Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China
Soma Zaidi
Toleo la Tafsiri: Safari ya Milimita Elfu Tisa
19 December 2021 | By 斯瓦希里语(sw) | SISU
Safari ya Milimita Elfu Tisa ni kitabu kilichotungwa kwa watoto mwaka 2020 baada ya mlipuko wa virusi vya COVID-19 kwa madhumuni ya kuwajulisha watu jinsi ya kujikinga na virusi, kujitunza vizuri tulipokabiliana na janga hilo.
Hii ni toleo moja lililotafsiriwa na mwanafunzi mwetu. Ukitaka kujua mengi zaidi kuhusu hadithi hiyo, tafadhali ubonyeze kiungo hiki:
https://book.douban.com/subject/35044430/
Safari ya Milimita Elfu Tisa
Makala/Zhang Xiaoling
Picha/Yan Qing
Tafsiri/Najum
Page 4.
Nusura watu hawaonekani mitaani.
"Nataka kutoka nje na kucheza sana." Xiao Po anasema.
"Sasa haifai. Siku za karibuni zitafaa." Dada anaangalia nje, kisha anaangalia nyumbani, "nyumbani kwetu pia ni pakubwa."
Xiao Po anakunja pua lake. Mbona mahali hapa padogo panaitwa pakubwa na dada?
"Basi tupapime, unasemaje?" Dada anasema.
Page 5.
Xiao Po anapima umbali kwa makini kutoka mlango hadi roshani.
"Kwa jumla ni umbali wa rula thelathini. " Xiao Po anarepoti kwa sauti kubwa.
"Rula moja ina urefu wa sentimita thelathini, na thelathini zidisha thelathini, ni sentimita mia tisa." Dada anahesabu kwa makini kwenye karatasi.
"Ni wingi sana!" Dada na kaka mdogo wanastaajabu. "Sentimita mia tisa ikibadilika kwa milimita.." Dada anavuta pumzi nzito, "itakuwa milimita elfu tisa!"
Page 6.
"Lo! ", Xiao Po anasema, ambaye amejifunza kuhesabu hadi mia moja tu hivi karibuni, "Kama mimi ni siafu ndogo, mahali hapa ni pakubwa kama dunia kwangu! "
Maneno ya Xiao Po yameanguka tu, sakafu inaanza kuenea mbali, dari linainuka na kuelekea anguni, dafodili kwenye meza inakua na mwishowe kuwa mti mrefu.
Dada na kaka ndogo wanashangazwa.
"Ni nini kilichotokea?" Dada anamwuliza.
"Sijui." Xiao Po anasema. "Labda ni nguvu za uchawi. "
"Ah! Shangazi Gu alisema kwamba ameweka chakula cha mchana nje ya mlango, lakini..."
Page 7.
Wanawezaje kuvuka umbali huu wa milimita elfu tisa na kupata chakula cha mchana? Hii ni tatizo kubwa.
Xiao Po anaamua kuchora ramani kwanza, halafu anamwomba dada achore alama za mahali.
Haya, safari yao ianze——
Page 8.
Kwanza, wanapaswa kwenda kasri ambaye imejengwa kwa matofali ya kuchezea, kwa sababu chombo pekee tu cha safari kimewekwa pale.
Puku wa kichezo anaofumwa kwa manyoya ni mflame wa kasri hiyo. Anawatendea watoto hao wawili kwa ukarimu sana. Anawatoa mali zake zote.
"Hatuhitaji baraka." Dada anasema polepole, " Ikiwezekana, ungependa kutuazima gari lako?"
Page 9.
"Bila shaka ninapenda!" Mfalme anazungukazunguka kwa sababu ya msisimko. Anasugua mikono yake, huku akiwomba chura achukua gari hapa.
Kwa masikitiko, gari hilo linakosa gurudumu moja.
"Ninawapendelezeni kwenda Mbuga ya Usahaulifu." Mfalme anasema, “Vipoteavyo kwa sababu zisizoeleweka hutokeza pale.”
"Mbuga ya Usahaulifu?" Xiao Po na dada wanatazamana.
Ramani yao haiwaonyeshi mahali hapo.
Mfalme anawaonyesha upande wa sofa kwa kidole.
Page 10.
Bila kutarajia, Mbuga ya Usahaulifu inajificha chini ya sofa, ambapo mavumbi yamejaa. Mara wanapoingia ndani, wanaanza kupiga chafya bila kutua.
"Atishoo --- matofali yangu ya kuchezea!" Xiao Po anashangilia.
"Atishoo --- jigswa yangu!" Dada anashangilia pia.
Wanagundua soksi moja, gololi na kibanio vilevile.
Page 11.
Xiao Po anaokota kibanio hicho na kukinusa.
"Kina harufu ya mama." Xiao Po anasema.
Dada anakinusa pia. "Ni kweli, hii ndiyo harufu ya mama."
Wameachana na mama kwa siku kumi. Harufu hiyo ni muhimu sana kwao. Wanakinusa mara na mara nyingine kwa sababu wanaogopa kuisahau.
Page 12.
Wanataabika sana kuweka gurudumu kwenye gari. Kama Baba yao akikuwepo sasa, ni hakika watamaliza kazi yao mara moja. Lakini baba yao hayupo hapa. Baba na mama wapo hospitalini, hawawezi kurudi nyumbani.
"Si kazi ya kuweka gurudumu tu?" Dada anasema, "Ni rahisi kuliko kutandika vitanda, ni rahisi kuliko kukuosha, ni rahisi kuliko kuchukua juhumu ya mama...Jambo lolote lina mara yake ya kwanza."
Xiao Po hawezi kukubali maneno ya dada vingi zaidi.
Xiao Po anafanya jitihada kubwa kuweka gurudumu kama baba.
Halafu, wanachukua kibanio na kukiweka kwenye kiti ndani ya gari. Kwa njia hiyo harufu firidi wanayofahamu inaweza kuwaandama njiani. Gari hilo inawakumbusha gari lile kubwa la baba.
Page 13.
Pengine kwa sababu ya ukosefu wa kifaa, gari hili linatetemka linapokwenda mbio. Lakini haidhuru, mwendo wao umeongezeka. Wanapovuka msitu unaoumbwa na miguu ya meza na viti, muziki unakuja kutoka anguni.
Page 14.
Sauti ya baba ni nzito yenye hema, lakini hii ndiyo sauti ya baba, pia yenye furaha kama zamani.
"Baba, unaweza kutambua kutoka simu kuwa mimi na dada tumekuwa ndogo!" Xiao Po anarukaruka kwenye meza, "Nyumba yetu imebadilika kuwa mkubwa sana, ina upana wa milimita elfu tisa!"
"Hii ni ajabu sana!" Baba anasema huku akicheka, "Je, mmekula chakula cha mchana?"
"Tupo njiani kwetu kuchukua chakula cha mchana." Dada pia amepanda juu, anajaribu kutumia kiimbo kipevu, "Baba, tunaendelea vizuri. Kila siku nafagia sakafu, natandika kitanda, hata nilimwosha Xiao Po jana."
"Dada anasema uwongo!" Xiao Po anasema huku akicheka, "Hakutandika kitanda leo! Alisema kuwa kwa vyovyote atalala kwenye kitanda chake leo usiku!"
Baba anasema: "Xiao Po, unatarajiwa kumtunza dada vizuri pia."
"Bila shaka," Xiao Po anasema, "Ni jukumu kwa wavulana kuwachukua wasichana!"
Sauti ya baba inasimama, halafu anasema kwa upole:"Wanangu, mjitunze vizuri. Baba na mama tutarudi nyumbani majira ya machipuko yanapokaribia"
Page 15.
Baada ya kuzugumza na baba kwenye simu, unyamavu unaingia nyumbani. Hata kwa dakika kadhaa chakula cha mchana kimesahaulliwa na watoto hao.
"Ninakumbuka mama yangu." Xiao Po anasema kwa sauti ndogo. Pua lake linabadilika jekundu.
"Watarudi nyumbani siku za karibuni." Dada anasema kwa uhakika, huku akijaribu kujizuia kutokwa na machozi.
Dada anawambia Xiao Po ashike vipande viwili vya baraka ili washuke salama kwenye ardhi.
Shauri la dada linamsahaulisha Xiao Po huzuni yake. Anachukua baraka moja kwa furaha, halafu anafuata mfano wa dada. Anashika vipande viwili imara, kisha anaruka nje.
"Wow——" Watoto hawa wawili wanapaa hewani.
Page 16.
Wanaelea hewani kwa wakati wingi kabla wanapoona ardhi.
Wanashuka katika mzingile wa viatu.
"Xiao Po, jihadhari na chini!"
"Lo! Sitakwama!"
Page 17
"Don Don Don!" Nani anapiga hodi?
"Xiao Mei na Xiao Po, mpo nyumbani?" Sauti ya Shangazi Gu inakuja kutoka nje.
"Shangazi Gu, tupo!" Dada anasema.
"Ninaona kuwa bado hamjachukua chakula cha mchana. Nina wasiwasi kwenu." Shangazi Gu anasema.
"Tutakichukua haraka." Xiao Po anasema.
"Mnaendelea vizuri? "
"Vizuri sana!"
"Basi sasa tuagane, nitarudi kuwatembeleeni baada ya muda kidogo."
"Asante sana Shangazi! "
Page 18.
Dada na Xiao Po wanatumia nguzu zao zote, mwishowe wanafanikiwa kufungua mlango.
Jua kali na hewa safi vinawakaribisha.
Ghafla, dada na Xiao Po wanakua na kukua, mandhari ya nje pia imebadilika kuwa kama zamani.
Chakula kinachopelekwa na Shangzi Gu kimewekwa kwenye kabati ya viatu mbele ya mlango. Joto lake bado lipo.
Dada pia anagundua kuwa machipuko machache kijani yametokeza katika chungu cha maua.
"Xiao Po uangalie, coreopsis imechipuka. "
Kumbe, Majira ya machipuko yamerudi japo binadamu hawawezi kujua wakati hususa.
Basi muda fupi baadaye baba na mama watarudi vilevile?
Press Contact
SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs
Tel : +86 (21) 3537 2378
Baruapepe : news@shisu.edu.cn
Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China
