Loading...

Soma Zaidi

Nasaba ya Kushan katika Barabara ya Hariri


 

Msemaji: Wang Yue

Wakati: 19:00-20:30, tarehe 17 (Jumapili), Aprili, Mwaka 2022

Mahali: Tencent Meeting (ID: 601-6788-2381)

Mwandaaji: Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika

Lugha: Kichina

 

 

Utangulizi:

Kwa mawasiliano ya utamaduni baina ya Mashariki na Magharibi, Nasaba ya Kushan ilikuwa na hadhi maalumu ya kihistoria wakati wa kuanzia karne moja hadi karne nne. Wakati wa ustawi wa Nasaba ya Kushan, ilitawala maeneo mengi ya Asia ya Kati na Asia ya Kusini. Katika upande wa mashariki, ilitazamana na Bahari ya Aral; kusini ilipakana na Mlima Wendeya; mashariki ilipakana na Uwanda wa Juu wa Pamir; magharibi ilipakana na Uwanda wa Juu wa Irani. Maeneo yake ilikuwa muhimu kwa mawasiliano baina ya kusini na kaskazini, mashariki na magharibi katika bara la Asia na Ulaya. Utamaduni wa Irani wa Asia ya Magharibi, sanaa ya enzi ya Ugiriki iliyoathiriwa na Alexander huko Asia ya Kati, na utamaduni wa Asia ya Kusini, ziliingiliana na eneo la Hezhong la Zamani kupitia mazingira ya mawasiliano yaliyoanzishwa na kuhakikishwa na Nasaba ya Kushan, jambo ambalo liliboresha kwa kiwango kikubwa sura ya kitamaduni ya eneo la Hezhong. Sifa hizi tofauti za kitamaduni pia ziliathiri na kuathiriwa na utamaduni wa China kupitia Barabara ya Hariri. Hotuba hii itatoa uchambuzi na maoni husika juu ya kipengele hiki cha kihistoria kutoka kwa mtazamo wa masalio ya kihistoria.

Gawanya:
Loading...

Soma Zaidi