Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Kumpokea na Kumsindikiza Mgeni


16 November 2019 | By 褚予钦 Jamila | SISU

Wakati wa likizo iliyopita, mwanafunzi mwenzangu wa sekondari alikuja Shanghai kutoka Hongkong kutembelea. Alinjulisha habari za ndege yake ili niweze kumpokea pamoja na marafiki zetu wawili. Siku yake ya kufika ilifika, lakini ndege yake ilifika uwanja wa ndege wa Hongqiao mapema sana. Maana wakati aliposhuka ndege bado hatujashuka treni ya ardhi ya namba kumi. Ilimbidi asubiri kwa nusu saa hadi tulifika uwanjani kumpokea. Tulifurahi sana kwa kuonana na tulizungumza kidogo huko uwanjani. Baadaye tulimsaidia kuchukua mifuko yake na tukakwenda hoteli yake pamoja.

(Baada ya wiki moja)

Siku yake ya kuondoka Shanghai ilifika baada ya wiki moja. Mimi mwenyewe nilimsindikiza kwa sababu marafiki zetu wengine hawalikuwa na nafasi. Aliagiza tikiti ya ndege ya saa moja jioni kurudi Hongkong. Mchana nilikwenda maduka pamoja naye kuinunulia familia yake zawadi. Kwa ajili ya kuwahi ndege, tulirudi hoteli yake saa kumi alasir kufunga mizigo. Kisha tuliondoka hotelini na tukakwenda katika uwanja wa ndege wa Pudong kwa treni ya ardhi ya namba mbili. Nikamsaidia kushughulika mambo ya kuchukua tikiti na kucheki mizigo. Tulisikitika sana kwa kuagana. Alisema kwamba atakuja Shanghai tena baadaye, na aliniomba niende Hongkong kumtembelea nikipata nafasi. Nilimjibu kuwa bila shaka nitakwenda. Zaidi ya hayo, nilimwambia kuniandikia ujumbe mara afike Hongkong na kunisalimia jamaa zake. Mwishowe tuliagana katika forodha.

 

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi