Loading...

Soma Zaidi

Kongamano la Awamu ya Tisa la Taaluma za Barabara ya Hariri na Semina ya Kitaaluma ya “China na Ulimwengu zinazounganishwa na Barabara ya Hariri”


Wakati:  tarehe 11 Septemba, mwaka 2021

Mwaka 2021 ni maadhimisho ya miaka minane ya ujenzi wa pendekezo la "Ukanda Moja, Njia Moja (One Belt One Road Initiative)", China kama nchi kubwa itaendelea kutekeleza jukumu lake. Katika mchakato wa kihistoria wa pendekezo la "Ukanda Moja, Njia Moja", ambayo limekita mizizi na limekuwa kuendelea kila siku, China imeshiriki kikamilifu katika mageuzi na ujenzi wa mfumo wa utawala wa ulimwengu, na imeendelea kuchangia hekima na nguvu za China.

Kuimarika kwa ujenzi wa pendekezo la "Ukanda Moja, Njia Moja" hakujafungua tu nafasi mpya ya masomo kwa maendeleo ya Taaluma za Barabara ya Hariri ulimwenguni, bali pia kumeleta fursa mpya za kihistoria za kufufua Taaluma za Barabara ya Hariri nchini China, na imeendelea kuchochea shauku ya kitaaluma ya wasomi wa Taaluma za Barabara ya Hariri ndani na nje ya nchi.

Jinsi ya kufasiri tena "uhusiano wa Barabara ya Hariri kati ya China na ulimwengu katika nyakati za zamani na za kisasa" sio tu suala la kitaaluma, bali pia ni suala la vitendo, ambalo linastahili kufanya majadiliano ya kina katika taaluma tofauti.

Ili kukuza ushirikiano na mazungumzo katika nyanja zinazohusika za utafiti na kujenga jukwaa la majadiliano ya kitaaluma, Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU), Jumba la Makumbusho la Bahari la China (China Maritime Museum) zinapanga kuandaa Kongamano la Awamu ya Tisa la Taaluma za Barabara ya Hariri na Semina ya Kitaaluma ya “China na Ulimwengu zinazounganishwa na Barabara ya Hariri” mnamo tarehe 11 Septemba, mwaka 2021 (Jumamosi).

Katika Kongamano hili la Awamu ya Tisa la Taaluma za Barabara ya Hariri la SISU na Semina ya Kitaaluma ya Awamu ya Kumi ya CMM, waandalizi mahsusi ni Idara ya Utafiti wa Mkakati wa Barabara ya Hariri ya SISU(Institute of Silk Road Studies) na Idara ya Utafiti wa Taaluma ya Jumba la Makumbusho la Bahari ya China. Mada za semina hii ni pamoja na: Barabara ya Hariri ya Bahari katika Enzi za Kale, Barabara ya Hariri ya Nchi Kavu ya Kale, Uhusiano wa Barabara ya Hariri ya kisasa kati ya China na Ulimwengu, Nadharia na Mbinu za Utafiti wa Taaluma ya Barabara ya Hariri, Urithi wa Barabara ya Hariri na Utafiti wa Jumba la Makumbusho na kadhalika.

Kwa sababu ya athari za janga la virusi vya Korona, semina ya kitaaluma ya kongamano hili imepangwa kufanyika katika mitandao. Ikiwa kuna mabadiliko yoyote, kutakuwa na tangazo linalohusika katika siku zijazo.

Gawanya:
Loading...

Soma Zaidi