Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Hadithi za Vinyozi wa SISU


03 May 2022 | By 宋艺婷 Monika | SISU

Wakati tunapokumbwa na janga la uviko-19, nywele zetu ni ndefu zaidi siku hadi siku. Tatizo hili linaweza kutatuliwa vipi? Wanafunzi na wafanyakazi chuoni waliunda “kikundi cha vinyozi cha SISU”, na kutusaidia kutatua tatizo hili.

Katika kampasi ya Songjiang, walimu na wanafunzi 16 waliunda “kikundi cha vinyozi cha SISU”. Kwa misaada ya wasaidizi saba, kikundi hiki kimewahudumia wanafunzi 200 hivi mwezi uliopita.

Mwanafunzi Song Keyuan kutokana na Kitivo cha Sheria ni nguvu muhimu katika kikundi cha vinyozi. Amewasaidia wanafunzi 36 kupunguza nywele hadi sasa. Alikumbuka kwamba siku moja, alisimama tu na kunyoa nywele za wanafunzi 13 kuanzia saa saba alasiri hadi saa moja jioni. Alieleza kwamba ingawa amechoka sana, kunyoa nywele kumekuwa fuhara yake wakati wa janga la uviko-19, “Baada ya mazoezi ya siku kadhaa, ufundi wangu umeboreshwa kwa kiwango kikubwa ukilinganishwa na ufundi wangu wa siku ya kwanza. Ninawapunguzia wanafunzi nywele, pia walinifundisha mambo fulani.”

Mwanafunzi Zhao Zirui kutokana na Kitivo cha Usimamizi wa Biashara cha Kimataifa sasa ni kinyozi wa Bweni la 32 katika kampasi ya Songjiang. Zhao alisema kuwa uviko-19 ulipolipuka mjini Wuhan, alikuwepo huko, kwa hiyo anafahamu mahitaji ya wanafunzi baada ya kufungiwa kwa muda mrefu. Anaamua kuwapunguzia nywele kwa bure, ili kuwasaidia wanafunzi kama anavyoweza. Baadaye, wanafunzi wengi walikuja kwa Zhao kwa ajili ya kupunguza nywele, hata wakiwemo mwanafunzi mgeni kutokana na Iran na mwalimu Hu Zhengming, na waliridhika naye sana.

Sasa watu wengi zaidi wanashiriki katika kikundi cha kinyozi cha SISU. Kikundi hiki chenyewe pia kinaandaa mafunzo ya kuboresha ufundi wa vinyozi wa kunyoa nywele. Mafunzo yanatolewa na walimu au wanafunzi wenye maarifa nyingi zaidi, ili kuwasaidia vinyozi wapya kuinua uwezo wao wa huduma za kunyoa nywele.

 

Katika Bweni la Tatu katika kampasi ya Hongkou, pia kuna kinyozi mwema.

Yeye ni mfanyakazi Wang kutokana na mjini Huangshan mkoani Anhui. Amefanya kazi katika SISU kwa miaka 20, na kuwajibika kazi za upishi. Ni bora tujue kwamba Wang aliwafundisha karibu nusu ya wapishi wa maandazi kantini. Kwa kawaida aliamka saa nane hivi alfajiri kila siku na kuanza kufanya manunuzi ya vitu kantini na kazi nyingine. Alijua harakati hiyo ya kupunguza nywele kutokana na mazungumzo na wafanyakazi wenzake. Wang anapenda kunyoa nywele, na aliwahi kuwapunguzia familia zake nywele. Wang alisema moja kwa moja kwamba: “Walimu na wanafunzi wana mahitaji, na nina ufundi. Kwa hiyo, nilijitolea kushiriki harakati hii. Ninapenda kuwahudumia wengine.”

Wanafunzi waliokuja kwa Wang walieleza kuwa walikuwa na wasiwasi mwanzoni kwa ufundi wa Wang, lakini waliridhika sana baada ya kupungunziwa nywele.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi