Loading...

Soma Zaidi

Je, Sayari ya Furaha iko Wapi? — Kuchunguza Falsafa ya Ucheshi ya Afrika Mashariki kutoka kwa Talk Shows


Msemaji: Ning Yi, Mwalimu wa Idara ya Kiswahili, katika Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika, Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).

Wakati: 19:00-20:30, tarehe 23 (Jumamosi), Aprili, Mwaka 2022

Mahali: Tencent Meeting (ID: 985-6087-8548)

Chapa: Hadithi za Usiku katika Kitivo cha Utafiti wa Asia na Afrika

Lugha: Kichina

 

Utangulizi

Afrika, bara la kichawi, ingawa uchumi wake haujaendelea sana, taswira ya watu wenye matumaini ya kuimba na kucheza imekita mizizi ndani ya mioyo ya watu. Katika jamii za makabila mengi na lugha nyingi barani Afrika, wazungumzaji hutumia lugha ili kusisitiza hisia ya uraia. Lugha kama kiambishi cha utambulisho hugawanya wazungumzaji katika vikundi maalum na kuhamasisha mitazamo tofauti ambayo huenda zaidi ya lugha yenyewe. Hotuba hii itaangazia ucheshi wa kitaifa wa Kenya, na kuchanganua sifa za lugha zenye kipuuzi, kinzani na miundo wa wacheshi wa Kenya, pamoja na majukumu yao katika kuweka alama za utambulisho, ujenzi wa mipaka, na kuunda utendakazi. Wawezaje kuhamasisha ucheshi bila kukasirisha? Wawezaje kupata hisia ya mpaka katika uhusiano wa maridadi wa makabila tofauti? Hebu tufuate nyayo za wacheshi wa Kenya na kugundua falsafa ya ucheshi ya kipekee kwa Afrika Mashariki.

Gawanya:
Loading...

Soma Zaidi