Loading...

Soma Zaidi

Sanaa mpya | Harakati ya Utamaduni wa Kijadi ya Awamu ya Pili katika SISU Yakuja


Wakati: 13:00-15:00, tarehe 19 Aprili, mwaka 2024

Mahali: Mteremko wa Wapenzi, Kampasi ya Songjiang

Waandaji: Kituo cha Elimu ya Sanaa cha SISU, Idara ya Usimamizi wa Kundi la Sanaa

 

“Huku ngurumo ya majira ya chipukizi ikipiga, vitu vyote vinakua.”

Mkusanyiko wa wanachuoni katika majira ya chipukizi unalenga kuvumbua kwa kina roho ya kibinadamu, maadili na haiba ya sanaa katika utamaduni wa kijadi wa kichina. Ikizingatia sifa za umaridadi, kimila, usasa na ushirikiano, harakati hii inaonyesha uzuri wa taifa na kuwaambia vijana wawe na roho ya uwazi.

Siku hizi tunatafuta mila za kichina, kama vile mashairi, kaligrafia, mchoro, ambazo ni mababu wetu walivyofanya kila siku. Tutawapa wanafunzi na walimu wanaopenda maisha mwaliko wa kuanza safari ya kisanaa katika majira ya chipukizi, ili kujenga masoko ya kisanaa ya majira ya chipukizi katika Mteremko wa Wapenzi kwa pamoja. Kupitia namna mbalimbali za kisanaa, tunatumai kwamba wanafunzi na walimu wanaweza kuwa na safari ya “elimu”, “michezo”, “uzuri”, ili wawe na mkusanyiko wenye sifa za kijadi na kisasa.

Kuna sehemu tatu katika harakati hii. Sehemu ya kwanza ni soko la mafunzo la “elimu”, ambalo wanafunzi na walimu watapata uzoefu wa mchoro na kaligrafia. Sehemu ya pili ni soko la “michezo”, ambalo litawapa furaha kwa kupitia michezo ya kuonja chai na pombe, ya kutupa mishale katika mtungi na kutengeneza mifuko yenye harufu nzuri. Sehemu ya tatu ni maonyesho ya “uzuri” yatakayoonyeshwa na kundi la sanaa, yakiwemo muziki wa ala za kijadi za kitaifa, ukariri wa mashairi ya lugha mbili na kadhalika.

Gawanya:
Loading...

Soma Zaidi