Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China
Soma Zaidi
Muhtasari wa Hadithi Jamila na Pete ya Ajabu
16 November 2019 | By 宋艺婷 Monika | SISU
Siku moja, baba Jamila aliporudi alikuwa amelewa. Baada ya maneno kadhaa, ghafla alianza kumpiga Jamila. Mama Jamila alitaka kumtunza Jamila na kupigana na Baba Jamila. Baba alikasirika sana na kuchukua shingo ya Mama Jamila. Wakati huo huo Mama Jamila hakuweza kutanafusi na alimwua Baba Jamila kwa kisu chake. Jamila aliogopa sana na kulia. Mama yake alimwambia kukimbia haraka haraka, kisha aliaga dunia pia.
Jamila aliona huzuni sana, lakini ilimbidi kuchuma pesa mwenyewe. Kwanza alikuja kwa bawabu moja wa nyumba kubwa na kuomba kazi. Bawabu akamchekelea na hakumpa kazi kwa sababu Jamila alikuwa na umri wa miaka kumi na moja tu.
Halafu alipoona mkahawa njiani, akakwenda kuomba kazi tena. Mwenyeji wa mkahawa alishangaa kuona mtoto mdogo aliyeomba kazi. Alimpa chakula lakini kukataa ombi lake. Baada ya kula chakula, aliendelea kuishi mtaani.
Kwa bahati nzuri, Jamila alipoishi njiani, alipata mikate iliyobaki. Lakini wavulana wakamkimbiza yeye kwa kusudi la kunyang’anya mikate yake. Jamila akakimbia na kujificha ndani ya gari moja. Dereva wa gari alistaajabu kuona Jamila na kumwuliza alifanya nini na wazazi wake walikuweko wapi. Baada ya kusikiliza hali ya Jamila, alisikitika sana na kumletea nyumbani.
Nyumba ya bwana huyu ilikuwa kubwa sana. Na alimjulishia Jamila jamaa zako. Lakini bawabu ya nyumba alifiriki Jamila alikuwa mchafu. Watoto wawili wa kike wa bwana wakamdharau. Na mke wa bawabu alimchuki kwa sababu bwana huyu akaamua kumlea Jamila. Bwana na mkewe waliongeana kwa muda mrefu. Bwana alisema kuwa alifurahi kumsaidia mtoto huyu. Baadaye, mkewe alikubali kumlea Jamila, lakini alimwatibu Jamila sana wakati ambapo bwana hakuwepo. Hata Jamila aliota kuwa nusura atote kwa sababu mkewe alitaka kumwua. Baada ya mwezi mmoja, bwana alihitaji kusafiri. Na hivyo watu wa nyumba hii wakamchokoza Jamila zaidi. Watoto wawili wa bwana walipiga picha katika kitabu cha Jamila na kumchekelea. Mke wa bwana akamfulisha nguo nyingi na hata kumpiga. Jamila alilia mara kwa mara. Mtumishi wa nyumba akamwonea huruma na kugombana na mke wa bwana, lakini akaondoshwa.
Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China