Soma Zaidi
Isimu ni nini?
Msemaji: Zheng Xinmin
Wakati: 13:00-14:30, tarehe 2 (Ijumaa), Desemba, Mwaka 2022
Mahali: Ukumbi wa Mashariki, Maktaba, Kampasi ya Songjiang
Lugha: Kichina
Muhtasari wa Yaliyomo:
Msingi wa isimu yenyewe ni lugha, na isimu inazunguka sifa za kindani za lugha ili kufanya utafiti, zikiwemo: 1) utaratibu wa kutoa na kupokea sauti; 2) ujenzi wa maneno na sentensi; 3) maana za maneno na sentensi; 4) maana za muktadha, na jinsi ya kutumia lugha kuonyesha mwenendo na kadhalika. Mambo yaliyotajwa hapo ni msingi wa masomo kwa wanafunzi wote wanaojifunza isimu, na pia yanaweka msingi imara kwa wanafunzi ikiwa wanataka kusoma zaidi au kufanya utafiti katika sekta fulani ya isimu.
Utangulizi wa Msemaji:
Zheng Xinmin alipata PhD yake ya Isimu ya Matumizi ya Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Hong Kong. Sasa yeye ni profesa na mwalimu wa madaktari wa Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU). Zheng hufanya utafiti katika elimu ya lugha za kigeni, ufahamu wa walimu wanaofundisha lugha za kigeni na ufundishaji kwa lugha nyingi na kadhalika.