KUIHUSU SISU

Katika wito wa, "Uadilifu, uaminifu, maono ya hekima na elimu pana, (格高志远学贯中外)” Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Shanghai (SISU) ni kituo maalum cha taaluma za kimataifa. Chuo hiki kinasifika kwa ajili ya asili na malengo yake ya kufunza wataalamu na viongozi wa kimataifa wa siku zijazo katika nyanja mbalimbali. Nia ni kuwawezesha viongozi hawa kukabiliana na masuala makuu ya nyakati za sasa.

HISTORIA YETU

mwanzo wa historia yetu ni Desemba 1949 wakati Shule ya Kirusi ya Shanghai (Shanghai Russian School) iliyokuwa tawi la Chuo Kikuu cha Mapinduzi cha Wananchi wa China Mashariki (Shanghai Russian School affiliated to East China People’s Revolution University) ilipoanzishwa. Hii ni mojawapo ya taasisi za kwanza kabisa nchini China ambamo lugha za kigeni zilifunzwa. Mhadhiri mkuu mwanzilishi wake ni Jiang Chunfang, msomi maarufu wa utafsir wa Kirusi ambaye pia aliongoza uchapishaji wa Encyclopedia of China.

Tangu mwanzowe, SISU imekuwa maskani ya kuvutia kwa wasomi maarufu wa kufundisha na kukukuza taaluma, baadhi wakiwa ni Fang Chong, Lu Peixian, Ling Dayang na Xu Zhongnian, ambao wanatajika kama ukwasi wa chuo hiki kikuu katika rasilimali zake kielimu.

WASOMI MAARUFU

SISU ni chuo kikuu ambacho kimejikita kimataifa na katika daraja la juu nchini China. Hivyo basi, SISU imefanikiwa kukuza taaluma nyingi teule huku lugha na fasihi zikiwa ndizo nguzo zake za kati.

Ufanisi wake mkubwa katika kuanzisha na kudumisha viwango vya juu vya taaluma kati ya vyuo vikuu, SISU inafadhiliwa kutoa masomo kumi maalum ya kitaifa na masomo sita ya taaluma muhimu zaidi Shanghai – yote haya yakiwa ni nyongeza katika taaluma zetu tatu muhimu za kitaifa -  tukiwa kitovu cha kitaifa cha shahada ya kwanza (undergraduate) ya lugha za Ulaya Magharibi.

Kila mwaka na hasa katika miaka ya hivi karibuni, SISU imezidi kuimarika na kukuza  shahada za lugha kufikia lugha arobaini hivi sasa, huku pia idadi ya shahada za uzamili na udaktari zikiongezeka pakubwa na hivyo kuudhibitisha muundo timilifu wa elimu.

Taasisi ya Uzamili ya Ufasili na Tafsiri  (Graduate Institute of Interpretation and Translation - GIIT) ya SISU ilituzwa na Chama cha Kimataifa cha Wafasiri wa Mikutano (International Association of Conference Interpreters – AIIC) kuwa ndiyo taasisi bora zaidi ya wafasiri. GIIT ndiyo taasisi ya pekee barani Asia, na ni mojawapo ya taasisi 15 tu zilizo na taaluma ya vyuo vikuu ulimwenguni.

UBORA WA UTAFITI

Katika kuujibu wito wa "kuuwasilisha ulimwengu mzima China" na "kuiwasilisha China ulimwenguni kote," SISU imefikia nafasi ya kipekee hapa China katika utafiti wa lugha, isimu na masomo ya kidiplomasia. Tuweza kulitegemea shehena letu lenye lugha mbalimbali na rasilimali anuwai, tunapohitajika kujibu masuala au kuhudumia mikakati ya kitaifa na ya kanda, kwa vile tuna zaidi ya taasisi na idara sabini za utafiti na uwezo mkubwa kitaaluma wa kutoa ushauri wa sera za lugha, mikakati ya kidiplomasia na maoni kuhusu China. Taasisi hizi zinachangia tafiti kabambe na pia zimejitoa kuikuza elimujamii nchini China.

Kwa sasa, SISU huchapisha majarida 13 maarufu sana ya taaluma yanayohaririwa kwa ustadi mkubwa. Miongoni mwao kuna the Journal of Foreign Languages  linalofadhiliwa na Shirika la Taifa la Elimujamii (China’s National Social Science Foundation) ambalo ni la kipekee la masomo ya isimu na lugha kati ya majarida thelathini bora ya elimujamii katika vyuo vikuu nchini China.

SISU ULIMWENGUNI

Kipaumbele cha SISU kimaendeleo ni kuwawezesha wanafunzi wake kuwa na mitazamo ya kiutandawazi na kushikilia juhudi za kuendelea kuukuza uwezo huu hususan kuwakuza wakiigiliana na tamaduni mbalimbali. Ushirikiano na zaidi ya vyuo vikuu 400 na pia na taasisi zingine 60 umeshaanzishwa katika mataifa na maeneo mbalimbali. Vile vile, uhusiano wa mzuri baina yetu na mashirika ya kimataifa yakiwemo Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Ulaya (EU) unadumishwa.

Kuna chapa kadha wa kadha za vitabu vya Kichina cha Mandarin (yaani lugha rasmi ya taifa), tulizozitunga na kuchapisha ili zitumiwe na wageni wasio Wachina na hii iwe ni njia moja ya kuendeleza ubadilishanaji wa kitamaduni baina ya Wachina na walimwengu wengineo. Kila mwaka sasa kwa muda wa miaka mitano iliyopita, wanafunzi wa kimataifa wapatao 4000 walisajiriwa katika programu zetu za lugha ya Kichina, kama vile, katika shahada 9 nyinginezo na katika Taasisi za Confucius (Kǒngzǐ) barani Asia, Afrika, Ulaya, Amerika Kaskazini na Amerika Kusini.

VIFAA VYA ELIMU VYUONI KWETU

SISU ina matawi mawili, yaani, Hongkou na Songjiang. Kwa jumla kuna eneo la hekta 74.7. Ingawa matawi haya ni chuo kimoja chenye uhusiano wa karibu sana, kila tawi lina sifa zake maalum na maarufu.

Maktaba ya SISU ni mmoja wa wanachama watatu wakuu wa CALIS (China Library Consortium of Foreign Studies). Maktaba hii inahifadhi vitabu zaidi ya milioni moja – zaidi ya nusu yake vikiwa katika lugha za kigeni- na zaidi ya nyaraka milioni 1.4 za elektroniki.

SISU inamiliki vifaa vya hali ya juu vya utafiti. Hivi ni pamoja na mitambo ya kipekee duniani ya ukalimani, vifaa vya setiliti vya kupokea habari na maabara ya lugha na isimu. Rasilimali tajika za elektroniki zenye midia anuwai ya taaluma za kimataifa inapatikana SISU ili kutumikia mahitaji ya kufundisha na kufanya utafiti katika nyanja husika.

USHIRIKA WA KIJAMII NA UJIRANI MWEMA

Kwa moyo wa ujirani mwema, na kwa kutumia ujuzi wa kitamaduni na wa kitaaluma, vitivo na idara za SISU na kupitia kwa wanafunzi wake, hujitolea kwa moyo wote kutoa huduma zao katika mikutano ya kimataifa, hafla, michezo na matukio mengine ya wahusika wenye lugha mbalimbali. SUSU pia ipo mstari wa mbele katika kuendeleza elimu ya lugha za kigeni nchini China. Shirika la Elimu ya Lugha za kigeni la Shanghai (Shanghai Foreign Language Education Press-SFLEP), lililo shirika la SISU ni moja mashirika bora zaidi ya habari ya vyuo vikuu nchini China. Kama ishara ya ubora wetu nchini, SFLEP ilichukua nafasi ya kwanza katika lugha na fasihi kwenye Chinese Book Citation Index ya mwaka 2015.

Tumejitolea kuwapapokeza wanafunzi wetu elimu-utu, timilifu na iwawezeshayo kufikiri kitandawazi, kitaaluma na kudumisha mawasiliano ya maelewano yanayovuka mipaka ya tamaduni.

Katika kipindi cha miaka 70 na zaidi iliyopita, wahitimu wetu wamekuwa wakichangia maendeleo kiuchumi, kitamaduni na kijamii China huku wakikuza maigiliano ya kirafiki baina ya watu duniani kote.

Gawanya: