembelea. Aliniambia kuwa alikuja hapa kwa ndege, kwa hivyo nilikwenda uwanja wa ndege kumpokea. Mara nilipoonana naye, nilimkaribisha kwa ukarimu na nikamchukulia mizigo yake. Na tukaongeana kuhusu safari yake na hali ya maisha yake siku hizi. Kisha, alikaa kidogo kwenye chumba cha kupumzikia, wakati huo nilikwenda kushughulikia mambo yote forodani.

Kwa vile rafiki yangu hakujua hali ya mahali hapa, ilinilazimu nimpangie mpangilio kwa makini ili asijali mambo yote na awe furaha sana. Nilikuwa nimemwagizia hoteli na baadaye nilimpelekea hapo. Halafu, nilimwambia kuwa akiwa shida yoyote ningemsadia kutatua matatizo.

Siku hizo zifuatazo, tulitembelea vivutio vingi maarufu hapa na kuonja chakula kitamu hapa. Sote tulifurahia kuwa na kumbukumbu ya kipekee pamoja.

Lakini siku ya kuagana ilifika. Kabla ya yeye kuondoka, nilikuwa nimemwagizia tikiti ya ndege na nilikwenda kwake kufunga mizigo. Baada ya vitu vyote kutayarishwa, tulikwenda uwanja wa ndege. Tulipofika hapo, tuliona huzuni sana. Lakini nilimtakia safari njema na niliwasalimia jamaa zake. Mwishowe, nilimwambia kuwa tutazidi kuwasiliana kwa kupigiana simu na kuzungumzana katika mtandao. Pia nilisema kuwa nilitarajia ataweza kuja tena atakapopata nafasi siku za baadaye.

Kujifunza kumpokea mgeni na kumsindikiza mgeni ni somo muhimu katika jamii yetu. Tukifahamu uzoefu huo, tutaweza kushughulikia vyema mambo kati ya watu, na tutajenga uhusiano imara zaidi na watu wengine.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi