Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Tamthilia ya Harry Potter I


01 January 2022 | By 宋艺婷 Monika | SISU

  • Hogwarts

  • Voldemort

 Mwandishi: J.K. Rowling

 

Utangulizi

Katika kozi ya Tamthilia ya Kiswahili, tulipewa kazi ya nyumbani ya kupendeza, yaani kutafsiri na kubuni hadithi zetu wenyewe kutokana na filamu au hadithi tulizopenda na kuzionyesha kwa njia ya tamthilia. Bila shaka ilitupasa kufanya mabadiliko kadhaa yafaayo wakati wa kubuni. Nilichagua onyesho la mchakato wa ufufuo wa Voldemort katika filamu maarufu ya Harry Potter, ambayo inajulikana sana kwa ujenzi wa dunia ya mazingaombwe na imetafsiriwa kwa lugha 73 ulimwenguni.

 

Katika onyesho hili, Voldemort alifufua na kufanya maarifa kupambana na Harry Potter, mtoto ambaye ilisemekana alimshinda Voldemort na kutokufa katika janga kubwa. Voldemort alitaka kudhihirisha kwamba yeye ni mchawi mwenye nguvu kubwa kabisa, na Harry ni mtoto mwenye bahati tu katika ajali ya miaka kumi na tatu iliyopita. Harry alikuwa akishiriki katika Mashindano ya Kikombe cha Moto. Lakini alipelekwa huko alipokuwapo Voldemort kwa sababu ya hila ya Mlafi wa Kifo. Katika hali hii ya hatari, Harry anayekabiliwa na maadui wengi wenye nguvu atafanya nini kujilinda na kujiokoa?

 

Onyesho la Ufufuo wa Voldemort

Harry Potter na Cedric Diggory wanapofungua macho wanastaajabu. Kwa sababu walikuwa wakishiriki katika Mashindano ya Kikombe cha Moto shuleni, na hawajui kwa nini wametoka shuleni na kuingia makaburi ya kigeni. Kuna giza tupu, na upepo unavuma kwa nguvu. Harry hawezi kuona kitu chochote ila kivuli cha nyumba kongwe kwenye kilele cha kilima.

 

Harry: Tuko wapi?

Cedric: Kuna mtu yeyote aliyekuambia kuwa Kikombe hiki ni ufunguo uliotupeleka mahali fulani?

Harry: Hapana. Labda sasa tunakabiliwa na mojawapo kati ya changamoto katika mashindano.

Cedric: Sijui. Lakini bora tutoe fido zetu, unaonaje?

Harry: Ndiyo. (Kuna kelele kidogo.) Mtu fulani anatukaribia!

 

(Mtu mfupi mgeni anakuja. Amevaa joho kubwa jeusi linaloweza kufunika uso wake. Mwili wake hauonyeshwi vizuri vilevile. Inaonekana kwamba labda anakumbatia mtoto mchanga au kitu kingine. Harry anaanza kuumwa na kichwa chake sana.)

 

Voldemort: Mwua mtu mwingine.

Wormtail: (kwa upande wa Cedric) Avada Kedavra!

 

(Cedric amefariki. Harry hawezi kuamini macho yake. Lakini punde si punde, anafungwa na mtu huyu mgeni kwenye mwamba. Wakati huo Harry anatambua kuwa kumbe huyu mwanamume ni Wormtail ambaye aliwasaliti wazazi wake. Wormtail anahangaika huku na huko na kufanya matayarisho kwa kutumia fido. Alitoa chungu kikubwa cha jiwe na kukijaza maji. Na chungu inazungukwa na moto mkali.)

 

Voldemort: Haraka!

Wormtail: (kwa hofu) Zi...ziko tayari, Bwana wangu.

 

(Wormtail anakiangusha kitu fulani kilichokumbatiwa naye kwenye chungu. Halafu anachukua fido yake, kufunga macho na kuanza kuzungumza gizani.)

 

Wormtail: Mfupa wa baba ulitolewa bila kujua. Utampa mwanao maisha mapya.

 

(Unatokea ufa kwenye kaburi moja karibu na Harry. Mfupa mmoja unapanda juu, na unaanguka kwenye chungu baadaye.)

 

Wormtail: (kwa hofu sana) Nya...ma ya mtumishi ili...tolewa kwa kujitolea. Utamfufua Bwana wako.

 

(Wormtail anachukua jambia kwa mkono wake wa kushoto, kisha anakata mkono wake wa kulia kwa jambia, mkono ukaanguka chunguni.)

 

Wormtail: Damu ya adui ilitolewa kwa nguvu. Utamfufua adui wako.

 

(Wormtail anakwenda kwa Harry. Anamdhuru kwa jambia kwa kusudi la kupata damu yake. Halafu anaimwaga damu ndani ya chungu. Chunguni maji yamekuwa rangi ya nyekundu na vitu fulani vinapiga kelele kubwa. Wormtail anatetemeka sana pembeni, na mkono wake unatoka damu. Ghafla mtu mwembamba, mkatili na mwovu ananyanyuka. Bwana Voldemort amefufua.)

 

  

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi