Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Tamthilia ya Harry Potter III


01 January 2022 | By 宋艺婷 Monika | SISU

  • Harry Potter

  • Voldemort

Voldemort: Lucius, rafiki yangu aliyependa kujificha. Nasikia kwamba hujaacha njia kongwe? Ingawa unaonyesha heshima wako, lakini uko tayari kuongoza harakati za kuwatesa Muggle. Lakini, Lucius, hukujaribu kunitafuta! Hata mara moja! Kwa nini hukutumia nguvu zako kumsaidia Bwana wako?

Lucius: Bwana wangu, nataka kupata ujumbe wako wakati wote! Kama nilijua ujumbe wako wowote, nilikuwa nimekwenda kwako. Hakuna vitu vilivyoweza kunizuia! Hakuna!

Voldemort: Lakini ulikimbia wakati Mlafi mmoja wa Kifo alipotoa ishara yangu? (Lucius hasemi neno tena.) Najua vitu vyote, Lucius. Lakini natumai unaweza kutoa huduma yako kwa uaminifu siku za mbele.

Lucius: Bila shaka, Bwana wangu, bila shaka! Asante sana kwa rehema yako!

 

(Voldemort aliendelea kutembea.)

 

Voldemort: Lestranges hawakuja hapa bado, kwa sababu sasa wanatiwa ndani ya Azkaban. Walitiwa ndani lakini hawakunisaliti. Tunapofungua Azkaban, wataheshimiwa na kila mmoja wenu. Mtu yeyote aliyeonyesha uaminifu wake kwangu atastahili kuheshimiwa na kila mmoja. Na Crabbe? Goyle? Mnanisikia? Natumai mtatenda vizuri baadaye.

 

Crabbe na Goyle: (waliinama) Ndiyo, Bwana! Kabisa!

 

(Voldemort alikaribia Harry.)

 

Voldemort: Harry! Nusura nisahau uko hapa. Nataka kukujulisha marafiki zangu. Lakini nasikia siku hizi unajulikana sana kama mimi. Mtoto aliyeishi bila kuuawa. Maajabu yako yamelundikwa na uwongo, mwanangu. Nifichue siri hii, ehh? Nifichue vipi nilipoteza nguvu zangu... Kwa sababu ya mapenzi! Mnaona Lily Potter alipompa mwana wake wa pekee maisha yake, alitoa ulinzi mkubwa kabisa kwake pia. Sikuweza kumgusa mtoto huyu. Hii ilikuwa uganga kongwe, ambao ningaliweza kujua. Lakini sasa si muhimu tena! Vitu vyote vimebadilika! Ninaweza kukugusa sasa! Hahahaha! (Voldemort aligusa kovu ya Harry, na Harry aliumwa na kichwa sana. Kisha Voldemort aligeuka nyuma na kumpa Harry uhuru kwa fido.) Chukua fido yako, Potter! Nimekuambia, Potter! Chukua fido yako! Umeshajifunza kupigana kwa fido, ehh? Kwanza, tunatakiwa kuinamana. Nidhamu inahitajika, Harry. Dumbledore hatatarajia kuona hukushiki, sivyo? Nimesema uinama! (Voldermort anaminamisha Harry.) Hivyo ni bora zaidi. Crucio! Crucio! (Harry anateseka sana.) Mtoto mzuri, Harry! Wazazi wako watakuwa na fahari kwako, hasa Muggle-mama yako mbovu.

Harry: Expelliar...

Voldemort: Expelliarmus! Nitakuua, Harry Potter! Baada ya usiku huu, watu hawatashuku nguvu zangu! Baada ya usiku huu, wakiongea kuhusu wewe, watakumbuka vipi utakuwa uliniomba kukuua! Na mimi, Bwana mwenye rehema, nitakuwa nilikidhi haja yako. Nyanyuka! (Harry ananyanyuka na kutaka kupata fursa ya kukimbia na kujilinda. Anajificha nyuma ya mwamba.) Usigeuke nyuma, Harry! Nataka unione nitakapokuua. Nataka kuona nuru iondoke kutoka macho yako!

 

(Harry anatoka na kusimama mbele ya Voldemort.)

 

Harry: Haya, kama ulivyopenda. Expelliarmus!

Voldemort: Avada Kedavra!

 

(Harry na Voldemort wanatoa uganga wakati huo huo. Uhusiano fulani wa ajabu unatokea baina ya fido zao mbili. Wazuka wa Cedric, Lily Potter na James Potter walitoka kwa sababu ya uhusiano huu. Lily Potter na James Potter wanakwenda kwa Harry.)

 

James Potter: Harry, wakati fido zimeshaunganishwa, lazima urudi kwa ufunguo ule uliokupeleka hapa! Tunaweza kukazana na kukupa muda wa kujitayarisha. Lakini muda si mrefu, unafahamu?

Cedric: Harry, tafadhali uniletee maiti yangu. Mletee baba yangu maiti yangu.

Lily Potter: Iache, Harry. Mwanangu, uko tayari. Iache, iache!

 

(Harry anaacha kuendelea kuunganishwa na Voldemort. Wakati huu, uhusiano haujapotea, na pia kuna ukungu wingi. Harry anakimbia kwa maiti ya Cedric na ufunguo ule kwa kasi. Mara anagusa ufunguo, anatoweka na kupelekwa kwa shule ya Hogwarts.)

 

Voldemort: Hapanaaaa!!!

 

(Mwisho)

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi