Loading...

Soma Zaidi

Jukwaa lenye Mada Maalumu ya Mkutano wa Akili Bandia wa Duniani Mwaka 2021


  • Mkutano wa Akili Bandia wa Duniani Mwaka 2021

Wakati: tarehe 9, Julai, mwaka 2021

Jukwa Kuu:
Chumba cha 618, Kitovu cha Shanghai EXPO Maonyesho na Mikutano ya Dunia, Nambari 1500 Barabara la Shibo, Wilaya ya Pudong, Shanghai
Saa: 9:00 - 12:20 a.m.

Jukwaa Saidizi:
Nambari 550 Barabara la Dalianxi, Kampasi ya Hongkou, Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai
Saa: 14:00 - 18:30 p.m.

 

Utangulizi wa Jukwaa:
       Baada ya maendeleo ya zaidi ya miaka 60, akili bandia (AI) imekuwa ukweli wa leo kutokana na dhana ambayo ilitolewa katika Mkutano wa Dartmouth uliofanyika mwaka 1956. Siku hizi akili bandia ni nguvu muhimu zinazohamasisha wimbi jipya la mageuzi ya kisayansi na ya viwanda, nayo inaleta athari kubwa katika sekta mbalimbali duniani, zikiwemo maendeleo ya kiuchumi, ubunifu wa kisayansi na maendeleo ya kijamii na kadhalika.
       Shanghai ni mojawapo kati ya maeneo yanayoongoza maendeleo ya akili bandia nchini China, na imefanikiwa kuandaa makongamano matatu ya akili bandia ya duniani tangu mwaka 2018.

Maudhui ya Jukwaa:
       Mada za jukwaa hili ni pamoja na: ujenzi wa Barabara wa Hariri (Silk Road) kwenye mitandao, maendeleo ya soko la data za kimataifa na utandawazi wa renminbi (RMB), maendeleo ya kisayansi ya data za lugha na utawala wa taifa wa kisasa na kadhalika.
       Wakati wa mkutano, Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU) kitafanya mijadala ya kiwango cha juu kwenye meza ya mviringo pamoja na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Maarifa ya Huashu ya China na taasisi nyingine. Wataalamu wa nchini na nchi za ng’ambo watajadiliana na kutoa mashauri na mapendekezo kuhusu mada maalumu, kama vile ubunifu wa akili bandia, maendeleo ya akili bandia na mkondo mpya wa elimu ya lugha za kigeni, maendeleo ya kozi za akili bandia na mafunzo ya kimataifa kwa watu wenye uwezo na zinginezo.
       Kampuni husika zitafanya maonyesho kuhusu akili bandia katika jukwaa hili na kuwaonyeshea wataalamu na watazamaji wa kawaida mafanikio mapya ya teknolojia na huduma ya bidhaa zao.

Gawanya:
Loading...

Soma Zaidi