Loading...

Soma Zaidi

Masomo ya Kibinadamu ya Kidijitali: Kutumia Dhana, Nadharia na Maarifa katika Utafiti wa Isimu


Wakati: 16:30-18:00, tarehe 26, Machi (Jumanne), Mwaka 2024

Mahali: Darasa la 7210 (Jengo la Saba), Kampasi ya Songjiang

Msemaji: Ou Yang Jian

Waandaji: Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika, Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU)

 

Utangulizi:

Miaka hivi karibuni, pamoja na maendeleo ya teknolojia ya masomo ya kibinadamu ya kidijitali, ujenzi wa mfumo wa mijadala wa isimu unaonyesha mwelekeo mpya. Kwa upande mmoja, “upya” wake unatokana na utafiti na ufahamu wa kina kuhusu maarifa na maendeleo ya uwanja wa sayansi ya kijamii na ya kibinadamu nchini China sasa. Kwa upande mwingine, “upya” wake unatokana na mabadiliko na uvumbuzi wa kozi ya isimu ya kijadi, ambayo itakuwa uwanja mpya wa taaluma kwa kupitia ujumuishaji wa makozi na aina mbalimbali.

Masomo ya kibinadamu ya kidijitali yanaweza kutoa fursa mpya kwa ujenzi wa mfumo wa mijadala wa isimu nchini kwetu. Kwa njia ya mtazamo wa masomo ya kibinadamu, ujenzi huu unaweza kufichua tofauti na ufanani katika utafiti wa lugha kati ya jamii na tamaduni tofauti, ili kuchunguza vipimo vingi vya utafiti wa lugha kwa kina na kwa undani.

Kuanzia mtazamo wa makozi mbalimbali, mhadhara huu utajulisha maendeleo ya masomo ya kibinadamu ya kidijitali, uundaji na mabadiliko ya dhana na kadhalika.  Kwa kutumia mifano, pia utaonyesha mawazo na dhana ya utafiti wa kibinadamu ya kidigitali, huku ukibainisha matumizi ya masomo ya kibinadamu ya kidigitali katika utafiti wa isimu.

Gawanya:
Loading...

Soma Zaidi